Finally naanza upya maisha ya kujitegemea nikiwa mfukoni nina laki 8 tuu



Ingekua mimi ningemshauri atoke dar aende visiwani akakusanye samak au dagaa akaushe alete mjini..kifupi ajitupe visiwani mazima..asipoudoble mtaji in a 3mths bas tena!
 

Hongera! Sio sawa kuishi chumba, jiko, sebule all in one compartment lakini sisi wengine tulianzia huko, siuiti uanaume though. Ni kukubaliana na hali yako then unapambana nayo.
 
Hongera! Sio sawa kuishi chumba, jiko, sebule all in one compartment lakini sisi wengine tulianzia huko, siuiti uanaume though. Ni kukubaliana na hali yako then unapambana nayo.
Na hawa wadogo zetu tuwahimize wajichanganye tu kitaa
 
Laki 8 ni hela nyingi sana. Tena kodi hudaiwi.

Usinunue chakula migahawani, nunua unga,mchele, dagaa, maharage weka ndani. Acha pombe na mademu wewe pambana na maisha tu, utafika mbali.
 
Ingekua mimi ningemshauri atoke dar aende visiwani akakusanye samak au dagaa akaushe alete mjini..kifupi ajitupe visiwani mazima..asipoudoble mtaji in a 3mths bas tena!
Inawezekana kabisa maana ilala sokoni pale hakuna bidhaa iliokuwa ina gharama kubwa kama dagaa 1kg@6000. Pia vitunguu swahumu 1kg@5000 samaki wakavu sikupata data
 
Inawezekana kabisa maana ilala sokoni pale hakuna bidhaa iliokuwa ina gharama kubwa kama dagaa 1kg@6000. Pia vitunguu swahumu 1kg@5000 samaki wakavu sikupata data
Ukipata soko la samaki wakavu hawasumbui kbs kuuza ukileta wa 700k jua unaondoka na 1.4
 
Sisi waafrika tuna laana yetu aisee,yaani kinachosifiwa hapo hata sikielewi mkuu,yaani kumbe ili uonekane mwamba inabidi uanzie majalalani? Ndo maana waafrika haturithishi mali kwa watoto ili waziendeleze kama wafanyavyo waarabu na wahindi,sio ajabu kukuta don wa kiafrika hataki kumpa mwanae hata laki ya mtaji kwasababu anaamini ili uonekane mwamba lazima uanzie matopeni,daah tuna tabu sana ngozi nyeusi
 
Mkuu point hapa tunaongea huna maisja wazaz ni maskini nn kifanyike? Unapenda kukaa kwenu umri wa 34 kisa tu huba direction? Kwann usianze maisha ya chin ukatoka kwenye comfort zone? Ndo maana walotusua Africa wachache mnoo aUnatakiwa KUJIKANA NAFSI JOMBAA
 
Ukipata soko la samaki wakavu hawasumbui kbs kuuza ukileta wa 700k jua unaondoka na 1.4
Nadhani atasoma hapa kila kitu, Hiyo pesa ni ndogo sana akiifanyia mambo tofauti. Yaani akitikisa tu kiberiti kwisha habari yake anaweza kimbia hadi hiko chumba alicholipiwa sababu ya njaa. Ila ni nyingi akiiwekeza.
 
Nimekuelewa mkuu,lakini ulivyoandika mwanzo ni kama unafurahishwa sana na watu kuanzia matopeni na kuwabeza wanaoanza maisha level nzuri,

Hiki kitu cha kuanzia sifuri sikipendi sana na nahisi mimi nitakuwa wa mwisho kwenye gen yangu,

Mimi naishi haya mambo nayaona,kuna watoto wa wafanyabiashara wengi sana wameajiriwa wanalipwa laki 7 kwa mwezi,na wengine wamejiajiri wana viduka vya pipi na viberiti mtaani lakini baba zao wana networth ya more than 10B na biashara za kueleweka mpaka unashindwa kuelewa shida nini?
 
๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…..sipendi kbs kutegemea hela za mzazi mm
 
Daahhhh nikiangalia jinsi ambavyo nikishika Millioni 1 inavyoyayuka kama barafu ndani ya wiki 3 hadi 4 wewe hiyo laki 8 nakuonea huruma kwa kweli. Ila kwa kuwa wewe sio mimi na mimi sio wewe basi nakuombea dua ikidhi mahitaji ya mwanzo wako wa maisha. Nakutakia kila la kheri!

Sasa kwa mazingira ya Dar es salaam laki 8 sio hela hususan kama wewe ni muhitimu wa Chuo Kikuu. Unachotakiwa uachane na akili za Chuo kwa muda na uuvae umachinga au maisha ya mtaani ili hiyo pesa isikuponyoke ukarudi Square 1.

Una option mbili za kuanzia:
1. Kazi/Kibarua cha kukusaidia kukupa network, Channel za fani yako, chakula, kodi, bili, akiba na matibabu.
2. Biashara ndogondogo isiyohitaji "bizinesi plani" wala fremu. Ukileta usomi wako trust me you are doomed to fail na utajiona fala sana kupoteza the last chance. Jichanganye na wamachinga, wachuuzi nk ili upate cha kuanza nacho ambacho hakitakugharimu sana na hakichukui muda kuzaa matunda.

Either of the two, ALL THE BEST!!!

Baadae akili yako ikishatulia ndipo utaweza kupanga na kuchagua.

Epuka sana Shortcut na vitu vya bure, mara nyingi mwisho wake ni mbaya.
 
Nadhani atasoma hapa kila kitu, Hiyo pesa ni ndogo sana akiifanyia mambo tofauti. Yaani akitikisa tu kiberiti kwisha habari yake anaweza kimbia hadi hiko chumba alicholipiwa sababu ya njaa. Ila ni nyingi akiiwekeza.
Kuna akili hapo ya kuwekeza sasa๐Ÿ˜†๐Ÿ˜†๐Ÿ˜ฌmtu andika yako unajua kbs huyu yes๐Ÿคฃ(natania)
 
๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…..sipendi kbs kutegemea hela za mzazi mm
Swala sio hela hapo,swala ni kujifunza biashara ya mzee ili hata akiondoka iendelee kusogea mbele

Unajikuta hutaki kutegemea hela ya mzazi wakati ikitokea akafa unaanza kukesha bar mpaka hela yote ya mzee inaisha

Unaifakamia fasta utafikiri mzee atafufuka akurudishe matopeni kwako๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
 
Nadhani hyo laki na themanini ni kodi ya miezi 6,yaani 30 kwa kila mwezi ndio nilivyoelewa.
 
We huwezi kuja kuoa na kustick na ndoa yako...kama unayoandika hapa yana ukweli....huna akili ya kijituma..ndoa itakushinda mapema...labda ukitaka istick oa mwanamke mpambanaji sana..ukioa mkr anayesubiria kuachiwa hela kila siku ndoa chali...

Unamjua personally? Au unaandika kufurahisha nafsi yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ