Fiston Mayele kutimka Yanga

Fiston Mayele kutimka Yanga

Mayele kwa Africa sasa ni kama Dhahabu , kwa sisi tunaoangalia michezo vituo vikubwa kama Supersport ,BBC ,Canal nk wanaelewa ila ukiwa unashinda kwa Jemedari Saidi hautoelewa.
Cheki naye huyu mpambe wako ukikaidi utapigwa2 ye ikishafikaga maswala ya Yanga na kumsifia Mayele anapiga thumb up bila kujua ukweli wa hicho kitu

Hivi mnazijua dhahabu?

Au ni vijana wawili ambao mmeamua kuitukanisha dhahabu kwa kuifafanisha na vitu vya kijinga?
 
Magodoro yake hayafai kabisa yanaumiza sana mgongo na ukiamka asubuhi unakuwa umechoka sana najuta kufanya sub na mshikaji nikamwambia godoro langu yeye akaniachia la GSM
Nasikia yanaumiza utumbo
 
Yaani Mayele ni mpumbavu wa kiasi cha kuondoka timu kama Yanga, na kusajiliwa Orlando Pirates au Kaizer Chiefs kweli!!

Mayele bado yupo yupo sana Yanga. Na muda si mrefu ataongeza mkataba. Just wait and see. Msimu ujao ataendelea kutetema kama ilivyo kawaida yake.
Bro unajua boli kweli?
 

Kuna taarifa zinazosambaa kwa kasi mitandaoni kumhusu mshambuliaji kinara wa Yanga, Fiston Kalala Mayele kutimkia moja kati ya klabu ya Afrika kusini ikiwemo Orlando Pirates na Kaizer Chiefs.

Duru nyingine zinamuhusisha kutakiwa na vilabu vya Afrika Kaskazini. Hapo awali alihusishwa kwenda Al Hilal ya Sudan ila machafuko ya kisiasa yanatishia dili hilo kufanikiwa.

JE, YANGA ATASIMAMA BILA MAYELE?
Yaani aondoke TZ aende South? South hakuna mpira kule
 
Sema tanzania tunajua kupromote wachezaji na kuwafanya wajisikie nyumbani ukitoa maslahi sidhani kama kuna mchezaji huwa anatamani kuachana na vibe, lifestyle na culture ya kibongo.
Sisi ni wakarimu sanaa..mlete mzungu tuu ndio tulimnyanyapaa na wale wajomba zake maximo😆😆
 
Yap maana ndio sehemu pekee aliyobakisha kwa ajili ya kujipatia ulaji.

Huku kwenye magodoro soko limebadilika watu wamesanuka
Kwamba watu wanalalia pamba au?
 
Kama hii tetesi ikiwa kweli basi Yanga ipo kwenye ushindani mkali sana wa kumfanya Mayele aendelee kubaki
Africa anajichelewesha sana Mayele, hawa francophones ni rahisi sana kupenya kwenye soka la ulaya kupitia France na Belgium. Kwanini asiende zake huko mapema kabla umri haujamtupa mkono?
 

Kuna taarifa zinazosambaa kwa kasi mitandaoni kumhusu mshambuliaji kinara wa Yanga, Fiston Kalala Mayele kutimkia moja kati ya klabu ya Afrika kusini ikiwemo Orlando Pirates na Kaizer Chiefs.

Duru nyingine zinamuhusisha kutakiwa na vilabu vya Afrika Kaskazini. Hapo awali alihusishwa kwenda Al Hilal ya Sudan ila machafuko ya kisiasa yanatishia dili hilo kufanikiwa.

JE, YANGA ATASIMAMA BILA MAYELE?
huyo wanatakiwa wamuuze kwa dau kubwa sana, si chini ya bilioni mbili. ndo wamwachie.
 
Africa anajichelewesha sana Mayele, hawa francophones ni rahisi sana kupenya kwenye soka la ulaya kupitia France na Belgium. Kwanini asiende zake huko mapema kabla umri haujamtupa mkono?
Ila we jamaa wewe.

Yani hapo alipo bado unaona umri wake unaenda sawa na muda?

Wenzetu wa mambele wametuzidi sana kwenye vision ya mpira hususani linapokuja swala la kutaka kusajili.

Wanaposajili wachezaji hawaangalii matokeo ya mwisho ya mchezaji sijui ana goli 10 na assist 8, wao wanaangalia ubora wa mpinzani mpaka jamaa akafunga hizo goli 10.

Sasa we unacheza na Rivers, Mazembe ambao ni too low as fck halafu unataka kukaa mstari mmoja na watu kama Peter Shalulile, Hamza Khabba na Kahraba

Ukiona Al Ahly, Mamelody hawashoboki na mchezaji ambaye wewe kwenye lihi yetu hapa unamuona ni hatari ujue huyo kwenye level za wakubwa ni Zuchu tu.

Yani Al Ahly wakuone regular halafu zitoke Clubs za ulaya zishoboke na wewe, hiyo inawezekana vipi?
 
Tutamuongezea mshahara

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Maana yake mshahara unatakiwa uwe mrefu ili iwe kikwazo kwa Club inayomtaka isiweze kumudu.

Naogopa hata Azam anaweza kuwa mshindani mwenye asilimia kubwa ya kumsajili mchezaji huyo ila tatizo lipo kwa ile cabinet ya Tate Mkuu na wenzake.

Kama kwa Feisali walitishia kususa bidhaa, kwa Mayele si watatia kiberiti kabisa viwanda vyenyewe?
 
Back
Top Bottom