Salamu Waungwana.
Binafsi ni mfanyabiashara wa kawaida au tuseme wa kati. Kwa mda nimekuwa nikiweka pesa kwenye fixed deposits account za mabenk tofauti na hata UTT-Amis.
Nimeweka CRDB (Mzigo Flex) ambao wanatoa riba ya 9% annually, TCB ambao wanatoa 11% annually and UTT-Amis ambao wanatoa ~12%.
Hata hivyo baada ya kufanya critical evaluation nimegundua dhahiri kwamba TAASISI hizi siyo sehemu za kuwekeza pesa bali kuhifadhi pesa tu ili isiendelee kukatwa monthly otherwise.
Nitatoa mifano kadhaa, mosi; CRDB niliweka 100M kwa annual interest ya 9% sawa na 0.75%monthly kwa maana hiyo kwa mwezi napata 750,000/= (Laki saba na hamsini elfu) baada ya makato ya VAT huwa inabakia maximum 700,000/= wakati mwingine pungufu kabisa.
TCB nimeweka 50M kwa riba ya 11% annually sawa na 0.916%monthly kwa hiyo kila mwezi napata 450,000/= baada ya VAT nabakia na 405,000/= Kwa hiyo kwa mifano hii miwili tu utaona kwamba kwa mwezi mzima uwekezaji wa 150M faida nayoipata Ni 1.1M tu, yaani milioni moja na laki moja tu.
Sasa basi Kwanini nasema huu siyo uwekezaji mzuri; Chukua mfano ukichukua kigari mfano Spacio au Wish 7 seats, bei ina range between 15M-18M. Halafu kila asubuhi uwe unachukua abiria 8 tu kutoka Mbezi to Kariakoo, nauli inakuwa 4000/person. Single route utakuwa na 32,000/= Mafuta 2Lts sawa na 6600/= utabakia na 25,000/= jioni chukua abiria 8 from Kariakoo to Mbezi, nauli 3000/= au Manzese to Mbezi kuanzia saa12 usafiri shida sana, utapata 24,000/= route ya kwenda kulala Ni mafuta. Utaona walau kwa siku huwezi kukosa 40,000/= bila TRA wala PT. Kwa mwezi unapata siyo chini ya 1.2M kwa uwekezaji wa 15M tu. Huu ni uwekezaji.
Kuna watu watabeza kwamba hizi ni biashara za kwenye karatasi lakini ukweli ni kwamba binafsi NAIFANYA biashara hii na return hii siyo estimation bali ni uhalisia kabisa.
NB: Huu ni mtazamo wangu tu siyo lazima kuyabeba. Jumapili Njema na herini ya siku kuu ya Utatu Mtakatifu.
Jebel.
Uko sahihi na hauko sahihi kwq sababu umetoa hitimisho ukitumia matazamo wako na mazingira yako na umesahau kuna factors nyingi zinahitajika kuwa proven
ok tuweke scenario tatu tuanze na ya kwako
Umewekeza kwenye huduma ya usafiri unaingiza 1.2m kila mwez gharama zako za uwekezaji ni 15m plus mda wako pengine siku sita za wiki au siku tano
fast foward miaka 10 baadae 2034 hiyo spacio itakuwa imekupa 100m+ ingawa probability hiyo tunaipa 50/50 na hapo nimekuwa over optimistic sababu hata ukisema kila baada ya mwaka au mwaka na nunu ununue spacio ingine bado price ya spacio haitakuwa 15m
kuna factor za hapa chini zinaweza kufanya hilo lisiwezekane
1. Consistance ya biashara kuhakikisha 1.2m kila mwez
2. Kuchoka kwa gari / ajali
3 mabadiliko ya mfumo wa maisha/sera za serikali
4. Sababu za kijamii na familia
5. Stability ya gharama za uendeshaji
So hapo utaona kuwa gari moja kukupa faida mjumuisho ya 100m+ ndani ya miaka 10 its nearly imposible So tufanye kuwa ili walau uongeze % za kuwa na uhakika kupata hiyo 100m+ kama Faida mjumuisho kufikia 2034 itabidi ujitanue zaidi na kuwekeza zaid mtaji labda kwa kuongeza gari zaidi au kubuni biashara ingine itakayokuingizia kipato cha 1.2m au zaidi
hapo utaona hatuzungumzii tena uwekezaji wa ile 15m yako itakuwa umeongezeka kwan itabidi ununue gari zingine na bado uhakika wa kuwa kufikia 2034 uwe na 100m+ ya faida wont be even close to 70% of probability
So utaona kuwa kwa mtazamo wa mda mfupi utaiona UTT haifai sababu inatoa faida ndogo wa uwekezaji mkubwa ila umesahau rule of thumb ya biashara ambayo ni "the high the risk the high the returns and the vice versa is true
scenario ya pili ni say mimi pia nimewekeza 100m UTT napata around 900k kwa mwez lakini mie ni mwajiriwa na napokea mshahara so kwangu mie UTT is close to safe heaven ya pesa yangu.. sababu sina mpango wa kufanya biashara kwa sababu mbali mbali kubwa ikiwa nature ya kazi yangu
nikiacha hiyo pesa UTT kwa 10yrs roughly itakuwa imeji double.. na kumbuka mie ni mwajiriwa sitegemei UTT inilishe ila miaka 10 baadae nina uwezekano wa kuwa na 200m+ ndio mtaji ulikuwa mkubwa qa 100m na sio 15m lakini je hata ningeamua kufanya biashara na hiyo 100m bado uhakika kwa kuwa miaka kumi baadae niwe na 100m kama faida nje ya mtaji bado aio guarantee
Je risk ni zipi za UTT kushindwa kunipa 100m+ ni hiz hapa chini
1. Thaman kushuka so nitapata chini ya 900k
2 mfuko kufa (kufilisika)
3. Nipate dharura niitoe ( familiy issue)
Utaona kuwa risk za hapo juu ukiondoa hiyo ya dharura zilizobaki risk ni ndogo sana kwa sababu ili UTT ife ni lazima Nchi iwe kwenye "default" yaani ifilisike kama venezuela au Argentina miaka
Kadhaa nyuma.. sababu UTT wanawekeza kwenye Bonds na co operates bussness na pia swala la vipande kushuka thaman itategema uchumi Mzima Wa Nchi uwezekano ni kupanda zaid kuliko kushuka. Yaani UTT ikifeli basi biashara zingine ziko kwenye hali Mbaya zaidi
Miaka 10 iliopita UTT imekuwa na consistency ya kurudisha 10% plus ya faida ndo maana tunaipa high chance ya uwekezaji wake kufanikiwa maana tuna data za kubackup hiyo claim..
Scenario ya tatu tuchukulie mtu ameamua kufata ushauri wako akawa na 15m akawekeza kwenye hiyo biashara je aje route yako maana tayari kuna reference kutoka kwako kuwa 1.2m ni guarantee, je atafute route zingine .. je atapata hiyo 1.2m kwenye route zingine anaweza akapata pungufu au zaidi.. je mfumo wake wa maisha una mfavour kwenye hiyo biashara
So utaona mafanikio yako yana factor nyingi ndan yake directly and indirect so ni hatari kumwambia mtu acopy paste biashara yako
Mwisho wa siku mtu kufanikiwa kwenye uwekezaji aina ya UTT inategemea na na mfumo wake wa maisha. Na ndio maana mifuko aina ya UTT inajulikana kuwa ni mifuko inayotengeneza compounded interest.. faida ya kudunduliza maana yake pesa ikae mda mrefu..
sio vibaya ukitumia UTT kulinda thaman ya pesa yako, infact kitendo cha kuweka pesa UTT kama kulinda thaman huku ukiwa na mipango yabkufanya biashara kinaonyesha kuwa UTT ni uwekezaji mzuri ni swala la kuwa Maono yako hayaendani na bussiness model ya UTT unaitumia kama bank
So uka sahihi kwa kadiri ya mfumo wako wa maisha ulivyoutengeneza lakini hauko sahihi kuona kuwa kuwekeza UTT ni kupoteza. Sababu kuna watu mifumo yao ya maisha inawa favour kwenye uwekezaji wa UTT