Fixed Deposits Account, UTT-Amis ni njia nzuri za kutunza pesa LAKINI SIYO uwekezaji abadani

N.B 40M katumia kama mfano hivyo unaweza kukopa ata pungufu kikubwa elewa hiyo concept aliyoitoa hapo
 
Uko sahihi. Mimi UTT naitumia kuweka hela kwa ajili ya lengo fulani.

Mfano: Pesa ya mahali Umoja fund.
Pesa ya Harusi: Liquid fund.

Nachanga mdogo mdogo kila mwezi, nikifika leongo natoa na kuanza upya.

Ila sifanyi biashara na UTT mimi. Na kama kuna mtu anazani hii ni moja ya biashara, aendelee kuzani tu 😀
 
UTT sio biashara mkuu. Kama una malengo ya mda mrefu pambana na UTT ila ukitaka kutoboa kwa haraka fanya biashara
 
Mkuu kama ulivosema we ni mfanyabiashara wa kati, je unakubaliana na mimi kwamba kuna wakati kwenye biashara inafikia unakuwa na hela cash ambayo ipo tu kiasi hata haihitajiki Kwenye biashara na wala kwa wakati huo hauhitaji kufanya diversification au expansion ya hio biashara, kwa mantiki hiyo, hzo pesa kuliko kukaa tu dormant basi unafanya investments za namna hiyo........
 
Hvi nguvu na muda wa kusimamia hiyo Toyota wish pamoja na shuruba zake katika monetary value waweza ifanya equivalent na bei gani.....mind you Kule kuna risk nyingi mnoo...kugongwa, kupata ajali na kuvunjika , kero za askari barabarani, sometimes kukosa vichwa kabisaaa.......
 
Zinapatikana mkuu... nenda CRDB wananunua kwa niaba ya wananchi pia
Sinilisiki kunamnada wa awali amanapo watu wengi wanaombwa wakati mwingine wanakoswa .Je hizi za CRDB na zile za mnada wa awali wa BOT zinatoifauti Gani?
 
Sinilisiki kunamnada wa awali amanapo watu wengi wanaombwa wakati mwingine wanakoswa .Je hizi za CRDB na zile za mnada wa awali wa BOT zinatoifauti Gani?
Hazina tofauti, sema tu unalipia ada ya 100,000. Bank ni mawakala tu, wanasaidia wananchi kununua
 
Kifupi unapambana na inflations
 
Wengi wanaosema siwez kuweka million 100 noasubr gawio la million kwa mwkaa wengi hawajawah shika ata million ya kwao , ivi unajua nguvu ya kupata million 100 na ku risk ipotee kizembe
 
Ni biashara hata kama hutaki umeipa UTT pesa yako wanaizungusha wanakupa faida iwe ni shilingi moja au shilingi 1000 bado inahesabika ni faida maana yake imezalishwa na mtaji ulioweka .. ndo maana inaitwa biashara ya uwekezaji

Matazamo wako haubadili uhalisia
 
Uko sahihi na hauko sahihi kwq sababu umetoa hitimisho ukitumia matazamo wako na mazingira yako na umesahau kuna factors nyingi zinahitajika kuwa proven

ok tuweke scenario tatu tuanze na ya kwako

Umewekeza kwenye huduma ya usafiri unaingiza 1.2m kila mwez gharama zako za uwekezaji ni 15m plus mda wako pengine siku sita za wiki au siku tano

fast foward miaka 10 baadae 2034 hiyo spacio itakuwa imekupa 100m+ ingawa probability hiyo tunaipa 50/50 na hapo nimekuwa over optimistic sababu hata ukisema kila baada ya mwaka au mwaka na nunu ununue spacio ingine bado price ya spacio haitakuwa 15m
kuna factor za hapa chini zinaweza kufanya hilo lisiwezekane

1. Consistance ya biashara kuhakikisha 1.2m kila mwez
2. Kuchoka kwa gari / ajali
3 mabadiliko ya mfumo wa maisha/sera za serikali
4. Sababu za kijamii na familia
5. Stability ya gharama za uendeshaji

So hapo utaona kuwa gari moja kukupa faida mjumuisho ya 100m+ ndani ya miaka 10 its nearly imposible So tufanye kuwa ili walau uongeze % za kuwa na uhakika kupata hiyo 100m+ kama Faida mjumuisho kufikia 2034 itabidi ujitanue zaidi na kuwekeza zaid mtaji labda kwa kuongeza gari zaidi au kubuni biashara ingine itakayokuingizia kipato cha 1.2m au zaidi

hapo utaona hatuzungumzii tena uwekezaji wa ile 15m yako itakuwa umeongezeka kwan itabidi ununue gari zingine na bado uhakika wa kuwa kufikia 2034 uwe na 100m+ ya faida wont be even close to 70% of probability

So utaona kuwa kwa mtazamo wa mda mfupi utaiona UTT haifai sababu inatoa faida ndogo wa uwekezaji mkubwa ila umesahau rule of thumb ya biashara ambayo ni "the high the risk the high the returns and the vice versa is true

scenario ya pili ni say mimi pia nimewekeza 100m UTT napata around 900k kwa mwez lakini mie ni mwajiriwa na napokea mshahara so kwangu mie UTT is close to safe heaven ya pesa yangu.. sababu sina mpango wa kufanya biashara kwa sababu mbali mbali kubwa ikiwa nature ya kazi yangu

nikiacha hiyo pesa UTT kwa 10yrs roughly itakuwa imeji double.. na kumbuka mie ni mwajiriwa sitegemei UTT inilishe ila miaka 10 baadae nina uwezekano wa kuwa na 200m+ ndio mtaji ulikuwa mkubwa qa 100m na sio 15m lakini je hata ningeamua kufanya biashara na hiyo 100m bado uhakika kwa kuwa miaka kumi baadae niwe na 100m kama faida nje ya mtaji bado aio guarantee

Je risk ni zipi za UTT kushindwa kunipa 100m+ ni hiz hapa chini

1. Thaman kushuka so nitapata chini ya 900k
2 mfuko kufa (kufilisika)
3. Nipate dharura niitoe ( familiy issue)

Utaona kuwa risk za hapo juu ukiondoa hiyo ya dharura zilizobaki risk ni ndogo sana kwa sababu ili UTT ife ni lazima Nchi iwe kwenye "default" yaani ifilisike kama venezuela au Argentina miaka
Kadhaa nyuma.. sababu UTT wanawekeza kwenye Bonds na co operates bussness na pia swala la vipande kushuka thaman itategema uchumi Mzima Wa Nchi uwezekano ni kupanda zaid kuliko kushuka. Yaani UTT ikifeli basi biashara zingine ziko kwenye hali Mbaya zaidi

Miaka 10 iliopita UTT imekuwa na consistency ya kurudisha 10% plus ya faida ndo maana tunaipa high chance ya uwekezaji wake kufanikiwa maana tuna data za kubackup hiyo claim..

Scenario ya tatu tuchukulie mtu ameamua kufata ushauri wako akawa na 15m akawekeza kwenye hiyo biashara je aje route yako maana tayari kuna reference kutoka kwako kuwa 1.2m ni guarantee, je atafute route zingine .. je atapata hiyo 1.2m kwenye route zingine anaweza akapata pungufu au zaidi.. je mfumo wake wa maisha una mfavour kwenye hiyo biashara

So utaona mafanikio yako yana factor nyingi ndan yake directly and indirect so ni hatari kumwambia mtu acopy paste biashara yako

Mwisho wa siku mtu kufanikiwa kwenye uwekezaji aina ya UTT inategemea na na mfumo wake wa maisha. Na ndio maana mifuko aina ya UTT inajulikana kuwa ni mifuko inayotengeneza compounded interest.. faida ya kudunduliza maana yake pesa ikae mda mrefu..

sio vibaya ukitumia UTT kulinda thaman ya pesa yako, infact kitendo cha kuweka pesa UTT kama kulinda thaman huku ukiwa na mipango yabkufanya biashara kinaonyesha kuwa UTT ni uwekezaji mzuri ni swala la kuwa Maono yako hayaendani na bussiness model ya UTT unaitumia kama bank

So uka sahihi kwa kadiri ya mfumo wako wa maisha ulivyoutengeneza lakini hauko sahihi kuona kuwa kuwekeza UTT ni kupoteza. Sababu kuna watu mifumo yao ya maisha inawa favour kwenye uwekezaji wa UTT
 
Biashara gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…