Flora Mbasha ajifungua, nani baba wa mtoto?

Flora Mbasha ajifungua, nani baba wa mtoto?

Kwani huyo Flora aliondoka lini kwa mumewe? Tunajuaje kama alikuwa mjamzito? Nimeona kwenye gazeti ya Mtanzania akipinga kuwa picha ya mtoto.inayosambazwa siyo ya mwanawe.
Kinauche mkeo akienda kukaa kwamjomba wake!!akizaa utasema mwanae??? Akiwa Ana NDA safarizake unakuwaga nae??Mungu awaongoze msijepatalaana za wajukuu zenu!!!!
 
hizi post watu wanabeba kila kitu wanachokiona online ovyo ovyo tu.. Mleta mada umekaa ukafikiria kua kuna possibility mtu alikaa home akatafuta picha ya mtoto anayefanana na msela mdomo then akaipost hewani?? afu personal life la mtu sijui kwa nini ukae unalifuatilia, ukifatiliwa wewe sijui kama utatoka msafi..
 
Jamaniee nasema neno moja tu!mtumishi wa Mungu yeyote hastahili kushutumiwa kwa lolote lile,asanteni
 
Tito 1:7
Maana imempasa Askofu asiwe mtu wa kushutumiwa kwa LOLOTE kwa kuwa ni WAKILI wa Mungu
Mchungaji wangu Gwajima hali ndiyo imefikia hapo kweli?nikuulize swali ni kwa nini hasa ushutumiwe kwenye mambo kama hayo??????????hivi unafahamu historia ya hao watu wawili??unaonaje ukiheshimu kazi ya yule mzee wetu aliyetangulia kwa kuheshimu familia yake????halafu mbona yule mzee wetu aliyeheshimika sana kwa kazi iliyotukuka hakushutumiwa kwenye mambo kama hayo???mchungaji jiangalie upya


View attachment 224512

Aliekwambia Gwajima ni mchungaji ni nani? Yule ni msanii kama walivyo wasanii wa mjini.Namaanisha tapeli ila sasa yeye Gwajima utapeli wake anatumia mazingaombwe ya kisukuma.Take care siku za mwisho hizi manabii wa uongo akina Gwajima ndio hao.
 
Kuna maswali mengi kuliko majibu juu ya tuhuma hzi za mahusiano kati ya wachungaji na kondoo wao,ni kweli wanasingiziwa?
 
SIKU chache baada ya picha za mtoto mchanga kusambazwa katika mitandao ya kijamii na kudai kuwa ni za mtoto wa mwimbaji wa nyimbo za Injili nchini, Flora Mbasha kuwa amezaa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima hatimaye wawili hao wamefunguka.


Hatua hiyo imekuja miezi saba tangu wawili hao walipoingia katika mgogoro wa ndoa yao hali iliyosababisha mume wa Flora, Emmanuel Mbasha kufikishwa mahakamani kwa kosa la ubakaji.
1.png


Akizungumza jijini Dar es Salaam jana ili kupata ukweli kuhusu taarifa za picha za mtoto huyo ambaye anadaiwa kuwa amezaa na Flora, Mchungaji Gwajima, alisema taarifa hizo ni za uzushi na huenda zinasambazwa na mume wa Flora.

Mchungaji Gwajima alikwenda mbali na kusema pamoja na uzushi huo unaosambazwa dhidi yake kwa kuhusishwa katika uhusiano na Flora anamwachia Mungu kila kitu.
“Hahaha… si unajua hiyo issue (suala, jambo) ya Mbasha ni ya muda mrefu tu… wakati mwingine mimi huwa sijibu ujinga,” alisema Gwajima huku akicheka.

“Awali niliwaza kuwashitaki (alipoanza kuhusishwa kwamba ana uhusiano na Flora) wanaoeneza uzushi huo lakini nikaona ‘It doesn’t hold water’ (haina mashiko), najua shutuma hizo zinatoka wapi,” alisema Mchungaji Gwajima.

Alipoulizwa kuhusu mtu anayemshuku kueneza uvumi huo alisema: “Probably’ (nadhani) atakuwa Emmanuel Mbasha mwenyewe. Tangu mwanzo alipotuhumiwa kumbaka shemeji yake na kutoroka kwake akihofia kukamatwa na polisi, mkewe alikuja kanisani kwetu na mimi nilimwagiza mwenyekiti wa kusaidia jamii amsaidie,” alisema Gwajima na kuongeza:

“Sasa Mbasha alipotoka huko alikokimbilia na kusikia kuwa mkewe yuko hapa kanisani, ndipo alipoanza kueneza uzushi,” alisema.

Gwajima alisisitiza kuwa Flora hakufikia kwake kwa jambo lolote bali aliendelea kuishi katika nyumba aliyopanga.

Alipoulizwa kwa nini hamshitaki Mbasha ili kulinda heshima yake, Gwajima alisema ameshawaita ndugu zake akiwemo baba yake mzazi lakini nao wakaonekana kutommudu Emmanuel.

“Nilishawaita wazazi wake, baba na mama yake, ndugu zake kina Mbasha na tukazungumza. Lakini baba yake alisema hata yeye amemshindwa. Yaani anawadharau hata ndugu zake,” alisema.

Akisimulia jinsi alivyokutana na Emmanuel na Flora Mbasha, Mchungaji Gwajima alisema awali walikuwa wakiimba kwenye mikutano aliyokuwa akihubiri.

“Hawa hawakuwa washirika wetu, ila walikuwa wakija kuimba kwenye mikutano yetu ya Injili. Walikuja Arusha, Moshi na Tanga, kwa hiyo tulikuwa tukiwatumia sana. Baadaye ndiyo yakatokea hayo hadi Flora akakimbilia kanisani kwetu,” alisema.

Hata hivyo Gwajima alisema hakujua kama Flora ni mjamzito wakati anakuja kuomba msaada kanisani kwake.

“Mimi sikujua kama alikuwa mjamzito, hata taarifa kwamba amejifungua ndiyo nazisikia kwako. Hapa nimetoka ‘airport’, sikuwepo Dar es Salaam,” alisema na kuongeza:

“Sasa kama mtu una wasiwasi na mtoto si ukapime DNA ili upate uhakika? Hii ni habari ya kutaka tu kulichafua kanisa na huduma,” alisisitiza.

Flora anena
Mwandishi alimtafuta Flora kwa njia ya simu ili kuzungumzia suala hilo ambapo alisema “Siko tayari kuzungumza lolote kuhusu Mbasha kwa sasa. Yeye anajeuri ya pesa ndo maana anafanya haya yote lakini mimi ninasimama na Mungu wangu na ninajua Mungu atanipigania,” alisema Flora.

Alipoulizwa kuhusu hali ya mtoto wake mchanga, alisema “Mtoto hajambo, lakini mtoto anayesambazwa kwenye mitandao siyo wangu, na hizo picha nyingine nafikiri ni za kutengeneza tu,” alisema Flora.

Mbasha
Kutokana na hali hiyo Mwandishi alimtafuta mume wa Flora, Emmanuel Mbasha, ili kuzungumzia suala hilo, licha ya kupokea simu yake ya kiganjani, aliishia kusema yuko njiani hivyo apigiwe baadaye.

Hata alipopigiwa baadaye, aliendelea kusema kuwa atafutwe baadaye na wala hakujibu ujumbe wa simu (sms).

Alipotafutwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa WhatsApp, ujumbe huo ulionekana kufika na kusomwa na baada ya muda alituma ujumbe wa sauti uliokuwa na wimbo na kuandika maneno mafupi yaliyosomeka ‘wimbo wangu mpya’.

Pamoja na mambo mengine, wimbo huo unamaneno yasemajo “Haribu mipango ya shetani, haribu…, Binadamu wengine mashetani mfano wa Cobra, wanawaza mabaya, kuna siku watakufa kabisa,” ulisikika ujumbe wa wimbo huo
Sehemu nyingine ya wimbo huo ulioimbwa kwa mwelekeo wa mipasho, inasema “Wanakesha kwa waganga kuliloga, darubini ya bwana imewamulika, ukiwaona utadhani ni wema,”

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo katika tovuti ya kituo cha televisheni ya East Africa (EATV), Agosti 27, mwaka jana Flora alihojiwa na kituo hicho kupitia kipindi cha Kikaangoni Live, kinachoendeshwa kwa njia ya mtandao wa kijamii wa Facebook, alisema ujauzito aliokuwa nao ni wa mumewe Mbasha na si Mchungaji Gwajima.

Flora alisema kuwa hawezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mchungaji Gwajima kwa kuwa ni mjomba wake na kwamba watu wamekuwa wakizusha kwa lengo la kumchafua na kumshushia hadhi.

“Hayo ni maneno tu ya watu mtaani ila Mchungaji Gwajima ni mtumishi wa Mungu na ni ‘Uncle’ wangu ninawezaje kuwa na uhusiano na uncle wangu..? ” alihoji Flora.

Kuhusu kuachana na Mbasha, Flora alisema hakuachana naye kwa sababu ya Gwajima na amedai kuwa bado anampenda, lakini anampenda Mungu zaidi.

“Sijamwacha mume wangu sababu ya Gwajima na kweli bado napenda sana Mbasha lakini nampenda zaidi Mungu,” alisema Flora.
 
Jamii Forum ni ni kama Kokoro - linavua kila uchafu. Ila ningeomba waleta mada wawe waangalifu na mada wanazozileta hapa jukwaani.
1. Lengo la forrum ni kufundisha,kukosoa, kuelimisha kujenga. Tusipafanye kijiwe cha porojo za vijiweni na mihemko isiyojenga.
2. Mtu akiwa na bifu na mwanasiasa au mtu yeyote amepafanya JF ndipo pa kunolea makali ya panga zao za kukata shingo za unayetaka kukata
3. Iwe Lowassa, Gwajima au membe - tuwe watu wenye misimamo na viwango (Principles and Standards) maana tukiendelea kwa kasi hii, tutaishia kuwa kuwa watu wa hoja za vijiwe vya gahawa!
4. Ni vizuri tukawa watu wa kupima mada kwanza kabla ya kuileta mjengoni ijadiliwe! Tuepuke kujadili hisia - tujadili hoja!
 
Haka kamalaika ka Mungu sijui kwa nini wanakaweka mtandaoni hivi jamani, hii si haki kabisa, ugomvi wa wazazi unakahusu nini kukasambaza mtandaoni hivi na kwanza aliyetoa picha yake ni nani? Namtetea huyu mtoto mtoeni mtandaoni.
 
Frola ndo anajua dingi wa mtoto.

je ni wangapi humu wana uhakika wa watoto wao?
 
Kinauche mkeo akienda kukaa kwamjomba wake!!akizaa utasema mwanae??? Akiwa Ana NDA safarizake unakuwaga nae??Mungu awaongoze msijepatalaana za wajukuu zenu!!!!

Samahani sana sijakuelewa kabisa. Lengo langu ni kwamba kwa kuwa mchungaji anatuhumiwa huku wote wakikataa dawa ni DNA. Sasa ni kwanini laana za wajukuu?
 
Jamaniee nasema neno moja tu!mtumishi wa Mungu yeyote hastahili kushutumiwa kwa lolote lile,asanteni

Ha ha haaaa. Hii kali. Itakuwa ole kwa wanaowashutumu kama shutuma hizo zitakuwa za uongo. Wasimame kama Yesu waulize ni nani anawashuhudia kama wana dhambi? Kumbuka maandiko yako wazi kuwa 'uasherati usitajwe kwenu"
 
Jamani jamani hata picha ya mtoto tupate ridhaa??? Au kwa vile yuko uchi lkn naona km kavaa. Don't exaggerate things swala ni nani baba wa baby .
 
Angalia macho ya mtoto na macho ya gwajima, copyright...usanii mtupu na kujifanya watumishi wa mungu...mammae!
 
Hivi, mbasha ameshakataa kuwa mtoto sio wake??
Na je, mama wa mtoto ameshasema kuwa mtoto sio wa mbasha???
Na je, kama mtoto sio wa Mbasha, ni LAZIMA atakuwa wa Gwajima??

Flora atakuwa alingonoana na mwanaume na akapata mimba. Kwa yeyote aliyengonoana nae, tunapaswa kufanyeje kama jamii?? Kuandamana???
 
Si vyema kudisplay picha ya mtoto asiyeweza kujitetea kwa lolote

Mkuu Jabulani kichanga kitapata madhara gani sie tukiona picha? Kitapata depression. Au kitaharibikiwa saikolojia??? Picha twalalama je uso kwa uso si itakuwa msiba? I just dont want to believe what you are persuading jf to
 
Back
Top Bottom