Jamii Forum ni ni kama Kokoro - linavua kila uchafu. Ila ningeomba waleta mada wawe waangalifu na mada wanazozileta hapa jukwaani.
1. Lengo la forrum ni kufundisha,kukosoa, kuelimisha kujenga. Tusipafanye kijiwe cha porojo za vijiweni na mihemko isiyojenga.
2. Mtu akiwa na bifu na mwanasiasa au mtu yeyote amepafanya JF ndipo pa kunolea makali ya panga zao za kukata shingo za unayetaka kukata
3. Iwe Lowassa, Gwajima au membe - tuwe watu wenye misimamo na viwango (Principles and Standards) maana tukiendelea kwa kasi hii, tutaishia kuwa kuwa watu wa hoja za vijiwe vya gahawa!
4. Ni vizuri tukawa watu wa kupima mada kwanza kabla ya kuileta mjengoni ijadiliwe! Tuepuke kujadili hisia - tujadili hoja!