Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kumekucha Wadau.
Leo asubuhi wakati nawahi kwenye Mitikasi yangu nimejikuta nimenasa katikati ya foleni ambayo hata kusogeza tu mguu ilikiwa shida na ni mchezo wa kila siku hasa kwenye barabara hii ya Mwai Kibaki.
Katika mji wa Dar es Salaam, foleni barabara ya Mwai Kibaki imekuwa ni kero kubwa kwa wakazi. Kila siku, madereva wanapotoka Kawe kuelekea Morocco, au Kutoka Morocco - Kawe hali inakuwa mbaya zaidi. Wakati wa safari zao, madereva wengi huamua kufungua barabara na kuingia kwenye upande wa pili, wakijaribu kupita kwa haraka, bila kujali sheria za usalama barabarani.
Hali hii inasababisha msongamano wa magari pande zote mbili, huku wengine wakijaribu kupita hadi kwenye sehemu ya watembea kwa miguu. Wakati mwingine, magari yanakosa kabisa kuelekea eneo husika, na hivyo kufanya foleni kuwa ndefu zaidi. Watu wanashuhudia vichochoro vya magari.
Ni wazi kuwa, iwapo hatua stahiki hazitachukuliwa, kwa mchezo huu adha hii ya foleni itakuwa mbaya zaidi.
Pia, Soma:
• Barabara ya Mbezi Mwisho, Kimara kuelekea Town kila siku asubuhi kuna foleni kubwa, hivi tatizo ni nini?
• LATRA imeshindwa kutuletea usafiri wa daladala njia ya Tegeta/Bunju-Kawe Ukwamani kupitia barabara ya Mwai Kibaki?