For Political Survival, Halima Mdee na wenzake wahamie ACT Wazalendo

For Political Survival, Halima Mdee na wenzake wahamie ACT Wazalendo

Hapa nadhani watakimbilia Mahakamani kama alivyofanya Zitto miaka ileeeee!! Wakienda Mahakamani wanazuia maamuzi ya Baraza Kuu kutekelezwa na wanafungua kesi ya kupinga mchakato wa kuwafukuza. Wanarudi Bungeni kuendelea na Ubunge wao, kedi inaendeshwa miaka 3 hivyo wanamaliza miaka 5!! Ngoma sasa ni kwa chama, watachukua ruzuku ama la??

Chadema haina shida na Ubunge wao, Cha msingi ni kwamba imewakataa na kwa Sasa chadema Ina mwakilishi mmoja bungeni pekee yake.
 
Jamani Zito alienda Mahakamani kutetea Ubunge wake enzi zile hata Magu hakuwa Rais bado, sijui kwanini binadamu tunasahau haraka, au mna shida gani na hayati Magufuli, muacheni mzee wa watu apumzike kwa amanii

Tofautisha ubunge wa Zitto na Ubunge wa viti maalum ambapo chama ndicho kinapeleka majina, Sasa anayepeleka majina kasema Hawa sio wanachama wangu utafanyaje?.
 
Ndicho nilichokisema. Mbinu ya kukimbilia mahakamani ndio short term goal sahihi itakayowasaidia kwa lengo la ku-buy time. Zitto bila shaka atatumia fursa hii vizuri kurudisha ubest wake wa nguvu na pacha wake wa kitambo Halima Mdee na kukiimarisha zaidi chama chake.

Zitto mwenyewe anaweza kurudi chadema. Maana ACT kabaki pekee yake.
 
Kazi ya mwanasiasa ni kufanya siasa.

Maamuzi ya mwisho ya kuwavua uwanachama wa CHADEMA wabunge Halima Mdee na wenzake 18 baada ya rufaa yao kukataliwa, huenda yakawatoa rasmi kwenye siasa za vyama, hivyo kulazimika kutetea ubunge wao mahakamani kwa ajili ya kusogeza siku mbele kuelekea 2025.

Labda wengi wanajiuliza au wengine wanadhani huu ndio mwisho wa kisiasa kwa wanasiasa hawa wazoefu na machachari. Kisiasa, hesabu nzuri zaidi ni wanawake hawa kuhamia chama cha ACT ili wapate jukwaa halali la kuendelea kuwa relevant kwenye siasa za upinzani na uwakilishi hapa nchini.

Jambo la muhimu zaidi, maamuzi ya CHADEMA yaheshimiwe.

You know it is quite interesting that miaka yote CHADEMA haijawahi kukubaliana na matokeo ya Uchaguzi kwa ngazi ya Urais lakini Mbowe, Mnyika and the rest walienda Bungeni kama Wabunge hawajawahi kususia. Ila this one time ambapo wanaume wote “wameshindwa” uchaguzi ndo ubunge eti unasusiwa mazimaa…
 
Mahakamani wanaenda kutetea Ubunge gani?. Unaenda kutetea Ubunge ambao umeupata kinyume cha sheria?. Halafu ubunge wa viti maalum ni tofauti na wa kupigiwa kura. Ubunge wa viti maalum chama ndicho chenye nguvu ya maamuzi nani awe na nani asiwe mbunge. Yani chama kinaruhusiwa kuleta orodha ya wabunge wengine refer kesi ya Lipumba.

Hapo umemaliza kabisaaa mkuu.
 
Kama namwona Zitto anavyowatamani waende ht saiv wakajijenge chama, hakika watakuwa wamelamba dume
 
Hapa nadhani watakimbilia Mahakamani kama alivyofanya Zitto miaka ileeeee!! Wakienda Mahakamani wanazuia maamuzi ya Baraza Kuu kutekelezwa na wanafungua kesi ya kupinga mchakato wa kuwafukuza. Wanarudi Bungeni kuendelea na Ubunge wao, kedi inaendeshwa miaka 3 hivyo wanamaliza miaka 5!! Ngoma sasa ni kwa chama, watachukua ruzuku ama la??
Hii si zama ile, watamalizia hela zao mahakamani bure.
 
Wakitumia mbinu ya kupeleka shauri mahakamani, watavuta muda. Bungeni wapo sana tu. Case study ni kilichotokea kwa Zitto enzi zile.

Huko mahakamani sio kwenda kufungua tu mashitaka, wakitaka wawe wanaishi kabisa huko mahakamani, lakini chama kimeshachukua hatua. Na huko bungeni ni haki yao kwenda kwani walishahongwa huo ubunge kwenye hilo bunge kibogoyo.
 
Kam namwona Zitto anavyowatamani waende ht saiv wakajijenge chama, hakika watakuwa wamelamba dume

Wana haki ya kuhamia chama chochote hata CCM wakitaka, ila kuvuta watu itakuwa ngumu sana maana bado wanategemea washabiki wa cdm ndio wawe watu wao. Zito mwenyewe anaelewa vizuri mziki wa kuvutia watu ulivyo.
 
Back
Top Bottom