Kazi ya mwanasiasa ni kufanya siasa.
Maamuzi ya mwisho ya kuwavua uwanachama wa CHADEMA wabunge Halima Mdee na wenzake 18 baada ya rufaa yao kukataliwa, huenda yakawatoa rasmi kwenye siasa za vyama, hivyo kulazimika kutetea ubunge wao mahakamani kwa ajili ya kusogeza siku mbele kuelekea 2025.
Labda wengi wanajiuliza au wengine wanadhani huu ndio mwisho wa kisiasa kwa wanasiasa hawa wazoefu na machachari. Kisiasa, hesabu nzuri zaidi ni wanawake hawa kuhamia chama cha ACT ili wapate jukwaa halali la kuendelea kuwa relevant kwenye siasa za upinzani na uwakilishi hapa nchini.
Jambo la muhimu zaidi, maamuzi ya CHADEMA yaheshimiwe.