Bila shaka Mdee anaipenda sana Chadema. Hata Matiko. Lakini kwa alichokifanya kimemuondolea thamani mbele ya wanachama wengi wa Chadema ambao waliamini kuwa yeye na wenzake ni wafia chama. Mbowe angeanzaje na reconciliatory statement kwa watu ambao wamekataa kabisa kuonyesha kuwa wanajutia walioyafanya. Wao walitaka rufaa yao ikubaliwe na waendelee na ubunge wao, kitu ambacho ni impossible. Naamini kabisa kuwa wangejiuzuru ubunge wakati Mbowe yuko ndani, chama kingewasamehe.
Chadema haiwezi kuyumba. Itajengeka zaidi baada ya kuthibitisha wanasimamia principles. Chadema imethibitisha kuwa inaweza ku survive bila ya wakina Halima lakini sidhani kama wakina Halima wana future nje ya Chadema. Ushauri wangu kwao ni kuwa wangekaa kimya na kuhamia kwenye punditry ambako sasa wana nafasi nzuri ya kusimamia haki bila kuegemea chama chochote. Wamuige binti ya Sarungi. Kuna maisha nje ya vyama vya siasa.
Amandla...