For Political Survival, Halima Mdee na wenzake wahamie ACT Wazalendo

For Political Survival, Halima Mdee na wenzake wahamie ACT Wazalendo

Hapa nadhani watakimbilia Mahakamani kama alivyofanya Zitto miaka ileeeee!! Wakienda Mahakamani wanazuia maamuzi ya Baraza Kuu kutekelezwa na wanafungua kesi ya kupinga mchakato wa kuwafukuza. Wanarudi Bungeni kuendelea na Ubunge wao, kedi inaendeshwa miaka 3 hivyo wanamaliza miaka 5!! Ngoma sasa ni kwa chama, watachukua ruzuku ama la??
Sio kwa Tanzania ya sasa, Kama Mbowe na Samia Wana good working relationship usishangae kesho NEC ikatoa barua kutangaza nafasi ziko wazi!
 
You know it is quite interesting that miaka yote CHADEMA haijawahi kukubaliana na matokeo ya Uchaguzi kwa ngazi ya Urais lakini Mbowe, Mnyika and the rest walienda Bungeni kama Wabunge hawajawahi kususia. Ila this one time ambapo wanaume wote “wameshindwa” uchaguzi ndo ubunge eti unasusiwa mazimaa…
Sasa upate wabunge 120 na 40% ya kura za Urais pamoja na 30% ya Halmashauri nchi nzima then ususe??? That is something.

Ila unaporwa majimbo yoteee afu Una settle kwa viti maalum 19?? Aisee hayo ni madharau makubwa sana
 
Jambo moja nafahamu nalo ni kwamba Halima Mdee ni CHADEMA hadi kwenye damu. Hata kama atatoka, mapenzi yake na imani yake kwa CHADEMA itaendelea kuwa moyoni mwake. Mpende msipende, kwa Halima Mdee CHADEMA imepoteza sana sana. Ningekuwa mimi ni Kiongozi CHADEMA nisingekubali kumwachia Halima. Angalieni wenzenu wa CCM, kuna mambo yalitokea ila hata kama wanafukuzana lakini wanakaa wanayajenga yanaisha wanasonga mbele kisiasa.

Kwa Mbowe kusamehewa na kufutiwa kesi yake basi naye angekuja na reconciliatory statement za kuwasamehe hawa wadada na kuanza upya. In short CHADEMA itayumba.
Bila shaka Mdee anaipenda sana Chadema. Hata Matiko. Lakini kwa alichokifanya kimemuondolea thamani mbele ya wanachama wengi wa Chadema ambao waliamini kuwa yeye na wenzake ni wafia chama. Mbowe angeanzaje na reconciliatory statement kwa watu ambao wamekataa kabisa kuonyesha kuwa wanajutia walioyafanya. Wao walitaka rufaa yao ikubaliwe na waendelee na ubunge wao, kitu ambacho ni impossible. Naamini kabisa kuwa wangejiuzuru ubunge wakati Mbowe yuko ndani, chama kingewasamehe.

Chadema haiwezi kuyumba. Itajengeka zaidi baada ya kuthibitisha wanasimamia principles. Chadema imethibitisha kuwa inaweza ku survive bila ya wakina Halima lakini sidhani kama wakina Halima wana future nje ya Chadema. Ushauri wangu kwao ni kuwa wangekaa kimya na kuhamia kwenye punditry ambako sasa wana nafasi nzuri ya kusimamia haki bila kuegemea chama chochote. Wamuige binti ya Sarungi. Kuna maisha nje ya vyama vya siasa.

Amandla...
 
Kuna kitu kinaitwa "political culture" itawashinda, kule watakutana namifumo iliyorithiwa kutoka cuf ya zamani na watu wao na mipango yao yamuda mrefu na muda mfupi,itawashinda tu
 
ACT imeshaimarika Zanzibar, Mdee na wenzake (kama watahamia) watakiimarisha Bara.
Kafulila na machali wako wapi?? Si tuliambiwa wangeizika chadema Kigoma. Mkuu kuna watu hawana nguvu nje ya mfumo wa chama nani alijua Dr.Slaa aliposusa, CHADEMA ingezoa kata zote za Karatu???

Hivi tuliambiwa Mashinji anajua Siri zote na ataiua CHADEMA ndani ya siku 2?? Leo hii hata unajua Yuko wapi?

Zitto pamoja na uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja na kukubalika na vijana ameweza itingisha CHADEMA hata Kigoma tu hapo?? Yaani CHADEMA ilikua na wabunge plus madiwani wengi kuliko ACT huko Kigoma then unasema watakuwa tishio kwa Chadema??

Anyway maadam wote ni upinzani then watasaidia kuiua CCM ila kama wataenda ACT Ili kupambana na CHADEMA basi watafutika kama tu Slaa,Mashinji, Kafulila, na Lijualikali walivyopotea.
 
Naunga mkono hoja, baadhi yao, akiwemo Halima Mdee na Esta Bulaya, hawa ni wanasiasa very good assets kisiasa, Chadema turned these assets into liabilities. Kama hawakutendewa haki, kiukweli kabisa, karma itaitafuna Chadema!.
Karibu mitaa hii A Kangaroo Court Moja, Kutoa Hukumu Kikangaroo, Kisha Kikao cha Rufaa, Kikiyabariki Maamuzi yale ya Kikangaroo. Je, nacho ni A Kangaroo?, dhulma za aina hii, husababisha karma zisizo za lazima kabisa kwa Chadema kama chama, na kwa individual players!.
P.
kwahiyo unaunga mkono wao walivyofoji nyaraka?
Vipi na nyie mlivyowatimua Nchimbi na Sophia Simba karma iliwapeleka wapi?
 
Zanzibar gani? Sasa hivi kumepoa hakuna harakati. Ngoja chadema waende Hilo tuone.
Chadema haina mvuto Zanzibar, kinaonekana ni chama cha kidini. Naweza nisikubaliane na hilo lakini ndio ukweli. Siasa za Zanzibar zina siasa zake. Siasa za siasa.
 
Jambo moja nafahamu nalo ni kwamba Halima Mdee ni CHADEMA hadi kwenye damu. Hata kama atatoka, mapenzi yake na imani yake kwa CHADEMA itaendelea kuwa moyoni mwake. Mpende msipende, kwa Halima Mdee CHADEMA imepoteza sana sana. Ningekuwa mimi ni Kiongozi CHADEMA nisingekubali kumwachia Halima. Angalieni wenzenu wa CCM, kuna mambo yalitokea ila hata kama wanafukuzana lakini wanakaa wanayajenga yanaisha wanasonga mbele kisiasa.

Kwa Mbowe kusamehewa na kufutiwa kesi yake basi naye angekuja na reconciliatory statement za kuwasamehe hawa wadada na kuanza upya. In short CHADEMA itayumba.
sasa umejuaje kama hayataisha?
ccm ilimtimua Membe lakini baadae akarudi

ccm ilimtimua Nchimbi lakini unajua baadae ilikuaje

nadhani kikubwa kikubwa ni kuipa heko CDM kwa kuchukua maamuzi bila hivyo uko mbele kila mmoja angefanya anachotaka kwenye chama
 
You know it is quite interesting that miaka yote CHADEMA haijawahi kukubaliana na matokeo ya Uchaguzi kwa ngazi ya Urais lakini Mbowe, Mnyika and the rest walienda Bungeni kama Wabunge hawajawahi kususia. Ila this one time ambapo wanaume wote “wameshindwa” uchaguzi ndo ubunge eti unasusiwa mazimaa…

Interesting take which might be viewed as a gender card 😄
 
Jambo moja nafahamu nalo ni kwamba Halima Mdee ni CHADEMA hadi kwenye damu. Hata kama atatoka, mapenzi yake na imani yake kwa CHADEMA itaendelea kuwa moyoni mwake. Mpende msipende, kwa Halima Mdee CHADEMA imepoteza sana sana. Ningekuwa mimi ni Kiongozi CHADEMA nisingekubali kumwachia Halima. Angalieni wenzenu wa CCM, kuna mambo yalitokea ila hata kama wanafukuzana lakini wanakaa wanayajenga yanaisha wanasonga mbele kisiasa.

Kwa Mbowe kusamehewa na kufutiwa kesi yake basi naye angekuja na reconciliatory statement za kuwasamehe hawa wadada na kuanza upya. In short CHADEMA itayumba.
Si walipewa nafasi ya maridhiano kabla ya kupiga Kura wakakataa!?wakijidanganya Wana Kura nyingi za kuwaunga mkono kumbe hawana!?Mwenyekiti ameeleza namna ambavyo alichukua hatua za kujadilia nai mara kadhaa ili kunusuru hili Jambo!?kwa kifupi Halima na kundi lake walisha amua kukengeuka kabisa.Hatujui walikuwa na makubaliano gani na waliowaingiza bungeni kupitia mlango wa uani.Pengine tungejua labda tungeelewa ugumu wa wao wa ku reconcile na chama kumetokea wapi.Nacho amini hata wao walijua kwa kukengeuka kwao mwisho wao na chadema ulikuwa uwe huu.
 
CHADEMA wanaitolea macho ruzuku wewe
Unajidanganya. Serikali inaihitaji Chadema kuliko Chadema inavyoihitaji serikali. Nadhani Mheshimiwa Rais ametambua umuhimu wa kuwa na wapinzani bungeni wenye baraka za chama chao. Sitashangaa kama sehemu ya makubaliano ya Wenyeviti wa CCM na Chadema ni Chadema kupeleka mbadala wa hawa 19 Bungeni hata kama wataendelea na msimamo wao wa kutotambua matokeo ya uchaguzi uliopita. Wataweza kujitetea kuwa kura zilizowapa hao wabunge ni sehemu tu ya kura walizostahili kwa hiyo ni haki yao kufaidika nazo.

Amandla...
 
Kafulila na machali wako wapi?? Si tuliambiwa wangeizika chadema Kigoma. Mkuu kuna watu hawana nguvu nje ya mfumo wa chama nani alijua Dr.Slaa aliposusa, CHADEMA ingezoa kata zote za Karatu???

Hivi tuliambiwa Mashinji anajua Siri zote na ataiua CHADEMA ndani ya siku 2?? Leo hii hata unajua Yuko wapi?

Zitto pamoja na uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja na kukubalika na vijana ameweza itingisha CHADEMA hata Kigoma tu hapo?? Yaani CHADEMA ilikua na wabunge plus madiwani wengi kuliko ACT huko Kigoma then unasema watakuwa tishio kwa Chadema??

Anyway maadam wote ni upinzani then watasaidia kuiua CCM ila kama wataenda ACT Ili kupambana na CHADEMA basi watafutika kama tu Slaa,Mashinji, Kafulila, na Lijualikali walivyopotea.

Mkuu mbona umeenda nje ya topic na uko too defensive? Wapi nimesema watakuwa tishio kwa CHADEMA au kupambana nayo? Labda kama umequote kimakosa.
 
Kazi ya mwanasiasa ni kufanya siasa.

Maamuzi ya mwisho ya kuwavua uwanachama wa CHADEMA wabunge Halima Mdee na wenzake 18 baada ya rufaa yao kukataliwa, huenda yakawatoa rasmi kwenye siasa za vyama, hivyo kulazimika kutetea ubunge wao mahakamani kwa ajili ya kusogeza siku mbele kuelekea 2025.

Labda wengi wanajiuliza au wengine wanadhani huu ndio mwisho wa kisiasa kwa wanasiasa hawa wazoefu na machachari. Kisiasa, hesabu nzuri zaidi ni wanawake hawa kuhamia chama cha ACT ili wapate jukwaa halali la kuendelea kuwa relevant kwenye siasa za upinzani na uwakilishi hapa nchini.

Jambo la muhimu zaidi, maamuzi ya CHADEMA yaheshimiwe.
Vyama vya upinzani ni vyama vya maslahi ndio maana huwa ni kufukuzana kila siku na havieleweki ..

Vinapanda vinashuka huu ni utoto na immature.
 
Naunga mkono hoja, baadhi yao, akiwemo Halima Mdee na Esta Bulaya, hawa ni wanasiasa very good assets kisiasa, Chadema turned these assets into liabilities. Kama hawakutendewa haki, kiukweli kabisa, karma itaitafuna Chadema!.
Karibu mitaa hii A Kangaroo Court Moja, Kutoa Hukumu Kikangaroo, Kisha Kikao cha Rufaa, Kikiyabariki Maamuzi yale ya Kikangaroo. Je, nacho ni A Kangaroo?, dhulma za aina hii, husababisha karma zisizo za lazima kabisa kwa Chadema kama chama, na kwa individual players!.
P.

Binafsi sioni kama wameonewa. Chama kilikuwa very clear tangu mwanzo na wao wakakaza so maamuzi yaliyofanywa ni logical na sio ya kushangaza, kitakachoshangaza ni kama CHADEMA watapeleka majina mengine mapya kwani walishasema kuwa viti maalum kwao ni haramu kutokana na matokeo ya uchaguzi yalivyokuwa. Mtego mzuri sana huu. Ngoja tuone.
 
Unazuia kuondolewa Ubunge na kufungua kesi ya msingi ya kupinga kufukuzwa uanachama!!
Naona kama unachanganya mambo. Kwa hiyo unataka wafungue kesi dhidi ya Bunge ili kulizuia kuwaondolea ubunge? Na hiyo waifanye kabla hawajavuliwa ubunge?
Hiyo ya kupinga kufukuzwa kwenye chama ni haki yao. Lakini haina uhusiano na wao kubakia kuwa wabunge.

Amandla...
 
Back
Top Bottom