For Political Survival, Halima Mdee na wenzake wahamie ACT Wazalendo


Chadema haina shida na Ubunge wao, Cha msingi ni kwamba imewakataa na kwa Sasa chadema Ina mwakilishi mmoja bungeni pekee yake.
 
Jamani Zito alienda Mahakamani kutetea Ubunge wake enzi zile hata Magu hakuwa Rais bado, sijui kwanini binadamu tunasahau haraka, au mna shida gani na hayati Magufuli, muacheni mzee wa watu apumzike kwa amanii

Tofautisha ubunge wa Zitto na Ubunge wa viti maalum ambapo chama ndicho kinapeleka majina, Sasa anayepeleka majina kasema Hawa sio wanachama wangu utafanyaje?.
 

Zitto mwenyewe anaweza kurudi chadema. Maana ACT kabaki pekee yake.
 

You know it is quite interesting that miaka yote CHADEMA haijawahi kukubaliana na matokeo ya Uchaguzi kwa ngazi ya Urais lakini Mbowe, Mnyika and the rest walienda Bungeni kama Wabunge hawajawahi kususia. Ila this one time ambapo wanaume wote “wameshindwa” uchaguzi ndo ubunge eti unasusiwa mazimaa…
 

Hapo umemaliza kabisaaa mkuu.
 
Kama namwona Zitto anavyowatamani waende ht saiv wakajijenge chama, hakika watakuwa wamelamba dume
 
Hii si zama ile, watamalizia hela zao mahakamani bure.
 
Wakitumia mbinu ya kupeleka shauri mahakamani, watavuta muda. Bungeni wapo sana tu. Case study ni kilichotokea kwa Zitto enzi zile.

Huko mahakamani sio kwenda kufungua tu mashitaka, wakitaka wawe wanaishi kabisa huko mahakamani, lakini chama kimeshachukua hatua. Na huko bungeni ni haki yao kwenda kwani walishahongwa huo ubunge kwenye hilo bunge kibogoyo.
 
Kam namwona Zitto anavyowatamani waende ht saiv wakajijenge chama, hakika watakuwa wamelamba dume

Wana haki ya kuhamia chama chochote hata CCM wakitaka, ila kuvuta watu itakuwa ngumu sana maana bado wanategemea washabiki wa cdm ndio wawe watu wao. Zito mwenyewe anaelewa vizuri mziki wa kuvutia watu ulivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…