Watu wanahoji kuhusu S S Bakhresa, kuna mambo kadhaa ya kujua
1. Ili uwe Bilionea kwa viwango vya Forbes ni walau uwe na utajiri wa Dola za Marekani Bilioni moja - $1,000,000,000, 2. Ili uwe Milionea kwa viwango vya Forbes basi walau uwe na utajiri wa kiasi cha Dola za Marekani Milioni moja. ($1,000,000).
Sasa twende taratibu;
Dola Bilioni moja ni shilingi ngapi za Kitanzania(huwa mnaita pesa za madafu) ; kwa mujibu wa BOT leo Dola 1 ya Marekani ni sawa na Shilingi 2339.026 za Tanzania
Hivyo; 1,000,000,000 x 2339.026 = 2,339,026,000,000 Hii ni Trilion 2 Bilion Mia tatu thelathini na tisa na Milioni Ishirini na sita.
Tunakubaliana kuwa Bakhresa ni tajiri lakini katika vyanzo vya Forbes utajiri wake haujafikia hizo Trilion mbili na Bilioni Mia Tatu za Kitanzania ambazo ni walau sawa na Dola Bilioni Moja.
Kwa mujibu wa Forbes utajiri wa Bakhresa unakadiriwa kuwa walau Dola Milioni Mia Sita na Sitini - US 660,000,000 ambazo ni sawa na hela za kitanzania 1,542,420,000,000 Trilioni Moja,Bilion Mia tano arobaini na mbili milioni mia nne ishirini.
Kumbuka Mo Dewji ana walau Trilioni tatu na Bilioni Mia tano za Kitanzania.
Sasa basi; kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali; Orodha ya Matajiri Tanzania ni kama ifuatavyo:
1. Mohamed Dewji - Metl
2. Rostam Aziz - Caspian, Mining, Gas, Telecom - etc
3. Said Salim Bakhressa - Bakhressa Group
4. Reginald Mengi - IPP
5. Ally Awadh - Petroleum
6. Shekhar Kanabar - Synarge
7. Subash Patel - Motisum Group
8. Ghalib Said Mohamed - GSM
9. Fida Hussein - Africarriers
10. Yusuph Manji - Quality Group