Forbes yamtaja Rais Samia Suluhu Hassan katika Wanawake 100 wenye nguvu zaidi duniani mwaka 2021. Yupo nafasi ya 94

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
31C65626-B207-490E-8239-3A721A543E52.jpeg

  • Samia Suluhu Hassan became Tanzania's sixth president and first-ever female leader in March 2021, following the death of President John Magufuli.
  • She rose to the position from vice-president, a role to which she was first elected in 2015.
  • In September, she became just the fifth-ever female African leader to address the U.N. General Assembly. She used her remarks to criticize Covid vaccine inequality.
  • Suluhu has differentiated her leadership from her predecessor by implementing stricter Covid protocols, including mandatory quarantines for travelers coming from countries with new variants.
Source: https://www.forbes.com/power-women/

====

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametajwa na jarida la Forbes kama mmoja wa Wanawake 100 wenye nguvu zaidi duniani kwa mwaka 2021.

Orodha hiyo si kwamba inajumuisha wanawake wenye fedha au madaraka, bali mwanamke aliyetumia kipaji chake, sauti au jukwaa kufanya jambo lenye manufaa kwa jamii.

Katika orodha hiyo Rais Samia ameshika nafasi ya 94 ambapo jarida hilo limeeleza namna alivyotumia jukwaa la Mkutano wa Baraza Mkuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) kukosoa mgawanyo usio sawa wa chanjo za Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO19).

Alihutumia mkutano huo mkubwa duniani ikiwa ni miezi sita tangu alipoingia madarakani kufuatia kifo cha Rais Dkt. John Magufuli, na alikuwa kiongozi mwanamke wa sita kutoka Afrika kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Forbes imetambua namna Rais Samia alivyotofautisha uongozi wake na wa mtangulizi wake katika mapambano dhidi ya UVIKO19, ambapo ametekeleza hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na karantini ya lazima kwa wageni kutoka nchi zenye aina mpya za virusi.

Nafasi ya kwanza kwenye orodha hiyo yupo MacKezie Scott (mtalaka wa Jeff Bezos) ambaye ni mwanamke watatu kwa utajiri duniani. Wengine ni Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, Melinda Gate, Nancy Pelosi, Spika wa Bunge la Wawakilishi la Marekani.

Wanawake wote 100 wametoka katika nchi 30, katika sekta mbalimbali kama teknolojia, fedha, siasa, burudani, wasaidia jamii, na wote wameunganishwa kutokana na utendaji wao.

Chanzo: Swahili Times
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametajwa na jarida la Forbes kama mmoja wa Wanawake 100 wenye nguvu zaidi duniani kwa mwaka 2021...
Hongera kwa Rais Samia. Hii ni alama ya utambuzi na kueleweka kwa utendaji kazi wake.
 
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametajwa na jarida la Forbes kama mmoja wa Wanawake 100 wenye nguvu zaidi duniani kwa mwaka 2021...
Kwa katiba ya Tanzania ya sasa lazima awe ndo anaongoza kua na nguvu kuliko wote. Katiba ya TZ anamfanya raisi yoyote alioko madarakani kua kama godfather.
 
Kuna muda huwa ninahisi Forbes huwa wanahongwa nao ili wawarushe baadhi ya mastar
 
20211207_202718.jpg

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametajwa na jarida la Forbes kama mmoja wa Wanawake 100 wenye nguvu zaidi duniani kwa mwaka 2021.

Orodha hiyo si kwamba inajumuisha wanawake wenye fedha au madaraka, bali mwanamke aliyetumia kipaji chake, sauti au jukwaa kufanya jambo lenye manufaa kwa jamii.

Katika orodha hiyo Rais Samia ameshika nafasi ya 94 ambapo jarida hilo limeeleza namna alivyotumia jukwaa la Mkutano wa Baraza Mkuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) kukosoa mgawanyo usio sawa wa chanjo za Ugonjwa wa Virusi vya Korona (UVIKO19).

Alihutubia mkutano huo mkubwa duniani ikiwa ni miezi sita tangu alipoingia madarakani kufuatia kifo cha Rais Dkt. John Magufuli, na alikuwa kiongozi mwanamke wa sita kutoka Afrika kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Forbes imetambua namna Rais Samia alivyotofautisha uongozi wake na wa mtangulizi wake katika mapambano dhidi ya UVIKO19, ambapo ametekeleza hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na karantini ya lazima kwa wageni kutoka nchi zenye aina mpya za virusi.

Nafasi ya kwanza kwenye orodha hiyo yupo MacKezie Scott (mtalaka wa Jeff Bezos) ambaye ni mwanamke watatu kwa utajiri duniani. Wengine ni Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, Melinda Gate, Nancy Pelosi, Spika wa Bunge la Wawakilishi la Marekani.

Wanawake wote 100 wametoka katika nchi 30, katika sekta mbalimbali kama teknolojia, fedha, siasa, burudani, wasaidia jamii, na wote wameunganishwa kutokana na utendaji wao.

Source: https://www.forbes.com/power-women/
 
Kilemba Cha Ukoka.

Kwa maana sio kila anayekusifia basi anania njema na wewe.

Watch Out Madam President.

Tunatoka kweye 'Bad' tunaelekea kwenye 'Worse'.
 
Back
Top Bottom