Forbes yamtaja Rais Samia Suluhu Hassan katika Wanawake 100 wenye nguvu zaidi duniani mwaka 2021. Yupo nafasi ya 94

Mtangazaji mashuhuri Zuhura Yunus wa BBC amesema Rais Samia ameingia katika orodha ya Wanawake 100 wenye ushawishi zaidi duniani kutokana na namna alivyolishughulikia kwa weledi mkubwa swala la Corona nchini Tanzania

Orodha hiyo imeandaliwa na Forbes na Rais Samia amekamata nafasi ya 94, anasema Zuhura.

Source: BBC Dira ya Dunia
 
Wanatuchanganya hawa watu,juzi wametangaza kuwa Tanzania siyo Nchi salama kwa kutembelea baada ya kutochukuwa hatua za COVID,Leo yamekuwa hayo Tena?
 
... ukiacha suala la uwanawake, yeye na JPM nani alishughulikia Covid-19 kwa weledi zaidi?
 
Huo ushawishi wake umemsaidia nini mtanzania wa kasimbo,Tandahimba,kipili nk kupata huduma bora za jamii ? na kupunguza mfumuko wa bei.?
 
Hili jarida ni la mchongo , amefanikisha wangap kuchanja?
 
Kaziiendelee
 
Umeme Mbeya ni Shiida,,Weka Huku umaarufu wako Kila Siku Umeme hamna.
 
Kaziiendelee Tanzania
 
Kusadikika "Shabaan Robert"
Kivuli Kinaishi "xxxx xxxx".

Naanza kufuatilia kwa karibu Forbes naona kama mali ya Benson Banna
 
Ukiwa Rais lazima uwe na nguvu unakosaje nguvu wakati kila kilichomo ndani ya nchi ni chako
 
Sema tu Samia Suluhu ameiba hela. Toka lini Forbes wanajishughulisha na watu wenyr nguvu?
 
Least and last! 94/100. Daah! Who is that woman 1/100?
 
#2025Fever itawapotezea muda wenu bure,hakuna wakumuangusha Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi hizi kubwa na nzuri anazozifanya,

#KAZIIENDELEE NA MAMA
 
Kama mambo ndio haya basi Tanzania kama kuna wakati tumepata Rais bora na wa kweli nadhani ni sasa,Tufanye kazi kwa bidii sana,

Hakika huyu Mama ni Mpango wa Mungu,

#WATANZANIA TUFANYE KAZI KWA BIDII
 
" Kwa mwendo huu Tanzania tutafika tunakotaka kwenda tena kwa kuwahi sana, Hongera Mama Samia, Watanzania tuko nyuma yako We chapa kazi achana na Wasio na jema "
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…