Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
Siye wajuvi wa masuala ya ujenzi tulionya na kuonya, tukaambiwa tunatetea ulaji wetu.
Kuna wawakilishi wetu tuliwatuma hadi Bungeni kupinga Force Accout , lakini walibezwa kuwa makandarasi ni mafisadi wa fedhe za umma.
Sasa kazi nyingi zilifanywa kwa spidi kubwa kwa kumtumia fundi Maiko.
Madudu sasa yanaonekana wazi kwa kupata kazi iliyo chini sana katika viwango, na fedha kuliwa vibaya na wasimamizi na mabosi, kuanzia ma DED hadi Madaktari na waalimu.
Kuna waliofungwa, kama yule mwalimu huko Musoma, na wengine kesi zao ziko Mahakamani na zingine kuendelea kuchunguzwa na TAKUKURU.
Tatizo kubwa ni wanasiasa kujifikiria wana akili kubwa kuzidi zile time tested project administration methods na procedures.
Sasa hela za serikali zimeliwa na wajanja kwa vile supervision systems za kifedha na kiujenzi ni very very poor au hakuna kabisa!
Sasa hivi hata Waziri Mkuu kachoka, anatembelea miradi pamoja na TAKUKURU ikiwepo, kila mradi ni madudu ya kutosha.
Mifano michache:
-Waziri Mkuu alitembelea mradi wa hospitali huko Songea. milango ilikuwa haifungi-fundi Maiko huyo na daktari kachukuliwa na TAKUKURU
-Huko Tabora , VETA, jengo la mlinzi milioni 11, msimamizi kachukuliwa na TAKUKURU
-Huko Katavi juzi nyaraka zimechomwa moto kuficha ulaji baada ya kumtumia fundi Maiko, TAKUKURU wamepewa kibarua
-Huko Tanga Mkuu wa Mkoa kawapiga wanted ma DED wawili kwa kufanya kazi na fundi Maiko na jengo likawa ndivyo sivyo, TAKUKURU wameitwa
-Huko Ruangwa, kazi ya fundi Maiko, jengo halina madirisha wala milango, Ths 75 million imaeliwa, TAKUKURU wamepewa kazi
-Huko Ikungi fundi Maiko kajenga jengo la Tsha 500milion ndivyo sivyo, DC kawapeleka TAKUKURU
-Huko Mwanza Mkuu wa Mkoa kawaita TAKUKURU, jengo la abiria, uwanja wa ndege kujengwa chini ya viwango na kusua kusua, hela imeliwa, fundi Maiko anachekelea
Kwa sababu hata hawa wanasiasa wetu haawajui waende wapi wa kukiuka taratibu za ujenzi, inabidi wakumbushwe kuwa TAKUKURU hawana muarobaini wa namna ya kurekebisha taratibu zilizopindwa katika ujenzi
Na kosa kubwa ni hao hao wanasiasa.
Force Account kwa kumtumia fundi Maiko imeleta hasara kubwa sana kwa Taifa.
Tunaiomba serikali, hasa wanasiasa, wadhibitiwe na sheria zinazohusu sekta hii ya ujenzi.
Bodi husika za Wizara ya Ujenzi, CRB. AQRB, ERB, NCC zina kazi kubwa kuwaelimisha wanasiasa wanaoingilia kiutendaji uendeshaji wa sekta ya ujenzi.