Jidu La Mabambasi
JF-Expert Member
- Oct 20, 2014
- 16,419
- 26,594
- Thread starter
- #21
Safi sana ulivyoidadavua, lakini ulichoongea ni hewa tupu.Umeongea kisiasa na kishabiki zaidi kuliko kitaalamu!!!
Muundo wa FORCE AACOUNT unataka Ujenzi ufanyike kwa kusimamiwa na Kamati za Ujenzi wa mradi; yaani
1. Kamati ya Ujenzi/Kamati ya usimamizi
2. Kamati ya Manunuzi
3. Kamati ya UKAGUZI na mapokezi.
Aidha best practices ni PROCURING ENTITIES kufanya screening za mafundi Wazuri na kuwaajiri kwenye kazi ya Ujenzi chini ya usimamizi wa Mhandisi wa PROCURING ENTITY....
Fundi anatakiwa kuwa na ujuzi na uzoefu wa kutosha na mwenye UWEZO WA KUSOMA RAMANI NA MICHORO na kuitafsiri kwa USAHIHI.
Wakati wa Utekelezaji wa Mradi Mhandisi wa PROCURING ENTITY anatakiwa kuwepo kwenye hatua zote muhimu kama
1. Wakati wa kuseti msingi
2. Kumwaga jamvi
3. Kuseti ukuta
4. Kwenye concrete zote
5. Kuseti paa n.k
Ukiangalia kwa Uhalisia Utaratibu wa Force account ni mzuri SHIDA NI WASIMAMIZI KUTANGULIZA MASLAHI BINAFSI KULIKO MASLAHI YA UMMAH.
Kununuliwa milango mibovu FUNDI ANAHUSIKA VIPI? Hapa maana yake Wasimamizi wametaka kitu cha bei RAHISI ili wapige HELA!!!!
Kwani MAJUMBA yetu hatujengi kwa kuwatumia hawa MAFUNDI????
UNATAKA KUNIAMBIA KILA NYUMBA NZURI ILIYOJENGWA MTAANI AMETUMIKA MHANDISI ALIYESAJILIWA EQRB, ARB, ERB, NCC n.k?
Mbona Miradi yetu Binafsi hatuweki milango ya hivyo? Au kwenye miradi ya Ujenzi ya UMMA HUWA WATAALAM WETU WANAGEUKA WATU TOFAUTI????
Ninachokiona ni KUENDELEA KUMOMONYOKA KWA UZALENDO MIONGONI WA WATUMISHI WA UMMA NA KUTANGULIZA ZAIDI MASLAHI BINAFSI.
NI KWELI FORCE ACCOUNT inakosesha WAKANDARASI FURSA ZA KUFANYA KAZI LAKINI HATUPASWI KUWA NA USHABIKI HASA KWENYE JAMBO LA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA TAIFA LETU..
Lakini kwa upande wa Wakandarasi nao ni vilevile Kwani tunashuhudia
1. Miundombinu inajengwa na baadhi ya WAKANDARASI ikiwa haina viwango...
2. Gharama kubwa mno za Ujenzi wa miundombinu
Ifike wakati tutatoa TATIZO NA SII KUKWEPA ILI TUENDELEE KULINDA MASLAHI YETU BINAFSI.
Unawezaje kujenga kwa Force Account mradi hadi wa bilioni 10 kwa kumtumia Afisa manunuzi, fundi Maiko na wasimamizi Kamati ya Ulinzi na Usalama.
Halafu leo tunashangaa TAKUKURU wanaitwa kila mradi wa Force Account!
Tunaona makosa lakini hatuelewi!!
Huu ndio ujinga usiokifani watu kujijengea uhalali wa kusimamia fedha za miradi ambapo sasa tunampa Waziri Mkuu kutembelea miradi akiambatana na TAKUKURU badala ya kusimamia proffessionals wa Project Management na Supervision.
Kwa hii hoja hata ukiamua kujitengenezea utaratibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama kusimamia urukaji wa ndege ni sawa tu maana wanajitengenezea ulaji.
Kwa kifupi hoja hii haina mantiki wala uhalali.