Force account ina changamoto zake lakini pia Lina faida, mtazamo wangu Mimi mfumo huu unatakiwa kuboreshwa sio kufutwa
mfumo wa force account unatumia nusu ya gharama na Kwa kiasi flan unaiona thaman ya hela, nitoe mifano kwenye ujenzi wa madarasa, madarasa ya zamani miaka ya 2000s kuja 2016 yalikua yanajengwa Kwa mil 40 Kwa kutumia contractors Ila ndio hayana ubora kabisa. Mfano madarasa hayo hayana vigae, hayana gypsum board wala madirisha ya alluminium na bado mtu alikula M40, Ila ya sasa ya mil 20 ni Bora na thaman ya hela inaonekana.
Kwa hela inayotengwa kwenye ujenzi wa force account ukitumia njia ya zaman huwez kujenga Kwanza hakna engineer atakubali kujenga Kwa gharama hizo na akijenga bas jengo litakua bovu Zaid hata ya hili la kamati ya ujenzi.
Shida ya ninayoiona Mimi ni serikali kutenga hela ndogo ya ujenzi. Mfano darasa moja 20 hapo kuwe na kigae, dirisha alluminium, rangi, board na madawati 40. Wajamen hapo hakuna mtu anaweza kusimamia jengo likawa Bora kama mnavyotaka. Heb kwenye mil 20 toa 500,000 ya usafiri wa vifaa, 500,000 maji, fundi kuanzia msingi,Boma,kupaua, board,rangi, kigae tumbane m3, kiti na meza tukadirie 60, 000@ kiti Viti 40 ni mil 2.4, tofali 6" 1500@tsh 1500 ni Zaid ya mil 2, kokoto trip 6 @250,000 hapo ni mil 1.5, Mawe trip 8@100,00 inakua laki 8, mchanga trip 15 kila trip tufanye 80,000 inakua mil 1.2, simenti 42.5N mifuko 110 kila mfuko 22,000 hapo tena ni mil 2.4, kigae box 45@ 32,000 hapo ni mil 1.4 hiv. dirisha aluminium complete kadiria 250,000 dirisha madirisha 5 ni m1.2 Hadi hapo ushatumia Zaid ya m17, hapo bado hujanunua board, mikanda, mbao, Bati, rangi, nondo, misumari nk.
kimsingi tutalaumu mfumo Ila shida sio mfumo bajeti imefinywa Sana, wanakamati hawajetengewa hata posho Yan mtu asimamie mwez mzima, wafate vifaa, waandikie malipo ya fundi Af wasipate kitu, wakijilipa kwenye hiyo hiyo M20 wanajilipa hela ndogo Sana na haiathiri ubora wa jengo, jengo limeathiriwa na bajeti ndogo. Engineer wa wilaya anayendaa BOQ analazimisha M20 itoshe kujenga darasa moja, matokeo yke anapunguza idadi, materials watu wakienda kununua havitoshi, Bati mtaongeza, misumari mtaongeza, mbao, board, rangi mtaongeza. Yan lazma hela itoke kwenye chanzo kingine kumalizia jengo.
Uzalendo sitaki kuongelea, sidhan kama kuna mtu anao hapa. Serikali iongeze hela ya ujenzi, waweke na posho ya kamati ili wasile kwenye material wala Kwa hela ya fundi. Force account inasingiziwa Tu Ila hela hiyo inayotengwa Kwa ujenzi haiwez kujenga Kwa ubora stahiki. Wanakamati wanachukuliwa hatua, wanalipishwa, wanawekwa ndani Ila hawana shida kama wanajilipa ni kidogo Sana hakiendani na kazi wanayofanya.
Wanasiasa kuingilia shughuli za ujenzi- nayo ni shida nyingine, Yan jengo huku linapauliwa huku linawekwa kigae, huku lipu huku rangi , hata kama local fundi anajua kanuni za ujenzi- Ila hapo anatakiwa kutii maelekezo ya wanasiasa ubora utatokea wap.
Nilikua kiongozi wa taasisi Ila nilifikia hatua nikaomba kupumzika maana kuna muda unaongeza mpaka hela yako ujenzi ukamilike ilimradi uwafuraishe maboss na bado wakija wakaguzi lawama kibao, mtaani mnazushiwa mnaiba hela ya mradi, Yan ukinunua Gari kosa, ukijenga kosa kila unachofanya wanasema hela ya ujenzi ndo imefanya.
Mfumo wa force account Una faida nyingi kuliko hasara, unahitaji maboresho kiasi ili kuleta tija