Forex: Biashara Yenye Utajiri Mkubwa Zaidi Duniani Ambayo Hakuna Benki Itataka Uijue!

Status
Not open for further replies.
Kwa hiyo ulitaka kusemaje.......au mi sijakuelewa?
 
mkuu hebu kuwa muwazi tupe knowledge zaidi,swala langu hii App unatumia,tufahamishe umecheza kivipi,thanks
Kuna member mmoja humu nilimwambia ni app ipi hiyo, anyway ni meta trader 4 ipo play store.
Kuhusu kujua kucheza soma soma soma. Anza currency trading for dummies kisha soma naked forex hapo utapata picha halisi nn hasa cha kufanya. Mimi natumia naangalia trend ya price action kisha naidentify the lowest and highest prices kwa kipindi kifupi cha nyuma kisha najua kwa hapa price iliposhuka haiwezi kushuka zaidi isipokuwa kama kuona new economic release, hapo Nina buy Mara ninapoona imereverse. Kisha naanza kumeneji risk
 



Tuliacha kuzungumzia habari za watu, coz hiyo sio focus yetu... malengo yetu ni kuwa na deep knowledge na kutumia hiyo knowledge kuleta mabadiliko ya kiuchumi among Tanzanian. Lkn kwakuwa uzushi ukizungumzwa bila kukanushwa unabadilika kuwa ukweli.

Kwanza kabisa niseme humjui Sandile shezi, hufahamu hata kitu mpk ugoogle na yawezekana hata baada ya kugoogle hujaelewa kilichoandikwa.

Sandile anatumia broker mmoja... mmoja tu na anaitwa TD markets, ni brokerage firm ya SA. Unazungumza AMC, hiko kitu hakipo, acha nikueleweshe. Kuna kitu kinaitwa AMG African Medallion Group, hii si brokerage company bali kampuni ya kwanza Africa kuzindua crypto currency yake inayoitwa AMG. Nikisema crypto currency kama huelewi ni Digital Money kama Bitcoin, ByteCoin, DigiByte, ReddCoin, PeerCoin nk.

Sasa Sandile mwaka huu kalipa mamilioni ya kutosha kununua shares kwenye hiyo kampuni, katoa pesa ndefu sana sana ambayo mpk sasa haijawa disclosed. Hakuna mtu amewahi kulalamika kuhusu hilo, sijui hata unaongea nini...

Kuhusu kucopy utirio, ni kweli Sandile syllabus yake baadhi ya vitu alitoa kwenye web ya Babypips.com. Kitu ambacho alikosea labda ni kutoku-acknowledged, jambo ambalo si geni sana. By the way hakuna mtu anaweza kutengeneza 100% learning syllabus kutoka kwenye kichwa chake, lazima kufanya literature search nk. So sidhani hilo nalo ni jambo la kukomalia, watu wanacopy Thesis na dissertation za PhD sembuse learning materials za kuwafundisha wanafunzi wako.

Boss kajipange upya... tuhamie kwenye facts tuache hbr za watu.
 
Thanks bro,Among many you are the one.....
 
Moja ya matamanio yangu baada ya mwaka mmoja tunakuwa na Forex Club of Tanzania.
Tunasafiri popote duniani kukutana na Forex Traders toka nchi mbalimbali kubadilishana uzoefu..
Hata kuenjoy, maisha yenyewe ndo hayahaya..
Mkuu bavaria na salute kwako kwani roho yako ni nyeupe sana huna roho ya kimaskini unataka watu watoke kama alivyo Ontario
 
Mkuu hii kitu imenivutia sana ningependa kujumuika kuwa Kati ya watu 300 wa mwanzo kujifunza kuhusu forex...hongera sana
 
Nimeona lazima niwe mkali ktk hili

Dear traders,

Jana jioni nilikua nina appointment na jamaa yangu wa faida, rafiki yangu wa muda mrefu hapa JF na subscriber wa huu uzi. Tukazungumza sana kama masaa mawili hivi, akaona napiga live trade mbele yake, macho yakamtoka kweli kweli, kidogo azimie, hahaaa!! Jokes[emoji23]

Nifupishe habari, baada ya maongezi nikaingia Mary brown kupata msosi then niingie church. Sasa nilivyokuwa pale Mary Brown kuna jambo la ajabu sana nililiona na lilinishangaza mno. Very coincidentally!!

Kulikuwa na jamaa mmoja, amekusanya wadada wa2 na wakaka 6, anazungumza kuhusu forex. Kadri alivyozidi kuzungumzo ndipo alipozidi kuniattract. Kilichonishangaza ni hiki -

kuna mdada mmoja pale akauliza, hii forex unayozungumza ni real kweli ama ni blah blah. Basi huyo jamaa alichokifanya akasema ngoja niwaoneshe kitu, akatoa simu yake akaanza kusema "Unaona huu uzi, niliupost kwenye mtandao mmoja unaitwa JF, nilipost kuhusu hii habari ya forex, na mpk sasa huu uzi umesomwa mara 170,000".

Mimi sikuamini macho yangu, jamaa akaja kwenye post fulani ya jana ambayo nilipost withdraw ya £500, jamaa anawasisitizia hao watu wake kua ile ni faida yake ya siku 1.

I was so shocked, sikutaka kuleta timbwili ama kumdhalilisha mtu, ni mtu anayetokea humu humu. Anafahamu mpk operations zng nje ya forex. Yani nilishangaa mno. Sikatazi mtu kumfundisha mtu mwingine kuhusu forex, that's non of my concern, lkn kwanini mtu atumie jina langu.

Sijajibu PM yoyote ya mtu kuhusu Forex, sijatoa number yoyote ya simu zangu ama mawasiliano yoyote, sijaunda group lolote lile kuhusu forex. Fanya chochote huko nje at your own risk. Usidanganye/usidangamywe kwa mgongo wa jina la Ontario.

Mimi nikimaliza process zote tutataarifiana, kila kitu kitafanyika ofisini, classes zote zitafanyika ofisini, sitoi personal appointment sehemu yoyote nje ya office. Let's take care.

Salute!!
 

Mkuuuu ungefanya kitu flan. Mpige picha as memory halaf uitume huku tumjue.....
next time hope..
 
That's why i salute you boss..... Working in transparency...
Tunakuombeaa miaka mia mafanikio yako ndo mafanikio yetu
 
Mtzmweusi ili uelewe kinachoendelea humu ,soma comments zote mwanzo mwisho,bila kufanya hivyo ni sawa na kuingia advance class before lower class
 
Duuuh,hii kali!![emoji134] [emoji134] [emoji134]
 
ANKO ELLY HAMTUMFUATI MTU TUNAIFUATA BIASHARA,JIULIZE HII BIASHARA DUNIANI IPO ? JIBU IPO,WATU WANAPATA PESA ? JIBU NDIYO WANAPIGA KWANINI MIMK NA WEWE TUSIPATE?JIBU WOGA WAKO NDIYO UMASIKINI WAKO JIFUNZE KWA WALIOFANIKIWA,JE IPO TAASISI AU MTY YOYOTE WA KARIBU ANAYETOA MAFUNZO KUHUSU BIASHARA HII ? JIBU HAKUNA ISIPOKUWA KUNA MSAMARIA MWEMA ANAITWA ONTARIO KAJITOLEA KUANZISHA MAFUNZO HAPA DAR NA HIVI SASA KATUFUMBUA MACHO TUENDELEE KUSOMA VITABU ,MITANDAO NA KUJADILIANA BEFORE CLASS TRAINING,SASA NAKUULIZA WEWE SISI NA ONTARIO TUMEKOSEA WAPI? NAKUONYA ACHA KUKURUPUKA SISI SIO WATOTO WADOGO
 
Leo nimekaa nikawa najiuliza! INAKUAJE MTU UNACHOMA ACCOUNT?? yaani unapata hasara?!!

So far nnavyojua huwezi kuuza bila wewe mwenyewe kwa kichwa chako kubonyeza kitufe cha SELL au BUY!

Ivi kama nikiona nachezea negative red which means ni hasara....nikaacha mpaka ije ipande au ishuke irudi kwenye blue then ni excute order kwa faida...inakua kosa??

Sasa kwann mtu uuze au ununue kwa hasara?? Wakati unaweza kuacha ukashuka weee then badae ikapanda thamani ili uuze kwa faida??

Cheki huu mfano...

Hizi ni positions kama tatu hivi na zote zina loss ...ziko kwenye red!

Kwa hapo sintauza wala kuuza mpaka thamani ipande au ishuke ili niuze kwa faida...ikiwa kwenye blue!!

Embu nielewesheni wakuu...INAKUAJE UNAPATA LOSS AU UNACHOMA ACCOUNT???

Labda nakosea...naomba mnieleweshe wadau!!
 


Mkuu hili ulishaeleweka ndio maana mimi nasubiri tangazo, hao ni wavivu wa kutafuta facts ndio maana wanaingia mkenge kirahisi, anayekufuatilia kila hatua hawezi kudanganyika kirahisi yaani mtu anakuambia amepost ame withdraw some cash kwanini usijiridhishe on your own kuusoma uzi wote uwe 100% sure.

Mkuu fanyia kazi hiyo na Mungu akubless uulete kwa vijana ili tuchoke kumlilia Magu kupiga stop ajira.
 
Hili angalizo limekuja wakati muafaka.

Labda nikuombe weka angalizo hili pia kwenye post namba moja hapo juu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…