Nimeona lazima niwe mkali ktk hili
Dear traders,
Jana jioni nilikua nina appointment na jamaa yangu wa faida, rafiki yangu wa muda mrefu hapa JF na subscriber wa huu uzi. Tukazungumza sana kama masaa mawili hivi, akaona napiga live trade mbele yake, macho yakamtoka kweli kweli, kidogo azimie, hahaaa!! Jokes[emoji23]
Nifupishe habari, baada ya maongezi nikaingia Mary brown kupata msosi then niingie church. Sasa nilivyokuwa pale Mary Brown kuna jambo la ajabu sana nililiona na lilinishangaza mno. Very coincidentally!!
Kulikuwa na jamaa mmoja, amekusanya wadada wa2 na wakaka 6, anazungumza kuhusu forex. Kadri alivyozidi kuzungumzo ndipo alipozidi kuniattract. Kilichonishangaza ni hiki -
kuna mdada mmoja pale akauliza, hii forex unayozungumza ni real kweli ama ni blah blah. Basi huyo jamaa alichokifanya akasema ngoja niwaoneshe kitu, akatoa simu yake akaanza kusema "Unaona huu uzi, niliupost kwenye mtandao mmoja unaitwa JF, nilipost kuhusu hii habari ya forex, na mpk sasa huu uzi umesomwa mara 170,000".
Mimi sikuamini macho yangu, jamaa akaja kwenye post fulani ya jana ambayo nilipost withdraw ya £500, jamaa anawasisitizia hao watu wake kua ile ni faida yake ya siku 1.
I was so shocked, sikutaka kuleta timbwili ama kumdhalilisha mtu, ni mtu anayetokea humu humu. Anafahamu mpk operations zng nje ya forex. Yani nilishangaa mno. Sikatazi mtu kumfundisha mtu mwingine kuhusu forex, that's non of my concern, lkn kwanini mtu atumie jina langu.
Sijajibu PM yoyote ya mtu kuhusu Forex, sijatoa number yoyote ya simu zangu ama mawasiliano yoyote, sijaunda group lolote lile kuhusu forex. Fanya chochote huko nje at your own risk. Usidanganye/usidangamywe kwa mgongo wa jina la Ontario.
Mimi nikimaliza process zote tutataarifiana, kila kitu kitafanyika ofisini, classes zote zitafanyika ofisini, sitoi personal appointment sehemu yoyote nje ya office. Let's take care.
Salute!!