Ni Ontario boss.
Watu wazembe kama wewe mtakuja kunisumbua darasani na kunichafulia jina. Uzi una post 2600 unashindwa kusoma, utaweza kumaliza page 660 ya Bible of a trader?!
Nilishatoka kwenye 300, nipo kwenye 150.
Kila mwenye nia ya kujifunza na kubadili knowledge into reality ndio watakaopata fursa ya kunijoin. Sitaki kuwa kama syllabus za Kibongo mtu anasoma miaka 17-20 lkn akitoka shule hajui nini kinafata. I want real traders - na real traders mpk sasa atakua anajua ABC kuhusu forex. Hakuna nafasi nitakazotoa kama sanda kalawe - watoto wenye akili za kiInstagram hii kitu haitawahusu, I need serious people who know what life means.
Pili haya mafunzo hayatakuwa ya batch 1, nitakua sijafanya kitu - sawa na kusema nitakua nimetengeza tu gap kati ya have and have not. Hiki kitu ni continuous, baada ya batch ya kwanza itakuja ya 2, ya 3, ya 4... mpaka tunafika batch 10 hivi by mwisho wa mwaka - lkn hawa itabidi wachangie ela ya AC na umeme.
Na kama alivyopendekeza ndugu yangu
Bavaria, wanafunzi wa batch za mwanzo mwanzo nataka tuanze as soon as possible ili hadi kufika Dec tupange trip ya kwenda Capetown au Durban, yani tunabook SA Airways yote, tunaenda vacation kujipongeza
(I'm only happy when the whole team is winning). Tukifika hatua hiyo nahisi watu wataelewa nini namaanisha. Kuanzia mwakani sasa kila kichwa kitakua kinalipia ada kama ya CPA au school of law. Ndipo tutakapoweza kufungua branch Mwanza, Arusha, Mbeya, Dodoma nk.