Swali zuri,....wadau ni kweli inabidi tuwe makini na hizi bank kwani ukifanya mambo kwa pupa na ku-take easy itakuja kula kwako....Hapa namaanisha nini? Kwa wale ambao wanafungua akaunti za live hakikisha kuwa huyo broker wako atakuwa na njia nzuri ya kukulipa, hapa nina maana kuwa ni lazima ujue kuwa ni njia ipi anatumia broker kukulipa pesa zako pindi pale unakapohitaji ku-withdraw.......nina hakika kila broker ana njia zake za kulipa......najua kuna wengine wanalipa through paypal......wengine wanalipa through kadi yako ya bank ambayo itakuwa Prepaid credit viza card.....na kuna broker wengine wanalipa kupitia Bank tranfer au bank wire system.....Kwahiyo cha msingi hapa ni kuwa makini na broker wako analipa kwa mfumo upi! ambao kwako itakuwa rahisi kupata hizo pesa zako iwapo ukiamua ku-withdraw. Kwani kama nilivyotaadharisha kuwa inawezekana ukashindwa ku-withdraw dola zako kutokana na mfumo ambao broker anatumia kulipa trader.....kivipi? ......Kwa Mfano kuna broker ambao wao wanalipa kupitia PAYPAL MERCHANT TU!.....Na hana njia nyingine ya kulipa zaidi ya hiyo ya kupitisha pesa zako through paypal account yako!.....Je broker anayetumia paypal account unaweza pata pesa zako???.....Jibu ni hapana! huwezi pata pesa zako, kwa sababu Paypal merchant au paypal money processor hawana mkataba wa makubaliano wa kufanya online transaction through kadi zetu za viza au bank za hapa tanzania, kwa sababu hiyo hakuna huwezo wa pesa kuingia kwenye account yako ya paypal na kisha uka-withdraw au ku-transfer pesa kwenye account yako hapa bongo......Kwa wale ambao wanafahamu maswala ya online transaction wanajua ni nini anaongelea hapa.....Ebu naomba mnielewe vizuri hapa....ninaposema kuwa Paypal money processor hawana mkataba au makubaliano.....jua kuwa ni lazima serikali inahusika hapa...kwahiyo hayo makubaliano au mkataba ni lazima waingie na serikali ambayo ndio BOT. Lakini kumbuka kuwa hii paypal kwa Tanzania inafanya kazi lakini ni kwa kufanya malipo ya online tu na si kupokea pesa!.....kwa kutumia paypal account yako ambayo utaifungua basi inayo feature ya kukuwezesha ku-link kadi ya either ya debit viza card au Pre-credit viza au mastercard viza......ambayo sina hakika kama inatolewa hapa tanzania.....kwahiyo kwa ku-link hiyo kadi yako kupitia paypal basi unaweza kufanya mihamala ya online popote paypal account inapohitajika...lakini huwezi kulipwa kupitia paypal kwani hakuna features za ku-transfer au ku-withdraw pesa zako mpaka kwenye account yako ya bank.
Kwahiyo wadau wa Forex Tanzania.....nilitaka kutoa hilo angalizo na muwe makini sana bila hivyo unaweza pata usumbufu mkubwa mno wakati wa ku-withdraw pesa zako..............Sasa je ni mfumo upi ambao unafaha kupokea pesa hapa tanzania??...Hili ndio swali lamsingi....kwani kuhusu kupata viza kadi toka bank ni rahisi sana...na kufanya malipo ni rahisi sana ....lakini kutokana na upeo wangu mdogo ....kupokea pesa au ku-withdraw au cash out kuna matatizo sana......ndio maana nimetoa angalizo la wadau kuwa makini sana wakati unafanya registration kwa broker, hakikisha kuwa inapofikia kuvuna pesa zako basi kusiwe na shida ya kutoa pesa kwa broker na kuingiza kwenye account yako............na hapa sisemei kuhusu kutoa pesa kwenye account yako bank.....nazungumzia jinsi ya kutoa pesa kwa broker wako na kuituma kwenye account yako ya bank,.........ni lazima ujue je broker wako iwapo uki-withdraw ni siku ngapi inachukua mpaka pesa kuingia kwenye account yako ya bank?..........na njia ipi anatumia katika malipo?...je anatumia bank Transfer? au bank wire?....au anatumia money processor kama paypal, payza, perfectmoney, au skrill...na nyinginezo nyingi!.....hapa ndicho kitu cha msingi!...........Mimi ninanavyofahamu kuwa nchi yangu hii Tanzania si rafiki sana katika maswala ya online transaction!...ndio maana ukienda katika local bank zetu unaweza usipate ushirikiano wa kutosha kwa sabau ya kutofahamu haya maswala au ndio sheria zilivyo!.....Mfano.....wenzetu wa kenya wao paypal inafanya kazi hawana kizuizi....wanauwezo wa kulipia na kupokea pesa throuth paypal money procesor..........na hata bank zao...mfano bank ya KCB bank wao hawana shida na paypal,,,,ila shida ipo kwenye taratibu za nchi ambazo haziruhusu kupokea pesa throuth paypal!............wao kama wao bank KCB wanakwambia kuwa kadi zetu za visa zinapkea pesa toka paypal........lakini ikiwepo hapa tanzania haziwezi kupokea kutokana na utaratibu wa nchi....lakini kwa kenya wao hakuna shida !
Je ni njia ipi nzuri ...au njia ipi inatumika kupokea pesa?!!........Kwa mimi na upeo wangu mdogo....nimeona kuna njia mbili tu au tatu za kupokea pesa kwenye account zetu.....moja ni kwa Bank transfer!.............pili kwa viza kadi za bank zenye uwezo wa kupokea pesa nje.....
Kuna aina mbili za hizi viza kadi....kuna masterviza card..............na credit viza card.
Pia kuna aina mbili ya credit viza kadi........kuna pre-paid viza kard..........na debit viza kadi
(A) Ukifungua account ya Foreign exchange au wanaita Forex account....au kibongobongo tunaita account ya dola.......ni lazima utapewa kadi ya debit credit viza card,ambayo hii kadi itakuwa na namba mbili za account.......namba moja ni hiyo ya account ya dola na namba nyingine ni kwa ajili ya kufanya mihamala ya online ...account lakini ni moja tu....sasa account hii faida yake ni kuwa na uhakika wa kupokea pesa kwa hali yoyote ile either kwa bank transfer au kwa kulipwa kupitia viza card yako..........
(B) Ufunguaji wa account ya pre-paid credit viza card ni rahisi sana hapa ni kitambuklisho chako tu either cha taifa au kupigia kura........na ni kwa sh 10,000/= au 15,000/= hivi......
Kwahiyo hapa point yangu ya msingi ni jinsi utakavyolipwa na broker......je kadi yako ya bank je atakubaliana nayo?...na je malipo yatachukua muda gani kufika kwenye account yako?....hivi ni vitu muhimu ku-note!
Kitu kingine cha ku-note ni hiki...........Ni lazima broker atahitaji taarifa zako sahihi ujaze....mfano street address! majina yako kamili..........na kikubwa ni uhakika wa umiliki wako ya hiyo account ambayo anatakiwa kukulipa.......ni lazima umtumie kitambulisho....na kitambulisho wanachohitaji ni lazima kiwe kitambulisho cha taifa........iwapo kitambulisho cha taifa hakiitaji basi ni lazima utumie copy ya paasport yako ikionyesha majina kamili na anwani yako...ili kuthibitisha umiliki wako wa account ambayo yeye anapashwa kupitisha pesa ambazo wewe uta-withdraw...Angalizo...kwa wale wanaotumia kitambulisho cha taifa.... ni majanga...kwani kitambulisho chetu cha taifa hakitambuliki kimataifa.....kina kasoro kubwa mno...kwahiyo hivi vinatumika humu ndani tu.
Mimi naishia hapa!...na huo ndio mtazamo wangu kuhusu maswala ya bank na malipo yoyote mwenye kuongeza au kukosoa taarifa hii ni vyema tu ili sote tuweze kupata mafanikio!.............ila taarifa ilishatolewa kuwa bank nzuri kwa maswala ya online ni FNB....basi ni vyema kufungua huko...kuliko kutegemea bank zetu hizi local ambazo znaweza kukukatalia hata kufanya malipo nje!.......