Nashukuru sana mkuu wangu!
Kuna kipindi nilishaletaga mada kuhusu technical na fundamental kwenye huu uzi siwezi kumbuka ni page gani ila kwa kifupi...
Technical analysis unaangalia market movement basing on price...unaweza tumia tools/indicators kama fibonacci tracement, moving average, RSI an nyingine nyingi kama hizo! Japo ina mapungufu yake ila ni moja ya njia zinazotumika sana kuangalia at what point uingie/ufungue position au muda gani ufunge position! as I said, ina mapungufu yake...
Kuna ingine inaitwa naked forex trade.... hii inatumia price tu, hamna indicators (kasome naked forex trader imeelezewa njema sana)
Fundamental...hii ndo yenyewe na ina impact kubwa sana katika currency husika, both in long and short term! sasa hapa tunaangalia matukio kama wars(refer tension kati ya Kiduku na Trump), terrorists attacks, elections(refer kipindi cha kampen za akina trump na uchaguzi wa UK...terresa May), employment data (refer payrow, NFP), natural calamities (refer mafuriko kule USA na impact yake kwenye bei ya oil) na kubwa zaidi ni interest rates znazotangazwa na bank kuu za nchi fulani mfano benki ya Euro(ECB), Banki kuu ya USA (Fed), banki ya UK na nyingine nyingi!!
Ukitaka kupata fundamental data unaweza tumia hizi web...
Forex Trading News & Analysis
Investing.com - Stock Market Quotes & Financial News
Sentiment analysis...hii imebase sana kwenye mood ya soko au how investors feels about currency movement!! Japo haitumiki sana ila ina inatoa mwelekea wa soko mfano kwa kutumia technical analysis unaweza dhani soko liko hivi kumbe kwa kutumia sentiment analysis unakuta soko liko vingine kabisa....(hapa wadau watailezea zaidi maana sina uzoefu nayo sana mkuu)!!
Ila nakushauri sana upitie kitabu cha astrofx na forex bilbe zimeelezewa vizuri sana humo...
NB: Ni vyema uka tumia analysis zaidi ya moja kujua price movement....
Karibu!!