At least wewe unaongea kama professional ama mtu mwenye uelewa, sio km baadhi ya watu wanatema mashudu hata hawaelewi nini wanasema.
Umetukumbusha tena kitu ambacho nimekizungumza hapa mara kadhaa, kua forex inahitaji dedication sana sana sana.
Nirudi kwenye hoja zako ulizozinumber.
1. Kwanza naomba usipindishe maneno, sielewi kama umekosea ama umekusudia. Hii ni continuous thing ambayo itarun kwa decades za kutosha, unaposema nafungua office ya kutrain wa2 300 bure unakua umenimisquote. Nimesema natoa special offer kwajili ya member 300 kutoka JF, wapate training then nitakua nao benet kuhakikisha wanamake profitable trades. Baada ya hapo programme itaanza rasmi - tutaingiza wanafunzi wa kutosha tu, na sitawapa free trainings. Nitawacharge kitu kidogo ambacho tutaona inafaa kwao na kwetu pia.
Mimi kumleta broker ni kurahisisha mambo. Huwezi ukamtrain mtu hasa mbongo ambae uelewa wake ni mdogo afu kisha unamwambia broker yupo UK au USA. Hapo ni ngumu , mimi kumleta broker ni katika kufanya vitu kiuhalisia, kwa openness na transparency. Naona unazungumzia mambo ya mimi kuwa IB, cjui nani kasema, na hata kama ni hivyo iko wapi shida?!
Pia kama umesoma vzr post yangu nimegusia kdg type ya broker ambae ninadeal nae. Sijui kama uliona hiyo ama hukuelewa.
2. Boss hii point yako ya 2 imekaa kama kuna kitu you want to prove... yani kuna negativities ambazo hazina logic unaraise.
Mtu mwenye akili timamu hawezi akahoji faida ya Office, mtu anakuchallenge kisa unafungua office afu hapo hapo anasema forex inahitaji knowledge kubwa afu kisha anashauri hiyo knowledge itolewe WhatsApp. Tusiwe na roho ya kwanini - wewe umepata knowledge usichukie uonapo mwenzio nae anatolewa usingizini??
Mimi hii si biashara yng ya kwanza. Hata biashara ya kuku, inabidi uingie gharama ya kujenga mabanda na kuandaa kila kitu ndio uanze kufuga kuku. Wewe umepata hiyo elimu kwa njia zako unazozijua wewe, haimaanishi njia zingine ni za kipvmbavu. Yani unanishauri nichukue watu 300 then niwafundishe forex kwa group la WhatsApp na si kufungua office afu niwadirect kwa broker ambae hata hawajui alipo au anaoperate vipi.
Biashara yoyote lazima ugharamie, mimi kupanga office space, kuleta mentors nk ni 1 ya vitu ambavyo nilividraft ili kuhakikisha natengeneza consistent profitable traders na gharama zote nilizipiga. Naweza nisitengeneze pesa leo ama kesho but baada ya mwaka nikiwa nimeestablish mizizi, nina watu TZ wananizungumzia naweza kutengeneza pesa.
If you have any doubts about me, naomba nianze hii kitu ili nikuprove wrong. Nafungua ofisi, natafuta vibali vyote, naleta broker, natrain mamia kwa mamia, nitajitahidi mimi na team yangu tutengeneze traders ambao wataina matunda ya forex, na through the whole process nitatengeneza faida yangu na watu watakua na freedom ya uchumi kuliko leo graduate anagombania remote na mdg wake wa primary.
Mimi kama mimi Ontario nilianza biashara nikiwa bado mdg sana, nilianza na kuku 50 wa broilers, watu walinicheka, wengine wakawa wananidiscourage even my own parents. Leo hii hiyo biashara inakuwa featured Forbes, CNN, BBC World Service, SABC, DW nk. Hata hii nayo siwezi kuishia kati, afe kipa afe beki. Ipo siku watu wote wanaoleta senseless negativities nitawaprove wrong. Nipe miaka miwili tu, yani miezi 24 tu since nikianza.
I will leave a living legacy ya hii biashara kwa hapa TZ - nitakumbukwa si kwa utajiri bali kwa namna nitakavyowafungua watu macho na fikra ktk Global businesses. That alone kwangu ni ushindi mkubwa