Forex: Biashara Yenye Utajiri Mkubwa Zaidi Duniani Ambayo Hakuna Benki Itataka Uijue!

Status
Not open for further replies.
I was passing through the whole thread, page by page, post by post. Am glad that I have done.....

Hongera sana Mkuu kwa hili. Hakika ni jambo ambalo wachache ndiyo wana udhubutu wa kuwaonyesha wengine ili nao wafaidike. Mungu aendelee kukusimamia.

Naona kama nafasi zimeshajaa, ila mimi naomba nafasi moja kuchungulia kutoka nje, yaani kupiga Chabo. Hahahaha.
 
Mimi niko mkoani Mr ONTARIO lakini kwenye suala la fursa niko tayari kwa lolote nikumbuke na mimi kwenye hyo training nami nitafika hapo dar bila kujali umbali.
 
Katika hii dunia nimegundua kuna watu wapo kwa ajili ya discouraged wengine pale wanapotaka kupiga hatua au kuwafungua wengine kutoka katika minyororo.
Kaka Ontario usife moyo,na nimependa msimamo wako Mungu akulinde na akupiganie ili iwe kweli na watu waone kwa macho yao,
Kingine hakuna kumlazimisha mtu au hakuna mtu aliyelazimishwa km anaona hii biashara ina hasara au atafaidishwa Ontario, lakini kati ya sisi ambao tunatamani basi acha tujiandae kujifunza.
 
Mkuu Ontario nmekusoma mwanzo mwisho,nmekuelewa kwa kadri Mungu alivyoniwezesha,japo nahitaji kujifunza zaid,swali langu ni moja tu,hii kitu inaweza kuwa applicable kwa watumish wa umma?pls ukipata nafasi nijibu,Thanks in advance.
 
Watanzania wt wangekua km ww bro onta yani tungekua mbali. Nimesoma comments zako hadi natamani kulia. Mungu akuomgezee, si kila mtu ana moyo km wako wa kusaidia. Live long kk.
 
Mkuu kwanza nashukuru kwa maelezo yako ya kina kwa lengo la kujenga na kuelimisha zaidi..

Lakini tambua nipo pia kwa ajili ya kujenga na kuelimisha kama lengo la Uzi unavyosema, kwahiyo kuwa tofauti kimawazo, kimtazamo na kiuelewa ndio njia pekee ya kujifunza zaidi...

Kwanza naomba nitoe ufafanuzi kulingana na uelewa wangu pamoja na uzoefu wangu katika biashara ya FOREX

1.kwanza nashukuru kwa kudeclare interest kwamba kwa baadae umekusudia kupata faida kwa juhudi ambazo umezianza (Hongera kwa hilo). Jambo la msingi hapa, ni wanajamvi watambue kwanza mbali na hii elimu wanayoipata hapa kutoka kwako lakini pia umekusidia kupata faida baadae kupitia wao au rafiki ama jamaa zao. Hii itawasaidia zaidi kupambanua na kuchambua kwa kina pindi watakapofanya maamuzi ya kuingia katika hii biashara bila kuacha doubts zozote.

Kwahiyo lahi yangu kwa wanajamvi ni kutambua baada ya elimu ya mtoa mada hapo baadae anategemea kupata profits kupitia sisi, marafiki na jamaa zetu (ni jambo jema tu sina doubts maana mtoa mada amekua muwazi ila kazi imebaki kwetu kupambanua)

2.Kuhusu kauli yako ya wabongo kuwa na uelewa mdogo kwamba ni vigumu kumuelimisha kama broker yuko mbali (US or UK).
Hapa mkuu natofautiana na wewe kwa sababu zifuatazo,

Nikianza na Mimi nimeanza kujifunza mpaka nimeingia kwenye hii biashara sijawai kukutana na broker wng ana kwa ana (kumbuka Mimi pia ni miongoni mwa wabongo hao wenye uelewa mdogo lakini Leo nafanya vizuri)

Lakini pia tambua kuwa uelewa wa mtu na kumuona broker ni vitu viwili tofauti. Jambo la msingi hapa ni kumpatia mtu elimu mwisho wa siku ataamua mwenyewe kuitumia au kuiacha. Yaani hapa sisi jukumu letu ni kutoa elimu tu halafu swala la maamuzi ni LA mtu binafsi (mtu anaweza kumuona broker lakini bado asifanye maamuzi mfano mzuri nchi wanazotoka brokers kuna watu wanawaona brokers kila kukicha lakini hawajihusishi na hii biashara japokuwa elimu wanayo)

3. Kuhusu hoja yako ya kusema kwamba sitaki wengine wajifunze si kweli. Ndio maana nipo hapa kwa ajili ya kutoa hii elimu kwa usawa zaidi bila kuegemea upande wowote. By the way sio Mara ya kwanza kushare hii elimu na watanzania wenzangu, wapo nilioshare nao na wengine wanafanya vizuri zaidi yangu (Japokuwa sijawahi kupost hapa Jamiiforum hii inatokana na kutokuwa active sana katika kupost Jamiiforum)
Kwahiyo Mkuu natamani sana watu waipate hii elimu tena kwa ukweli na uwazi ndio maana nimevutiwa na Uzi wako

4.Mwisho nakushauri usifanye personal attack au (kumshambulia kwa ku-base on one side) kwa watu wanaokuwa na mawazo tofauti na wewe (simaanishi umeniattack ila natoa kama ushauri)
Critism ni njia nzuri ya kufanya jambo kuwa more developed.
Hivyo kwa kufanya hivyo itasaidia zaidi watu wasio na uelewa kuifahamu hii biashara kwa undani zaidi..

Zaidi nikutakie kila la kheri katika wazo lako hilo lenye tija kwa umma lakini pia niwatake members wa JF kuwa makini zaidi.
 
Watanzania wt wangekua km ww bro onta yani tungekua mbali. Nimesoma comments zako hadi natamani kulia. Mungu akuomgezee, si kila mtu ana moyo km wako wa kusaidia. Live long kk.
Unatamani kulia nini sasa [emoji23] [emoji23]

Wewe inaonyesha utakuwa miongoni kwa wadau wa mwanzo kabisa kupoteza vijisenti vyenu.
 
Hivyo nyiye mnaojiita wasomi, kwanini mara nyingi hamujadili hoja, kazi mnajisifia na putting down wengine? Mara "mimi nimesoma uchumi, mimi nimesoma finance, wewe hujui!" So what? Kwanini uongelei unachokijua ili tujifunze badala ya kuongelea usomi wako na kuto kujua kwa wengine?
 
Sorry nilikuwa namjibu member mmoja hivi sikuwa na nia ya kutangaza elimu humu jf. Cool down.
 
Ontario kwa elimu nzuri tunasubiri darasa nitakuja na kigoda changu acha niwe wa 302
 
Big Idea inayoitaji kufuatilia na kujifunza kwa umakini kabla ya kuzamisha miguu katika biashara hii.


Kiongozi wangu katika Forex Trading Mr. Ontario Mimi binafsi Niko tayari kuwepo katika shamba darasa lako. Kati ya hao 300 naomba niwe mmoja wao.
 
Hili ndo tatizo la kuajiriwa! Unataka kufanya biashara au unataka kujiridhisha kama anachosema Ontario ni sahihi?
 
Sasa kama broker anakula commission kutoka kwa retailers, inawezekanaje broker apige chapaa wakati huo retailers wake wakiloose? Yaani hapa sijakuelewa kabisa
 
You are less informed man, nahisi sote tunahitaji muda wa kujifunza ili tuelewe vizuri hichi kitu,otherwise you are an extreme pessimist
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…