Naimani mko salama wana JF!
So far so good, achilia mbali kusoma na kujua how to trade au kuwa na capital/pesa kwenye account bado kuna kitu ambacho ni LAZIMA wewe kama trader ujue. Forex inaendeshwa kwa matukio mbali mbali yanyotokea duniani na nnaposema duniani namaanisha mataifa makubwa sio haa yetu ya dunia ya tatu!
Mfano, nakumbuka baada ya Donald trump kushinda uchaguzi (kabla hajaapishwa), soko la hisa na bidhaa mbali mbali duniani hasa USA zilitikisika sana hapa utajiuliza kwanini??
Kuna matukio kama lile la brexit,lile tukio la Uingereza kujitoa kwenye umoja wa Ulaya, japo sikusikia any bad new infact kwasababu sikufwatilia, ila I believe hili tukio lilitikisa sana thamani ya euro na pound!!
Haya turudi tena kwenye chokochoko za china, usa, Russia, iran, North korea na israel. Hizi zote ukiziangalia kwa angle flani zina impact katika forex. Kuna wakati naamini hizi chokochoko zinaanzishwa maksudi ili kutikisa ulimwengu wa flow ya pesa!
Haya turudi huku kwetu, baada ya magufuli kushinda uchaguzi (hata wakati wa kampeni) biashara/makampuni baadhi yalifungwa, je ni kwanini?? Najua wale wenzangu weanaopenda majibu mepesi watadhani wamefunga kwa sababu walikua hawalipi kodi which to some point is not true! Tuangalie lile tukio la ACACIA, baada ya kutokea yaliyotokea jamaa hisa zao zilishuka, je kwanini?? Hapa tuombe wasiende mahakamani na wakashinda kesi maana kwa hasara waliyoipata hawatatuacha salama!
Pia mikutano mbali mbali ya kimataifa kama G7 na G20 ikitokea, kuna mengi yanajadiliwa na kwa upande flani yana impact katika uchumi na siasa ambazo kwa upande Fulani yatapelekea kuyumba au kukua kwa soko la pesa!
Kwa kifupi tu FOREX inaendeshwa na matukio, na matukio haya ni yanagawanyika katika sehemu tatu, yaani siasa/politics, jamii/social na uchumi/economic! Na haya matukio yakitokea jua kuna faida au hasara inatengenezwa.
Bottom line, FOREX imeegemea katika speculation, na kwa trader/speculator mzuri, kuwa na capital tu haitoshi, ni lazima pia ukawa MFWATILIAJI MZURI wa habari na matukio mbali mbali kimataifa hasa ya nchi ziizoendelea na zenye nguvu duniani yaani G7 na G20!
Wasalaam!
Mwenzako katika kujifunza,
LT(Eng.)