Forex: Biashara Yenye Utajiri Mkubwa Zaidi Duniani Ambayo Hakuna Benki Itataka Uijue!

Status
Not open for further replies.
NIMEAMUA KUSOMA HUU UZI NENO PAGE KWA PAGE, POST KWA POST. SIJAONA COMMENT NZURI KULIKO HII.
 
Swali dogo:
Hizo hela za huo utajiri zinatoka nani?
Kwa wasio wazoefu wanaochoma akaunti zao?
Ni rahisi. Mfano leo Bongo US$ 1 inauzwa kwa tshs 2250 na kununuliwa kwa tshs 2200. Sasa mtu anaweza kutarajia Dola itapanda thamani kwa maana kufikia kuuzwa kwa tshs 3000 ifikapo December mwaka huu, hivyo akanunua sasa hivi labda dola zake 1000. Atakuwa ametumia tshs 2,250,000. Akasubiri ikafika hiyo December kweli dola 1 ikawa imepanda mpaka kuwa inauzwa tshs 3000. Huyo mtu akauza zile dola zake 1000 na kupata tshs 3,000,000. Hapo atakuwa amepata faida ya 750,000 nzima kutoka 2,250,000 aliyonunulia.

Kinyume chake kinawezekana, kwa maana alitegeme dola ipande thamani ifikapo december lakini ikashika chini ya aliyonunulia, mfano ikashuka mpaka tshs 2000 kutoka tshs 2250 aliyonunulia. Sasa akitaka kuuza zile dola zake 1000 wkt huo atapata tshs 2,000,000 na hivyo kuw amepata hasara ya 250,000 ktk huo muamala.

Sasa huu mchakato unafanyika globally kwenye system the forex. Broker ndio mnunuzi na muuzaji wako. Ni kama vile unavyoenda Bureau de Change...ukiwa na shikingi unataka dola unapata, ukiwa na dola unataka shilingi unapata.

Natumai nimekujibu swali lako.
 
Mjomba, katika baishara yeyote kuna kitu kinaitwa SWOT Analysis ikiwa na maana ya Strength, Weakness, Opportunity na Threat. Kwahiyo, husiangalie opportunity tu bali lazima uangalie hivyo vingine vitatu au utakwenda alijojo!
SWOT analysis unafanya baada ya kuijua biashara yenyewe .sasa mtu ndo kwnza katoa taarifa lakin wapo wahuni wanadiscredit ..we dont judge books by their covers ..we read the content first and understand!
 
Nimefurahi sana kupata kitu kama hiki hapa JF maana katika kusoma kwangu nimekutana na masomo kama International Finance na vitu kama speculation and arbitrage. Kinadharia najua kitu kwa maana ya kujibu maswali kwa usahihi linapokuja swala mitihani.

Sasa nadhani ni muda muafaka wa kufanyia kazi ujuzi huu kwa vitendo. Nipo Mwanza nasubili ONTARIO kwa kazi. Najiandaa kiakili na kifedha kuanza mbio na kwa kasi yako.
 
Nimesoma hii kitu nilishawahi kuisikia ila nilikuwa sijaelewa leo umenifungua macho japo si sana kwenye watu wako 300 usiniache
 
NIMEAMUA KUSOMA HUU UZI NENO PAGE KWA PAGE, POST KWA POST. SIJAONA COMMENT NZURI KULIKO HII.
Hapo umenena hebu tuwewavumilivu kidogo
Msisahau kuna vitabu sita
Alisafiri mpaka south
Soo tuwe wapole ili ukishaielewa hii shule waweza kopa mkopo mkubwa na ukaufanyia kazi hiyoo na sio kwenda lima ufuta
Isije mwisho watu wakaaja toa lawama zisizo na kichwa watanzania niwazuri kwenye maneno but vitendo sifuri
 
Nashauri Muwambie Ukweli Kabisa Watu wanahitaji Milioni Ngapi Watu wako Excited sana wanaona It real deal I'm warning you Guys! Mimi ni mwalimu wa Haiba ya Michezo I have some advise for you.

Siyo Rahisi wewe Kupata Fedha kirahisi Na sh.200,000 yako na Unaweza Ukaliwa pia ukashangaa ipo sh.196,000. Nashauri kama mna Fedha chache please Fugeni Nguruwe (sorry for Muslims) au Kuku au Unaweza Kufanya Kitu kingine.

Concept yaake ni ya Kawaida Unanunua Pesa ya Kigeni kwa Bei ya Chini na Kuiuza Kwa Bei ya Juu mfano

U$/YEN 1/76.662 Asubuhi
Jioni Unakuta U$/YEN 76.664 hapo siyo lazima jioni Mda wowote ambapo kutakua Kuna Mabadiliko katika Global trade.

Mara nyingi vina badilika hivyo Vipoint vya Mwisho Sasa chukua Calculator 76.654-76.652 hapo Utapata Faida ya $0.002 zidisha Sasa $10,000 (Kiasi Hiki sidhani kama Watu wengi humu wanacho) Hapa ukiuza Utapata faida ya $20 ambayo ni sawa na sh. 44,000 kwa ulivyouza kwa Mtu aliyewekeza kwa $10,000 Sasa Imagine wewe mwenye Mtaji wa sh.1,000,000 uliyefungua Group la WhatsApp tayari ambayo Sawa na $500 Sasa zidisha kwa 0.002 hapo Ujajikuta Unatapa $1 (Toa Pesa ya Kula na Bundle) maana lazima Ukodoe macho. Pia hiyo $ Unaweza Kuipoteza wewe its a win/lose situation Kimsingi

Speculating =Gambling
Mimi si wa Discourage Watu ila Ni vema Kila kitu kikawa Uchi Inspirational Speakers do make things look easier many entered in the game and got fuckedUp!

Nakushauri Vijana wenye pesa ndefu ingieni.
Baadaye Kidogo wakuu!
 
Kwenye email yangu kumejaa msgs kutoka forex na hua wananipigia simu mara kwa mara kunishauri niwekeze kiasi kidogo cha pesa na watakua wakiendelea kunitrain nikiwa tayari nineshawekeza hicho kiasi kidogo ila nilikua naogopa nikinua ni scammers uninishaurije??? Please reply
 
Speculation sio sawa na Gambling mkuu.

Speculation inahusisha na analysis za aina mbalimbali.
Gambling haina analysis yoyote. Unabahatisha, ukipata sawa na ukikosa sawa pia.
 
Kuwa makini mkuu. Usije kulizwa hapo.

Ni broker gani huyo anakupigia simu?
 
Hii itakuwa poa
 
The moment you mentioned Burundi, your whole comment became meaningless!
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…