Hizo sio major currencies.
Kuna siku ( end of summer 2007) nilitoka likizo Tanzania nikawa narudi New York. Kawaida binamu zangu hunikung'uta hela za kibongo nikiwa airport Dar kama bado ninazo.
Siku hiyo nikawa na mambo mengi mizunguko kibao kuaga watu nikawa sijaweza kumaliza hela za Tanzania nilizokuwa nazo, na nikawa naongea na simu njia nzima kwenda Uwanja wa ndege nikajisahau kuwagawia zile hela za Tanzania binamu zangu.
Long story short, nimefika New York nina shilingi 400,000 za Tanzania.
Nikasema hu mchezo mdogo tu, ngoja nitafute Bureau De Change hapa New York nitabadilisha.
Nikaenda 42nd St, nikawaambia nataka kununua dola kwa kutumia 400,000 hela za Tanzania. Wakanikatalia. Kama vile zile hela za Tanzania ni "monopoly money".
Ilibidi nitafute kichaa wangu aliyekuwa anakuja Tanzania nimpe na yeye anipe dola.
Hizi hela zetu wengine katika soko la kimataifa hazipo kabisa, hapo ndipo nilipojifunza.
By the way, nimeuliza kama kuna mtu kashawahi kutumia NADEX hapa, sijapata jibu.
Nadex
By the way 2, I am taking a serious interest in trading Forex, nina vitabu kibao hapa na a NADEX account.
Wanaotaka kubadilishana vitabu let me know.