Forex: Biashara Yenye Utajiri Mkubwa Zaidi Duniani Ambayo Hakuna Benki Itataka Uijue!

Forex: Biashara Yenye Utajiri Mkubwa Zaidi Duniani Ambayo Hakuna Benki Itataka Uijue!

Status
Not open for further replies.
Biashara hii Nayo haina Tofauti na Hisa na Inahitaji Mtaji Mkubwa let say una $10,000 ukipanda kwa $0.05 ndo unaenda Kuuza unapata faida biashara hii Kama una 1,000,000/= Subiri
 
Mkuu kwanza nashukuru kwa maelezo yako ya kina kwa lengo la kujenga na kuelimisha zaidi..

Lakini tambua nipo pia kwa ajili ya kujenga na kuelimisha kama lengo la Uzi unavyosema, kwahiyo kuwa tofauti kimawazo, kimtazamo na kiuelewa ndio njia pekee ya kujifunza zaidi...

Kwanza naomba nitoe ufafanuzi kulingana na uelewa wangu pamoja na uzoefu wangu katika biashara ya FOREX

1.kwanza nashukuru kwa kudeclare interest kwamba kwa baadae umekusudia kupata faida kwa juhudi ambazo umezianza (Hongera kwa hilo). Jambo la msingi hapa, ni wanajamvi watambue kwanza mbali na hii elimu wanayoipata hapa kutoka kwako lakini pia umekusidia kupata faida baadae kupitia wao au rafiki ama jamaa zao. Hii itawasaidia zaidi kupambanua na kuchambua kwa kina pindi watakapofanya maamuzi ya kuingia katika hii biashara bila kuacha doubts zozote.

Kwahiyo lahi yangu kwa wanajamvi ni kutambua baada ya elimu ya mtoa mada hapo baadae anategemea kupata profits kupitia sisi, marafiki na jamaa zetu (ni jambo jema tu sina doubts maana mtoa mada amekua muwazi ila kazi imebaki kwetu kupambanua)

2.Kuhusu kauli yako ya wabongo kuwa na uelewa mdogo kwamba ni vigumu kumuelimisha kama broker yuko mbali (US or UK).
Hapa mkuu natofautiana na wewe kwa sababu zifuatazo,

Nikianza na Mimi nimeanza kujifunza mpaka nimeingia kwenye hii biashara sijawai kukutana na broker wng ana kwa ana (kumbuka Mimi pia ni miongoni mwa wabongo hao wenye uelewa mdogo lakini Leo nafanya vizuri)

Lakini pia tambua kuwa uelewa wa mtu na kumuona broker ni vitu viwili tofauti. Jambo la msingi hapa ni kumpatia mtu elimu mwisho wa siku ataamua mwenyewe kuitumia au kuiacha. Yaani hapa sisi jukumu letu ni kutoa elimu tu halafu swala la maamuzi ni LA mtu binafsi (mtu anaweza kumuona broker lakini bado asifanye maamuzi mfano mzuri nchi wanazotoka brokers kuna watu wanawaona brokers kila kukicha lakini hawajihusishi na hii biashara japokuwa elimu wanayo)

3. Kuhusu hoja yako ya kusema kwamba sitaki wengine wajifunze si kweli. Ndio maana nipo hapa kwa ajili ya kutoa hii elimu kwa usawa zaidi bila kuegemea upande wowote. By the way sio Mara ya kwanza kushare hii elimu na watanzania wenzangu, wapo nilioshare nao na wengine wanafanya vizuri zaidi yangu (Japokuwa sijawahi kupost hapa Jamiiforum hii inatokana na kutokuwa active sana katika kupost Jamiiforum)
Kwahiyo Mkuu natamani sana watu waipate hii elimu tena kwa ukweli na uwazi ndio maana nimevutiwa na Uzi wako

4.Mwisho nakushauri usifanye personal attack au (kumshambulia kwa ku-base on one side) kwa watu wanaokuwa na mawazo tofauti na wewe (simaanishi umeniattack ila natoa kama ushauri)
Critism ni njia nzuri ya kufanya jambo kuwa more developed.
Hivyo kwa kufanya hivyo itasaidia zaidi watu wasio na uelewa kuifahamu hii biashara kwa undani zaidi..

Zaidi nikutakie kila la kheri katika wazo lako hilo lenye tija kwa umma lakini pia niwatake members wa JF kuwa makini zaidi.
Mkuu unaonekana una experience kidogo kuhusu hii biashara ila kwa jinsi ninavyokusoma kwa mbaaali unaonekana hupendi watu wajoin hii biz....yan kiuhalisia unaungana na wale jamaa wa mabank wanaopenda hizi info ziendelee kuwa in curtain.
Nasema hivi kwa sababu katika maelezo yako 70% ni kutujaza uoga na wakati huohuo unasema una uzoefu na hii kitu na kwamba sasa unaendelea vzr,sasa si uwaambie watu kwa namna gani unafaidika kuliko kukatisha watu tamaa? Hivi kuna biashara gani haina risk?

Pili,kufaidika kwa ONTARIO.
Ndugu yangu hivi mtu anaekuletea maarifa ya kifedha na ukayafanyia kazi hayo maarifa kisha ukafaidika kupitia hayo maarifa,meanwhile yule aliyekuletea mchongo pia akafaidika kupitia wewe ubaya upo wapi hapo mkuu,mbona hili swala la Ontario kufaidika wewe limekuuma sana? Mbona zile ada tunazotoa kule shule hazituumi Na ni nani anayeweza kukuhangaikia akutafutie maarifa wewe upate pesa tu bure? Tuache wivu usiokuwa na faida,yaani mimi binafsi kwa jinsi nilivyomuelewa huyu Ontario ningependa atoze fee katika hii training tulipie kwa sababu hata kule shule zinapotozwa ada huwezi fundishwa hii kitu.
Ila nilichofurahi ni kwamba pamoja na risk zilizopo forex ila na wewe bado unaendelea nayo na sasa upo "vizuri"...thanks.
 
Nimekuwa nikifuatilia na kusoma online books mbali mbali regarding forex trading na binary trading.
safi sana kaka tuko pamoja hapo, huu ndo mwelekeo wa 21st century
 
Naona kama umeamua kutuita wateja zako watarajiwa wapumbavu pasipo na sababu yeyote. Mimi nilitegemea jinsi ulivyo mwalimu na mwandishi mzuri ungetumia busara zaidi kutujibu, lakini you lost it kwa kuni refer mimi kama mpumbavu. Bora niwe mpumbavu sasa ili nieleweshwe kuliko kuwa mpumbavu to the end.

Anyway, hebu nieleze nitaweza register vipi kwenye www.forex.com nikiwa kama mtanzania? Hizo MasterCard zitakazotolewa zitakuwa za prepaid au hapana? Kama siyo za prepaid zitakuwa na limit ya kiasi gani? Baada ya kupata training nitaweza tumia platform zipi online na payment card ya namna gani? Je itanipasa kulipia chochote baada ya training?
tatizo una haraka na Papara kama una oga nje mbona jamaa ame eleza vizuri kua kila kitu ata weka sawa ame anza na kutupa vitabu vya kusoma sasa ww hata definition ya Forex huijui unataka kukimbilia kufungua A/C uko www.forex.com izo mambo za mastercard zote alisema ata tolea ufafanuzi
kwa kua huu uzi atakua ana post Updates zote


punguza kiherehere! taratibu tutafika tuu
 
Swali makini sana!
Boss si mbaya ukacheki YouTube videos, zitakutoa tongo tongo kwa kiasi kikubwa sana. Hata mimi binafsi zimenisaidia.

Lakini... kila trader ana strategy yake ya kutrade, sasa ukicheki sana YouTube unaeza ukajikuta unafika point unachanganywa, huyu anasema tumia fibonacci, mwindine anasema tumia lagging indicators, mwingine anasema tumia support and resistance. Sasa unakua huelewi which is which.

Forex unaeza kuanza na kiasi chochote, inaendana na ntu na ntu. Lakini kadri unavyokuwa na balance kubwa ndivyo unavyokua na wigo mpana wa kutrade. Kuna vitu nikiongea hapa hautaelewa viko technical kidogo. But mimi na recommend usiwe na less than $200.

Kuhusu muda wa kuvuna: Forex unavuna kadri unavyotrade winning trades. Unaeza ukaanza na $200 ndani ya wiki 1 (siku 5) una profit ya $500. Na muda wowote unaweza ukawithdraw, unaweza leo ukatrade ukapiga profits $50 na ukaichomoa yote ukafanya mambo yako mengine.
Nimejaribu kucheck You tube confusion ni kubwa mpaka mtu wa kukufundisha tu apatikane.
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Sasa kama broker anakula commission kutoka kwa retailers, inawezekanaje broker apige chapaa wakati huo retailers wake wakiloose? Yaani hapa sijakuelewa kabisa
Amesema brokers wapo wa aina nyingi ila yeye ameainisa wa aina 2 ambao ni market maker na ECN forex broker.
Market maker hawa sio wazuri kwa sababu kuloose kwako ndiyo gain yake
ECN hawa ndiyo wazuri kwamba kufanikiwa kwako ndo faida kwao,na faida zaidi kwako ndiyo faida lukuki kwao na hawapo tayari wewe upate hasara so watakulinda kivyovyote ili usipate lose....me ndiyo nilivyomuelewa mkuu Ontario.
 
Pia mkuu Ontario me nauliza hv,mimi ni mkulima nipo matombo sasa nataka kuvuna nyanya zangu ili nisafirishe kwenda dar sokoni kuuzwa,sasa kabla nyanya sijazichuma nikaamua kupiga simu dar sokoni ili kuuliza bei ya "MASLAHI"....Je hapo si nime'speculate? Nimeuliza hivi nina maana yangu mkuu nisaidie kujibu.
Pili, kuna vigrop viingi vya whatssap sasa hivi vinatoa ushawsishi kwamba eti weka 5000 mpaka 50000 kisha baada ya siku 7 unapokea mara 4 ya ulichoweka,swali langu je hawa jamaa wanaokusanya hizi pesa wanafanya hizi biahara za Forex kama wafanyavyo mabenk pendwa?
 
Hujui lolote mkuu..

Rudi siasani ukabishane..
Mkuu Usione Niko Katika Siasa Ukafikiri Vitu Vingine sivijui Huwa Kuna Slight Change ndogo sana tunavyofanya Swaping ya Currency

Mkuu Niko Vizuri katika hayo Mambo ya Money Markets

Ma Forward Contracts
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom