Aisee nahitaji badly tuition na clues za kuchora trend lines. Nadhani hili ndilo somo nililobakiza linalohitaji nguvu kubwa, na ndiyo milion dollar subject, masomo mengine ni ya kupiga brush tuu juujuu, na yanaeleweka ukiyasoma. Lakini hili la kuchora trend lines ni somo ambalo halipo katika sylabus, na naona ndo topic ngumu katika hii biashara
Hapa kwenye kuchora trend lines nahisi sina uwezo wa kujifundisha mwenyewe, na nahisi kuna maujanja ambayo yapo ambayo mtu huwezi kuyaelewa wewe kama wewe mwenyewe ukiwa newbie. Na naona kabisa inahitajika uwe na experience ili uweze kuelewa hii sekta ya kuchora trend lines
So kama kuna clue yoyote ambayo inampa mtu basic knowledge katika kuchora trend lines, where to start, what to look at, where to stop, what to do, when to look what n.k just give us some guidance.
Kwa maana kwa jinsi nilivyoobserve hili game, mnaweza kupewa same chart muifanyie analysis, ila mwisho wa siku kila mtu anaweza chora trend lines ambazo zikawa tofauti na mwenzake kwa jinsi anavyoona yeye. Na wote hao wanaweza kuwa wamechora sahihi.
Your guidance please katika hili.
CC : Bavaria, Ontario and other gurus.