Hellow guys!!
Leo nimeona nishee nanyi chochote kuhusu hawa watu/makampuni yanayoitwa Brokers!
Kiuhalisia wote tunaojifunza humu au hata wale ambao tayari ni wazoefu wa forex... by any chance lazima utakutana/ utafanya biashara na hawa watu wanaoitwa "brokers"! Kikawaida sisi kama indiviadual traders LAZIMA uwatumie brokers ili uwezo wa kujumuika katika hili soko la forex!!
Sasa kama kawaida, hawa brokers wako wengi, pia wako na sifa tofauti tofauti! Kawaida hawa brokers wamegawanyika katika makundi makuu mawili!! la kwanza wanajulikana kama dealing desk brokers au kwajina lingine wanajulikana kama marker makers! Kundi la pili wanajulikana kama no dealing desk brokers ambao nao wamegawanyika katika sehemu kuu mbili, yaani Electronic Communication Network (ECN) na Straight Through Processing (STP) .
Kundi la kwanza market makers/ dealing desk brokers!
Hawa wao ndio wanaoleta kwako orders, yaani wao ndio wanapanga bei ya kuuza na kununua! kwa kifupi wao ndio wana control bei! Pia lazima ujue, in some cases...kufanikiwa kwako ni hasara kwao na kutofanikiwa kwako mara nyingi ndio faida yao!! yaani wana operate kinyume na wewe. unless unawajua vizuri, I'd not advice you to trade with them as a retail trader!!
Kundi la pili ... No dealing desk brokers!
Tofauti na wale wa kwanza, No dealing desk brokers wao mara nyingi hawana direct control na orders hasa kwenye bei, wao wapo kwa ajili ya kukuunganisha wewe na other parties(say, market)!
Kama tulivyoona hapo juu, non dealing desk brokers wanaweza gawanyika katika sehemu mbili yaani ... Electronic Communication Network (ECN) na Straight Through Processing (STP) .
Straight Through Processing (STP)
Hawa kazi yao ni kuchukua order yako na kuipeleka kwenye soko, yaani wanakuunganisha na soko! mara nyingi STP brokers wanakua na wanunuaji au wauzaji wengi, so wewe ukiweka order yako ya kuuza au kununua then wanakuunganisha na wanunuaji/wauzaji sokoni!
Sasa kuna kitu lazima ujue, market makers wao wanapanga bei na wao wanaamua jinsi gani ya kupata faida. sasa kwa STP brokers kupata kwao faida wanachukua order yako, mfano unataka nunua EURUSD kwa 1.1230, sasa wao wataangalia katika list yao ni waauzaji wangapi wanauza EURUSD kwa 1.1230? wakiwapata wataangalia nani ana dau kubwa mfano akipatikana anayeweza kutoa 1.1240 basi huyo ndiye atapewa! so wewe utapewa 1.1230 yako na wao watachukua cha juu!!! ni kama madalali flani hivi...
ECN brokers
Hawa wanafanya kazi kinyume na STP brokers japo wote wako kwenye kundi moja yaani No dealing brokers! STP wao wanakua na list ya participants sokoni, then wanachukua order yako na kuilink na participant mwenye dau kubwa na kwa hii njia ndio wanapata faida/cha juu...
Ila kwa ECN brokers wao wanakupa direct link ya soko, kwa kifupi wanakuachia uwanja ili udeal na soko. Mara nyingi wanapata faida kupitia spreads na commisions tofauti na STP brokers ambao wanapata faida kupitia cha juu!!!
So far, no dealing brokers ndio wazuri hasa kwa retail traders kama mimi na wewe!! swali la kujiuliza kwa nini market makers (achilia mbali tabiayao) kwanini hadi leo wana survive?? may be because of higher risk higher reward (Aint sure!!)!
Wewe kama trader, kabla hujajiunga na broker yeyote ni lazima ujue aina ya broker, pia ni vyema ukajihakikishia kama wako regulated au la!! Forex ina risks nyingi, hatua ya kwanza kupambana na hizo risks ni kuanza vizuri kwa kuchagua broker anayekufaa!!
Wako katika kujifunza,
Lodrick Thomas (Eng.)