Leo kama ulibet against kusell euro kwa kutegemea itashuka bila kujua kuna news Fulani imekula kwako. Nilikuwa nacheza na practice account bila speculate kwamba USD itabanda against Euro kwa hiyo nikawa nauza Euro nanunua USD. Ebwanee kumbe kuna jamaa katoa speech leo , Euro imeshoot kwa kiwango ambacho hajashoot karibu miezi kumi...Yaani Mimi nilikuwa na practice kwa kucheki ceiling na floor. Hapo nimejifunza kitu kimoja kikubwa sana jinsi kuna news zina impact kubwa kwenye forex trading.
Euro sijaigusa kipindi,nilikuwa na deal na Aussie na Yen.
Kuna sehemu nimetaja hilo hapo awali, nikasema investment ya forex si ku bet au kamali, inatakiwa ufuatilie indicators na news.
Vitu kama.
Bei ya mafuta ikoje na wazalishaji wa mafuta ni nani na wanatumia hela gani?
Bei ya dhahabu ikoje na wazalishaji wa dhahabu ni nani na wanatumiahela gani? Benki kuu gani zina dhahabu sana?
Viongozi gani wakubwa wa Benki Kuu kubwa duniani, IMF, World Bank wana maongezi gani na maongezi hayo yataathiri vipi soko?
Wapi kuna political unrest na zitaathiri vipi soko?
Fedha gani huwa zinakwenda pamoja kwa sababu za kisoko? Mara nyingine fedha kama Australian Dollar na Chinese Yuan huwa zinaenda pamoja kutokana na chumi za mashariki ya mbali kufungamana sana.
Muda gani ni mzuri wa ku trade kwa kuangalia masoko ya New York, London, Singapore, Tokyo yanavyokuwa wazi na kuruhusu watu wengi zaidi wa trade.
Muda gani katika saa yoyote (dakika) ni mzuri zaidi kununua, mara nyingi kunakuwa na patterns za hourly rallies on the hour, unaweza kuzi note na kuzi avoid.
Dakika kama hii 59 ya saa unaweza kuona kitu kinapanda tu, kumbe ni hourly rally ambayo dakika chache baadaye inashuka tena.
Sasa hivi inavyoandikanaona Yen inapanda kwa hourly rally, ingawa Yen imeuawa sana leo.Ukijichuza kununua sasa, baaada ya dakika 15 inashukatena.
Mambo mengi sana ya kujifunza.