Wakuu,mimi nabukua bado sijaanza ku trade hata kwenye demo, nauliza kwenye hizi type za order kuna pending order na market execution,
Mkuu habari yako?!
Okey iko hivi, unaosemea "market excusion" unamaanisha kama ukiuza/ukinunua kitu basi utanunua kwa bei ambayo uko sokoni mda huo! Mfano kama bei ya EURUSD ni 1.4000 basi kwa market excusion utainunua kwa bei hiyo hiyo yaani 1.4000!!
Sasa tunaposemea "pending order" ni order ambayo inasubiri na bado haijatekelezwa. Kwa lugha rahisi ni kama umetega mtego, maana kwamba mtego utafanya kazi ukitegeuliwa!!
Mfano kama bei ya EURUSD ni 1.4000 na unataka ku-go long ikifikia bei Fulani mfano 1.4005, basi kwa kutumia pending order ndio unaweza uka-set ikifika 1.4005 ununue! kwa case kama hii utatumia "buy-stop order"!
hii pending order mbona naona kama haina risk?
Pending order ukiiset ni kweli inakua haina risk ila ikifikia bei uliyo-set ndio utaona risk yake!! ni kama unapotega bomu, hutaona madhara yake mpaka litapolipuka!!
kwa maana uki set inunue chini ya market price itakuwa haifanyi chochote hata price ikipanda juu ,
Uko sahihi, ni kweli haitafanya chochote mpaka bei uliyoset ifikiwe!
nikiwa nai set inunue kwenye range za chini za market kila siku si nitakua naondoka na pips bila kuingia risk (kitu ambacho haki make sense)???
Uko sahihi, lakini utakua "unaondoka na zero pips"! hii order inafanya kazi only if target/price ikiwa imefikiwa. Ikiwa na maana kama umeset bei za chini na kama hizo bei hazijafikiwa ni kwamba hazita be excuted, which mean zero risk and zero pips as well!
Niongezee tu huwezi kuweka pending order bila kuwa na uhakika au bila kufanya analysis ukawa na uhakiaka kiasi Fulani kwamba hii graph itatrend mpaka price level Fulani. Ni vyema ukafanya analysis ya soko kujua unaelekea wapi then uweke pending order!!
hapa kuna risk gani au disadvanytage gani ukilinganisha na market execution?
Kwa mtazamo wangu pending order haina risk na inakua na risk mpaka pale itapokua excuted! Pia oending order ni kama defensive mechanism flani kwamba ikifikia level Fulani nunua isipofikiwa maana ni kwamba haitanunuliwa, hapa unakua umejilinda!
Tofauti na market excusion ambayo ukiingia umeingia haina mjadala wala kujilinda na kama mambo yakienda hovyo basi cha kukuokoa ni stop loss kama uliiset na kama hukuiset ndio basi tena either ukubali hasara au uishie kutia kibiriti akaunti!!
Pending order mara nyingi inatumika kama uko sure kwamba price Fulani lazima itafikiwa na kama ikifikiwa tu basi order inakua excuted!!, au kama hauko-sure na direction ya graph basi kama soko likienda tofauti unakua umepona tofauti na market excusion ambayo soko likienda hovyo ndio basi tena huna jinsi Zaidi ya kukubali loss!!
Sijui kama umenielewa ila naomba ukasome hivi vitakusaidia kuielewa Zaidi pending order...
Ukiweza kasome hizi terminologies kwanza...
1. Pending order
2. Buy limit
3. Sell limit
4. Buy stop
5. Sell stop
6. Stop loss
Books that I recommend: Terminologies zote ziko chapter ya mwanzo kabisa!!
1. The bible of forex
2. Astrofx
3. Forex trading for dummies
Unaweza angalia youtube pia, utapata video walizoelezea vizuri Zaidi!!
Karibu sana mkuu!!