Mimi binafsi naamini uko vzuri, na ni kweli kwamb nlitamani kama ungekuwa personal mentor wangu.
Lakini kwa kauli hz za vijembe kwa WAZAZI na serikali, sitaki kuamini kuwa una uwezo wa kumuelimisha mtu akaelewa.
Danpol aliulizwa kuhusu ishu hz akasema yameisha, lakn wewe unarudi na kauli zilezile....
Just imagine kama tabia yako angekuwa nayo ontario, kila akirudi kwa uzi wake kutupa maneno ya kejeli na matusi tunaouliza maswali ya kijinga kama RSI...
unadhani ni wangapi wangevumilia? Unadhani wangapi wangebaki? Binafsi, ningeacha...
Wewe unaweza, muelimishe asiyeweza ili kesho asikuulize tena bro!
Kwanini mahali ambapo wengine twadhani tutapata mafanikio nyie mwatumia mianya hyo kututukania wazazi wetu? Huu ndo ustaarabu kweli?
Al watan, kama wewe tayari unaweza mambo haya, tuache wajinga wajinga tujikongoje wenyewe...
Ni bora niwe na kampani ya wajinga wanaoniheshimu, kuliko genious anayenidharau na kunitusi.
Sio poa, bro! Unatukatisha tamaa...
Kama Ontario angekuwa wewe, haki wengi tungekuwa tuko tu gizani...
Ukitaka kuntusi, ni sawa kwa upande wangu.
Sent using
Jamii Forums mobile app