Wewe ni mpambanaji, kidume hasa.
Achana na biashara ya kilimo wala kufuga kuku.
Hizo biashara mwanzo zinachoma mtaji sababu ya kukosa uzoefu, ukikosea kitu kidogo kuku wamekufa au mazao yamekufa au yatatoa mavuno kidogo.
Hizo biashara zinatakiwa uanze kujifunzia na pesa nyingine sio ya mawzo kama yako.
Mimi nakushauri katafute goli/fremu zuri miataa mizuri iliyo na watu wengi wanao pitapita, au jirani na majengo kama kanisa la KKT au Katoliki anzisha Toy Shop na bidhaa za watoto zingine.
Weka na bicycle za watoto used, pikipiki za plastic used n.k.
Weka toy mpya na used.
AU
Tafuta frame ya kuweka Hardware lakini yako iwe ya kipekee, nenda kanunue vifaa kama wavu za madirishani, bati, nondo, n.k. viwe reject toka kiwandani kwa bei rahisi sana na wewe uuze bei rahisi sana, uweke bango kabisa ni linalosema vitu husika ni reject. Fedha ngumu na wabongo wanapenda vitu rahisi.
Hizo bati au wavu reject ni mpya na nzuri kama sio mtaalamu au fundi haujui kama ni reject. u
Unakuta labda rangi imepauka kidogo au kuna sehemu ndogo imejikunja au migongo ya bati haiko sawa kidogo, au wavu/bati zimekatwa vipimo pungufu kidogo kama sentimeta chache n.k.
NB: Hiyo Toy Shop na used fanya mix na viatu na nguo kali vyote vya mitumba vya watoto utatoboa mwanangu.
Kaweke duka maeneo mojawapo ya haya Tabata, Ubungo Riverside au Mabibo, Sinza, Mbezi Luis, Mezi Beach, Afrikana, Kawe, Mikocheni, Kinondoni, Temboni, Kwa Musuguri, Kunduchi, Goba, Salasala Gongo la Mboto, Makumbusho, Mwenge, Tegeta n.k.
Au katafute sehemu jirani na stendi za BRT kama Gerezani ndani ya BRT, Kimara, Morocco.
Kama upo temeke basi katafute fremu jirani na stendi za daladala.