Forex imenifilisi, naomba ushauri wa biashara ya kufanya kwa mtaji huu

Jamaa hawa mbona wamebadilisha title ya huu uzi naomba mods mrudishe jinsi title ilivyokuwa hapo mmechange title haiendani na mada nisaidieni kuwa tag hawa jamaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Inawezekana kwa kiasi chochote kile .. Mimi nimewahi kutoa dola 50 mpaka 500 kwa miezi miwili.....



Mimi nilitaka kukujenga kisaikolojia tu ili usikumbwe na tamaa za Faida TU ... Inakuwa Kama wale eti ukilima tikiti heka moja unapata milion 20 na mtu anaenda beba mkopo ... Matokeo yake Ni bonge la hasara .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ndo hapo sasa thus why umeambiwa trade kile ulichotayari ku loose hiyo ni kamali kama betting ni biashara ya kubashiri japo yenyewe una base kwa tips fulani
 
Miezi miwili mingi sana. Basi mimi najitahidiii sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ya pc inapatikana kwa broker... ila ya simu ipo play store inaitwa meta trader 4

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusoma kuna mwisho ila experience ya market inaweza kuwa inabadilika siku hadi siku. Kuna vitu vipya utakutana navyo tu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Forex mkuu ni biashara ambayo inalipa sana yani mzunguko wake wa pesa ni mkubwa sana.
Kunakipindi nilikuwa napiga faida mpaka nikawa nawasiwasi labda forex inaweza kuisha kesho hizi dola 20, 30,40 mpaka 100 ilikuwa nikugusa tu.

Lakini jinsi pesa inavyozidi unaona 20 ni ndogo unaanza kufukuzia 200 hapo ndio tatizo mfano unaweza kutrade j3 hadi alhamis ukawa umetengeneza dola 200 lakini ijumaa ukaleta tamaa ukapigwa hata dola 300 unamaliza wiki na hasara 100

Hiko kitu kimenitokea sana na sio mimi tu najua na matrader wengi wamepitia ishu kama hii.

Kikubwa ni emotional intelligence ukiweza hapo kidogo utamaintain

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni mpambanaji, kidume hasa.
Achana na biashara ya kilimo wala kufuga kuku.
Hizo biashara mwanzo zinachoma mtaji sababu ya kukosa uzoefu, ukikosea kitu kidogo kuku wamekufa au mazao yamekufa au yatatoa mavuno kidogo.

Hizo biashara zinatakiwa uanze kujifunzia na pesa nyingine sio ya mawazo kama yako.
Mimi nakushauri katafute goli/fremu zuri miataa mizuri iliyo na watu wengi wanao pitapita, au jirani na majengo kama kanisa la KKT au Katoliki anzisha Toy Shop na bidhaa za watoto zingine.
Weka na bicycle za watoto used, pikipiki za plastic used n.k.
Weka toy mpya na used.

AU
Tafuta frame ya kuweka Hardware lakini yako iwe ya kipekee, nenda kanunue vifaa kama wavu za madirishani, bati, nondo, n.k. viwe reject toka kiwandani kwa bei rahisi sana na wewe uuze bei rahisi sana, uweke bango kabisa ni linalosema vitu husika ni reject. Fedha ngumu na wabongo wanapenda vitu rahisi.
Hizo bati au wavu reject ni mpya na nzuri kama sio mtaalamu au fundi haujui kama ni reject. u
Unakuta labda rangi imepauka kidogo au kuna sehemu ndogo imejikunja au migongo ya bati haiko sawa kidogo, au wavu/bati zimekatwa vipimo pungufu kidogo kama sentimeta chache n.k.
Weka vitu vya umeme na vingine vya hardware vya kawaida vipya sio reject.

NB: Hiyo Toy Shop na used fanya mix na viatu na nguo kali vyote vya mitumba vya watoto utatoboa mwanangu.
Kaweke duka maeneo mojawapo ya haya Tabata, Ubungo Riverside au Mabibo, Sinza, Mbezi Luis, Mezi Beach, Afrikana, Kawe, Mikocheni, Kinondoni, Temboni, Kwa Musuguri, Kunduchi, Goba, Salasala Gongo la Mboto, Makumbusho, Mwenge, Tegeta n.k.
Au katafute sehemu jirani na stendi za BRT kama Gerezani ndani ya BRT, Kimara, Morocco.
Kama upo temeke basi katafute fremu jirani na stendi za daladala.
 
Asee mkuu barikiwa sana ushauri mzuri sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asee mkuu barikiwa sana ushauri mzuri sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Thanks mkuu.

kitu cha kukumbuka usikurupeke kukodi fremu sehemu bila kuichunguza sana, sana, sana kuhusu aina ya watu unaotaka wawe wateja wako.

Madalali ni sumu kubwa hata awe rafiki yako, yeye anataka upange apate pesa anaweza kukuchomesha maindi kizembe zembe.
Mitaa usiyo ijua kuwa makini kutembelea kwa kificho mara kadhaa masaa na siku tofauti kuangalia mzunguko wa watu.
Najua ukiona fremu sehemu madalali wanakutia presha fanya haraka hapa fremu hazikai utaikosa.
Jifunze kupitia kisa chako cha Sokoni Ilala.
 
Sijaona sehemu ambapo FX imekufulisi .

Nilichoona kuwa imekupa starting point ya kuishi

Wewe NI mzee wa kujilipua au gambler

Badili heading unakosea Taaluma za watu heshima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa gia hio unayokuja nayo lazima upigwe wahuni washaona fursa kwako[emoji1787]

Boss Tafuta vitabu kwanza

Nenda pdfdrive.com katafute hivi vitabu

[emoji336]Currency trading for dummies

[emoji336]The ultimate price action

[emoji336]Trendline secret revealed

[emoji336]The candlestick Bible

Uvisome uvielewe kisha ndio haya mawazo yako uendelee nayo

La sivyo thredi za malalamiko ya forex zitakuwa nyingi sana


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sawa mkuu shukran sana
Nitafanya hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…