sasa mkuu powell akisema tu good morning / afternoo tu muda wa news chart zinakimbia we hustuki mkuu?
au anyway nipe elimu kwenye hilo
forex huwa inatoa matokeo yakupanda na kushuka kutokana na habari husika huwa inasema nini, na watu huwa wana react palepale tu habari inapotoka utaona soko linafanya yake!.
Hii ni biashara ya live ndio maana unaona news zinakuwa namatokeo ya haraka hivyo.
ndio soko la forex muda mwengine hufanyiwa ukanjanja aidha na central banks wakiweza kuwasiliana wanaweza kufanya jambo walipeleke wapi soko!, hii ilishawahi kutokea na ilipokuja kubainika hatua zilichukuliwa, vilevile brokers wengine huwa wanamtindo wa kuchezea chat ili watengeneze faida ndio maana wengi wao wanashauliwa kabla hujaamua kumtumia broker fulani basi hakikisha sehemu alizosajiliwa n.k na ikithibitika wamechezea chart unaweza kuwashitaki.
Mi nafikiri swala hili la forex lina changamoto zake ambazo hata biashara nyengine zinachangamoto vilevile na ili uweze kufaulu kwenye biashara yoyote ile ni lazima uhakikishe unaweza kutatua walau asilimia 70 ya changamoto ktk biashara husika!.
kwani mkulima anaelima nyanya halafu anakuja kwenda sokoni anakutana bei kwa tenga ni tofauti na yenye hasara harudishi hata mtaji!, huyu anatofauti gani na mtu wa forex ambae amekula loss maana hawa wote wawili hawakulisoma soko vizuri.
tena huyohuyo mkulima anaweza kukutana na madalali sokoni na wakampiga!, nafikiri kila biashara inachangamoto zake na ukifaulu kuzitatua basi faida utaiona!.
kasome kisa cha George soros alivyoitetemesha serikali ya uingereza na wala hata hakushikwa!, na wala hata hakushikwa kwa maana halikuwa kosa lile yeye aliona upenyo akautumia!.