Fr Kitima: Unataka uridhiane na nani na hujakiri kosa?

Fr Kitima: Unataka uridhiane na nani na hujakiri kosa?

Ila huyu jamaa šŸ˜…šŸ˜…šŸ˜… leo anampokea kiongozi wa kiserikali ofisini kwake. In a week anakuja kupiga spana non stop
Hao ni wale watu kunguru. Hawafugiki
 
Kitima Kwanini haongelei pia uhalifu uliofanyika kwa kisingizio cha maandamano?
Shida ya nyie maCCM Iko hapa. Ni kuwa hamna utu wala ubinadamu...

Utaanzaje kuwaza mali kwanza kabla ya maisha ya maelfu ya watu masikini wasio na hatia waliouwawa ili mtu mmoja awe Rais wa Tanganyika...!!!?????

Miundombinu ikiharibika hutengenezwa upya na kurejeshwa ktk hali yake ya swali. Mali hutafutwa na kurejeshwa tena na ndio maana Kuna mpango unafanywa huko serikalini (tunajua) Ili waliopata hasara wafidiwe....!

āœ“ Vipi mamia kwa maelfu ya maisha ya watoto, vijana, kinamama na kinababa yaliyokatizwa kikatili bila hatia ili Samia awe Rais?
āœ“ Vipi vilio vya ndugu ambao mpaka sasa hawajakabidhiwa maiti za ndugu zao ili wawazike kwa heshima?

Sikiliza bibie.

Kila mtu anakubali kabisa kuwa, uharibifu wa mali nalo ni kosa. Lakini kuua au kumwaga damu ya mtu/watu wasio na hatia kinyume cha sheria ni kosa kubwa zaidi. Makosa yote mawili ni punishable according to the laws of the land. Makosa yote yanapaswa kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Kwanini hili linakwepwa na serikali yenu? Si kwa sbb nyie ndio wahalifu na wauaji wenyewe, au siyo?

Hata hivyo, jibu la hoja yako hii ni rahisi tu na limo kwenye jibu la maswali makuu mawili hayašŸ‘‡šŸ‘‡

1. kwanini watu waliuwawa kwa risasi za moto na Polisi wenyewe wakihusika? Na

2. Nani alitoa amri ya kuua watu na kwa nini?

#Kama aliyetoa amri ya SHOOT & KILL akisema aliua kwa sababu hao watu waliharibu miundombinu kama inavyosemwa, mali za umma na za watu binafsi, then hapo ndipo tutakapoanzia kuziangalia sheria zetu..
 
unawezaje kuthubutu kupima uhalifu na adhabu ya kifo, hiyo ni sheria ya wapi? Wacha kujitoa ubongo. Katafute nchi yako inayoua wananchi wake kwa sababu ya uhalifu wa kuharibu mali na miundo mbinu. Sio TZ, hii sio nchi ya kigaidi. Ufike wakati sasa wakiri makosa ili tu move on, wacheni utoto na kiburi.
Nyie wapumbavu leo mnatetea wahalifu wakati mkiwakamata sokoni wameiba nazi mnawaua kwa kudai mna hasira kali? Wanafiki wakubwa nyie.
 
Back
Top Bottom