TANZIA Fr. Privatus Karugendo amefariki dunia

Sawa Ila alianza shujaa wenu anajifanya hataki barakoa kabetri kakafreeze sijui kalimtandika shoti. Corona ipo ndio uvae barakoa jomba utakufa kama Mungu wenu.
Hebu jitazame hapa ulivyo 🤣🤣🤣

 
Amefia hospitali gani father, isije ikawa ni yeye aliendika jana hii post ya kutuaga.
 
Apumzike kwa Amani Fr. Peivatus Kalugendo.
Fikra na Msimamo wake kwenye mambo aliyoyaamini vitaishi vizazi na vizazi kwani alitumia vema kalamu kuhifadhi mawazo yake.
Pole kwa ndugu na familia.

Sent from my Nokia 3.1 using JamiiForums mobile app
 
75% yaweza kuwa kweli.
 
Kutoka kwa Askofu Kalikawe Lwakalinda Bagonza


BURIANI PACHA WANGU PRIVAT

NOOO. Nashindwa kuamini ninachosikia. Kwamba pacha wangu Privatus Karugendo hatunaye?! No. Hapana siamini hata kama inaaminika.

Juzi nimempoteza mdogo wangu. Haikutosha, nimpoteze pacha wangu?!

Tulifahamiana akiwa Padre kijana nikiwa Shemasi. Wakati huo tulikuwa Ujerumani, nikisoma, alifanya kazi za kitume. Watu wengi walisema tulifanana katika mengi.

Nilipobarikiwa kuwa Mchungaji alikuwepo kijijini kwetu kumzika babake Padre rafiki yake hayati Padre Buhorela.

Tuliyokubaliana yalivutia wengi kuliko tuliyotofautiana. Tulipenda kusoma vitabu, kuandika na kujadiliana. Alikuwa mfuasi wa Baba wa Taifa, Mimi nilikuwa mwanafunzi na sitahitimu.

Sikukubaliana naye aliponipigia. Alikuwa na uwezo wa kuona mazuri ndani ya kitu kibaya. Mimi ni mwepesi wa kuona udhaifu ndani ya kitu kinachoaminiwa na wengi kuwa kizuri.

Wote tuliuanika ujinga wetu kupitia Rai, Raia Mwema, Tanzania Daima, MwanaHalisi, Mwananchi na Mawio. Nilipostaafu hilo yeye aliendelea. Tuliulizana, "hivi ukianika ujinga wako ukaisha kichwani, Nini kinabakia kichwani?"

Pumzika rafiki, Pacha, Mtume wa jamii huria na mpenda watu wote pasipo ubaguzi. Ulijenga madaraja mengi kuliko kuta.
 
Mmh huyu sio yule aliyetuaga kwenye ile mada? Ana ID ya kike?
 

Apumzike kwa amani Fr. Karugendo.

Tangulia baba nasi tu nyuma yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…