LGE2024 Freeman Mbowe akamatwa na Jeshi la Polisi akielekea Mbozi mkoani Songwe

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mheshimiwa Freeman Mbowe amekamatwa na Jeshi la Polisi katika mapori ya HALUNGU akiwa njiani anaelekea Mbozi kwenye Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa baada ya kutoka Mlowo ambapo mkutano wale ulizuiwa na Jeshi la Polisi kwa Kutawanya Watu kwa mabomu ya machozi

Magari yameharibiwa kwa kuvunjwa Vioo,Watu waliokuwa katika msafara wa Mbowe wamepigwa vibaya mno,wamepoteza simu na fedha.

Polisi wamempakia Mheshimiwa Mbowe katika Defender na Kutoweka naye pasipo Julikana.

Viongozi wengine waandamizi wamekamatwa na Kupakiwa katika gari tofauti na ile iliyombeba Mheshimiwa Freeman Mbowe.

Pia soma
- LGE2024 - Polisi watawanya Mkutano wa Mbowe kwa Mabomu. Kosa kaingilia ratiba ya ACT-Wazalendo

======

UPDATES

=======

TAARIFA KWA UMMA

Jeshi la Polisi leo tarehe 22 Novemba,2024 katika Pori la Halungu lililopo Wilaya ya Mbozi wamevamia Msafara na kumkamata Mwenyekiti wa Chama Taifa Mheshimiwa Freeman Mbowe pamoja na Viongozi mbalimbali aliokuwa ameambatana nao .

Msafara wa Mwenyekiti wa Chama Taifa ulikuwa umeshafanya Mikutano ya kampeni katika Kata ya Itaka,Kijiji Cha Itewe na Kata ya Halungu Mjini.

Awali mkutano wa kwanza uliokuwa ufanyike katika mji wa Mlowo uliozuiliwa na Polisi pamoja na wenyeji wetu ambao ni Chama Cha ACT Wazalendo kutualika kushiriki kwenye mkutano wa pamoja ila Polisi walikataa na kutawanya wananchi Kwa mabomy ya machozi .

Kabla ya kuwakamata walifuatwa na gari ya Polisi ambayo ilikutana nao njiani na hivyo iligeuza na baada ya mwendo kidogo walikuwa njia imefungwa na gari za polisi ndipo walipofungua milango Kwa nguvu na kuanza kuwashambulia waliokuwa kwenye Magari hayo na kuwakamata Kwa nguvu.

Waliokamatwa ni :
1. Mhe.Freeman Mbowe
2. Mhe. Joseph Mbilinyi - Mwenyekiti Kanda ya Nyassa
3. Mhe. Pascal Haongo- Mbunge wa Mbozi mashariki Mstaafu
4. Mwenyekiti wa Chama Cha ACT Wazalendo Wilaya ya Mbozi
5. B Appolinary Boniface - Mkuu wa Digital platform
6. Paul Joseph - Afisa habari Kanda ya Nyassa
6. Calvin Ndabila - Afisa habari Kanda ya Nyassa
7. Mdude Nyagali - Mwanaharakati na mwanachama wetu
8. Wasaidizi wa Mwenyekiti wa Chama Taifa Bwire,Adamoo na Lingwenya

Jeshi la Polisi wameondoka na viongozi wetu na hajajasema wanawapeleka wapi na mpaka Sasa hatujui wanashikiliwa wapi na Kwa sababu gani.

Chadema Kwa hatua ya Sasa tunasema yafuatayo;

1. Tunalaani kitendo hiki kwani kinaonyesha wazi kuwa ni mkakati wa Polisi kuhujumu kampeni za chama chetu Kwa kushirikiana na CCM
2. Polisi wawaachie mara Moja na bila masharti yoyote ili waendelee na ratiba ya Mikutano ya Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
3. Wanachama na Viongozi wetu waendelee na kampeni za kuondoa CCM madarakani .
4. Tunaialika jumuiya ya kimataifa kuja kushuhudia uvunjifu wa Haki za kidemokrasia Kwa vyama vya upinzani nchini katika uchaguzi huu unaoendelea nchini .

Imetolewa Leo Ijumaa tarehe 22 Novemba, 2024

John Mrema - Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje
Mimi nilidhani CCM wameridhika na engua engua waliyo fanya kumbe Bado hawajatosheka.
 
amewaelekeza tu kwamba njooni mnikamate ili utengeneza story na kupoteza wabongolala maboya. hapo chadema wataishia kujadili kukamatwa kwake badala ya kuongelea mambo ya msingi. wengi tumesoma cuba alafu mnafikiri tunadanganyika kirahisi.
Siasa=Si-hasa=Si kweli
 
Magufuli alikuwa na mabaya yake ila huyu kazidi.
Anatumia nguvu kupita kiasi
Unaijua Nguvu Kupitia kiasi au ndio una shida zako?
.
Aliyemtandika Mbowe Hadi karibia kuvunja mguu na kudingia alilewa alikuwa Samia?

Aliyempa Mbowe kesi ya ugaifi alikuwa Samia?

Aliyewapiga marufuku kufanya siasa Nje ya majimbo Yao ni Samia?

Aliyewapira Mali zao eg bilicans , Kuharibu Mali zake Hai ni Samia?

Kimsingi hata Mbowe mwenyewe akikusikia atakuina mpumbavu na huna akili,
 
Hizo nguvu zingetumika pale Kariakoo, na imani watu wengi wangepatikana wakiwa hai.
 
Huyo mwenye nguo nyekundu aliyelambwa sio mdude kweli 😂
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mheshimiwa Freeman Mbowe amekamatwa na Jeshi la Polisi katika mapori ya HALUNGU akiwa njiani anaelekea Mbozi kwenye Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa baada ya kutoka Mlowo ambapo mkutano wale ulizuiwa na Jeshi la Polisi kwa Kutawanya Watu kwa mabomu ya machozi

Magari yameharibiwa kwa kuvunjwa Vioo,Watu waliokuwa katika msafara wa Mbowe wamepigwa vibaya mno,wamepoteza simu na fedha.

Polisi wamempakia Mheshimiwa Mbowe katika Defender na Kutoweka naye pasipo Julikana.

Viongozi wengine waandamizi wamekamatwa na Kupakiwa katika gari tofauti na ile iliyombeba Mheshimiwa Freeman Mbowe.

Pia soma
- LGE2024 - Polisi watawanya Mkutano wa Mbowe kwa Mabomu. Kosa kaingilia ratiba ya ACT-Wazalendo

======

UPDATES

=======

TAARIFA KWA UMMA

Jeshi la Polisi leo tarehe 22 Novemba,2024 katika Pori la Halungu lililopo Wilaya ya Mbozi wamevamia Msafara na kumkamata Mwenyekiti wa Chama Taifa Mheshimiwa Freeman Mbowe pamoja na Viongozi mbalimbali aliokuwa ameambatana nao .

Msafara wa Mwenyekiti wa Chama Taifa ulikuwa umeshafanya Mikutano ya kampeni katika Kata ya Itaka,Kijiji Cha Itewe na Kata ya Halungu Mjini.

Awali mkutano wa kwanza uliokuwa ufanyike katika mji wa Mlowo uliozuiliwa na Polisi pamoja na wenyeji wetu ambao ni Chama Cha ACT Wazalendo kutualika kushiriki kwenye mkutano wa pamoja ila Polisi walikataa na kutawanya wananchi Kwa mabomy ya machozi .

Kabla ya kuwakamata walifuatwa na gari ya Polisi ambayo ilikutana nao njiani na hivyo iligeuza na baada ya mwendo kidogo walikuwa njia imefungwa na gari za polisi ndipo walipofungua milango Kwa nguvu na kuanza kuwashambulia waliokuwa kwenye Magari hayo na kuwakamata Kwa nguvu.

Waliokamatwa ni :
1. Mhe.Freeman Mbowe
2. Mhe. Joseph Mbilinyi - Mwenyekiti Kanda ya Nyassa
3. Mhe. Pascal Haongo- Mbunge wa Mbozi mashariki Mstaafu
4. Mwenyekiti wa Chama Cha ACT Wazalendo Wilaya ya Mbozi
5. B Appolinary Boniface - Mkuu wa Digital platform
6. Paul Joseph - Afisa habari Kanda ya Nyassa
6. Calvin Ndabila - Afisa habari Kanda ya Nyassa
7. Mdude Nyagali - Mwanaharakati na mwanachama wetu
8. Wasaidizi wa Mwenyekiti wa Chama Taifa Bwire,Adamoo na Lingwenya

Jeshi la Polisi wameondoka na viongozi wetu na hajajasema wanawapeleka wapi na mpaka Sasa hatujui wanashikiliwa wapi na Kwa sababu gani.

Chadema Kwa hatua ya Sasa tunasema yafuatayo;

1. Tunalaani kitendo hiki kwani kinaonyesha wazi kuwa ni mkakati wa Polisi kuhujumu kampeni za chama chetu Kwa kushirikiana na CCM
2. Polisi wawaachie mara Moja na bila masharti yoyote ili waendelee na ratiba ya Mikutano ya Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa
3. Wanachama na Viongozi wetu waendelee na kampeni za kuondoa CCM madarakani .
4. Tunaialika jumuiya ya kimataifa kuja kushuhudia uvunjifu wa Haki za kidemokrasia Kwa vyama vya upinzani nchini katika uchaguzi huu unaoendelea nchini .

Imetolewa Leo Ijumaa tarehe 22 Novemba, 2024

John Mrema - Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje
 
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mheshimiwa Freeman Mbowe amekamatwa na Jeshi la Polisi katika mapori ya HALUNGU akiwa njiani anaelekea Mbozi kwenye Kampeni za Uchaguzi ...
Hakuna lingine zaidi ya njama ya kuwakwamisha kwenye kampeni yao na siku zenyewe za kampeni ni chache. Kwa uonevu huo wananchi watawapigia kura za huruma wanaoonewa.
 
Hawa CCM wanataka kuwakatisha tamaa wanachama wa upinzani ili wasusie kupiga kura, jambo ambalo litawapa mwanya wa kuchakachua.

Wapinzani mmeshavulia maji nguo, hakuna kurudi nyuma.
 
Usipotii Sheria utapigwa tu na kama amekaidi hao mapolisi wahakikishe anatumia magongo maisha yake yaliyobaki tunahitaji siasa safi za kistaarabu
Hembu tusanue kilichokosewa.
 
Kama Dk Kizza Besigye yuko mahabusu huko kwa makosa mbalimbali ya jinai, Mbowe nani asikamatwe, nchi hii lazima usalama upewe kipaumbele, halafu tukiandika ya kweli Jamiiforums wanayapuuza wanaweka yale ya kugombanisha Serikali, hata hii wataifuta pia
 
Wewe ni mpumbavu! Mbona tulivyokuwa tunamlinganisha Magufuli na BOKASA ulikuwa unashupaza kiuno?
 
Back
Top Bottom