BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ametoa msimamo wa chama chake, akisema kikifanikiwa kushika dola, lugha itakayotumika ni Kiingereza ili kuondoa alichokiita ubaguzi wa kiajira unaotokana na vijana wengi wa Kitanzania kutoijua lugha hiyo.
Akiwa wilayani Hai mkoani Kilimanjaro siku chache baada ya kutoka gerezani alipokuwa mahabusu, Mbowe alisema elimu ya Tanzania imejaa ubaguzi wa makundi kati ya wenye uwezo na masikini, huku akieleza kuwa ubaguzi huo unajidhihirisha hata katika ajira hususan kwenye taasisi na kampuni kubwa.
Akihutubia mamia ya wafuasi wake na wananchi waliojitokeza kumpokea katika viwanja vya Bomang’ombe, Mbowe alisema elimu inayotolewa kwa sasa haimjengi Mtanzania kuingia katika soko la ajira kutokana na mfumo wake ulivyo na kwamba inahitaji mabadiliko.
“Kumekuwa na ubaguzi katika elimu kwani viongozi wetu wamekuwa wakituhutubia tujifunze Kiswahili ni lugha yetu ya Taifa, lakini leo Kiswahili hicho kinazungumzwa kwenye shule zetu za kata, viongozi wote na watu wenye uwezo wanasomesha watoto katika shule za mfumo wa Kiingereza; huu ni ubaguzi,” alisema.
Kiongozi huyo anasema Chadema kikiingia madarakani, kitahakikisha watoto wote wanafundishwa kwa lugha ya Kiingereza, kwa kuwa ndiyo lugha ya kimataifa.
Anasema katika dunia inayokwenda kwa kasi huku ikichagizwa na mabadiliko ya teknolojia, maarifa ya lugha ya Kiingereza ni ya lazima na kwamba Kiswahili kitabaki kuwa kama somo la ziada.
Anatoa mfano wa namna Wakenya wanavyotamba katika soko la ajira, kwa sababu ya uwezo walionao katika kutumia Kiingereza.
‘’Vijana wa Kenya wamelikamata soko kubwa hata katika nchi zenye uchumi mzuri ndani ya Afrika tofauti na Watanzania, ambao licha ya kuwa na uwezo, wanakwamishwa na suala la lugha,’’ anaeleza.
Ilivyo sasa nchini, wanafunzi wa shule za awali hadi darasa la saba, wanafundishwa kwa lugha ya Kiswahili, huku Kingereza kikiwa kama somo.
Pia kuna shule za mchepuo wa Kingereza katika ngazi hiyo ya elimu, hata hivyo, nyingi zinamilikiwa na watu au taasisi binafsi. Wanafunzi hao wote wanapomaliza darasa la saba, wanalazimika kutumia Kiingereza kama lugha ya kufundishia.