Pre GE2025 Freeman Mbowe amesema sasa anaenda kutafuta Mafekeche akiwaaga Wajumbe Ukumbini, "ninyi jengeni Siasa"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Akihitimisha salamu zake za pongezi kwa ushindi wa Tundu Lissu, Mwenyekiti mpya wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe amesema sasa anaenda kupiga mzigo ili kutafuta mafekeche (fedha) na wataonana baadae.

Pia, Soma: Mbowe: Nikishindwa uchaguzi narudi kwenye biashara zangu

"Ngojeni nikapige mzigo, nitafute wanaita Mafekeche, nikatafute fedha kwasababu tukifanya biashara sawa sawa tunatengeneza uchumi, ninyi jengeni Siasa, tutaendelea kusaidiana, tutaendelea kushauriana, wote lengo letu la kuijenga demokrasia katika nchi hii haliwezi kufifishwa na uchaguzi"
Your browser is not able to display this video.
 
Hongera sana Mbowe na Lissu!
 
Sisiem or act wazalendo anaenda
 
Kwani ni lini aliacha kutafuta mafekeche? Kosa alilotaka kuendelea nalo ni kuyatumia hayo mafekeche kunyanyasa viongozi wenzake!
 
Unajua kwa kukomaa mpaka kwenye sanduku la kura kumeisaidiaje chadema kujitangaza
 
Kila la heri Tundu Lissu. Sasa utulize kichwa utafute hela, uendeshe chama. Ndio unaachiwa mzigo hivyo.

Na Mbowe alifanya vizuri sana kununua kabisa jengo la ofisi ya chama. Hawa wangekuta hela kwenye akaunti wangesumbua sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…