Pre GE2025 Freeman Mbowe amesema sasa anaenda kutafuta Mafekeche akiwaaga Wajumbe Ukumbini, "ninyi jengeni Siasa"

Pre GE2025 Freeman Mbowe amesema sasa anaenda kutafuta Mafekeche akiwaaga Wajumbe Ukumbini, "ninyi jengeni Siasa"

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hekima anayo ILA sio sana kama unavyosema. Angekuwa na hekima sana asingepambania kushinda hadi mwisho, pressure ya wapenda mageuzi ilikuwa kubwa sana kuweza kusoma alama za nyakati, asingetuhusu mtifuano na majeraha ya uchaguzi, angejitoa hata siku ya uchaguzi.

Vv
Demokrasia haijengwi hivyo. Mbona hamtaki kuiachia ccm miaka yote mnagombea na hamshindi.

Demokrasia lazima iamue, huo ndio ustaarabu wake. Kuachiana na kujitoa ni udhaifu labda kwenye mifumo ya kifalme.
 
FAM hakujua anachokifanya.
Angelitambua mapema, angejua kuwa kupambana na wakati kutamharibia kuliko kumjenga.
Pale alipo hata akigombea ubunge kutoboa ni ngumu.
Huu uchaguzi umemchafua na kufanya asinadike.
Ni fikra zako tu hizo
 
Sasa ndio wakati wa kujichanga maana tulimsema sana kuhusu yeye kusaidia chama kiuchumi.

Tunadhangilia matokeo ya uchaguzi lakini ni kwamba pesa yote ametoa yeye binafsi hata hao waliokuwa wamamtukana hawakudiriki kutoa hata shilingi mia.

Mwiba ukishakuchoma ndio unajua maumivu yake. Lissu sasa ajiandae kusaka hela za kuendesha programu za chama maana kama kutengeneza gari tu imebidi achangiwe hadi milioni 30 na Nchimbi wa CCM basi akae akijua uongozi sio harakati uongozi ni mipango madhubuti
 
Mbowe afanye bihashara awe mfadhili wa Chama kama Sabodo. Hii itampa heshima sana zaidi ya uwenyekiti.
 
Bado ni fedheha kwa kukatiliwa kwenye box la kura, angengatuka bila haya angebaki kukumbukwa zaidi.
Kama kushindwa uchaguzi ni fedheha, basi kitu peke cha kuepusha fedheha ni kufanya uteuzi, maana angeshinda Mbowe, bado ungeona Lissu amepata fedheha. Tuwapongeze basi CCM Kwa kukwepesha na kuamua kupeleka kina moja
 
Back
Top Bottom