SI KWELI Freeman Mbowe asitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike Septemba 23

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ametangaza kuahirisha maandamano yaliyopangwa kuanza tarehe 23/9/2024 mbele ya waandishi wa habari katika mkutano wa TDC ili kupisha mazungumzo yatakayofanyika baina ya viongozi wa dini na Rais Samia.
Nadhani jf wamekanusha hii habari muda sio mrefu
 
Tokea miaka ile ya vurugu za wale wa dini miaka ile, lile kasheshe la jwtz, siji kusogea kwenye maandamano.

Mnitukane, mniite majina yote magumu, ila nyie andamaneni, mie sipo.
 
Ilikua ni suala la muda tu tangazo la sitisho la maandamano yaliyopigwa marufuku na polisi nchini kutolewa, hasa baada ya hotuba nzito na bora zaidi ya Rais Dr. Samia Suluhu Hassan kwa Taifa, na jumuiya ya kimataifa,

Ni dhahiri hotuba ya Rais iliwanyongonyeza mno, hapangekuepo taasisi, chama cha siasa au mtu binafsi wa kuthubutu kukaidi, maelezo, onyo la rais, ushauri na mawaidha ya Rais, ambae pia ndie Amer Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania.

Kwa kiapo, Rais aliapa kulinda katiba na kulinda amani na utulivu wa waTanzania dhidi ya yeyote yule, ambae kwa namna moja ama nyingine anapanga au anajaribu kuhatarisha, kuharibu au kuvuruga umoja, amani na utulivu, eti kwa kuandamana kwa kwa amani, huku lengo la maandamano hayo likiwa ni kuvuruga Demokrasia ya Tanzania kwa mihemko tu.

Eti Samia Must Go, halafu eti ndio maandamano ya amani. Hiyo isingetokea.

Hata hivyo kusalimu amri ya Rais, kwa chama cha demokrasia na maendeleo chadema, ni miongoni mwa maamuzi magumu muhimu na ya kiungwana sana kisiasa, kwa mustakabali na uhai wa Chadema yenyewe.

Ni muhimu sana kwamba, pakitokea tatizo au changamoto ya kisiasa,kijamii au kiuchumi, ni muhimu kuketi chini kwa makini, kutafakari na kutafuta majawabu muafaka ya kutatua changamoto hiyo na sio kuanzisha tatizo lingine.

Kuna ombwe la uongozi wa juu kitaifa chadema. Ingekua sio sahihi kisiasa, kwa mtu kuamini eti maandamano hayo haramu yangefanyika chini ya yuongozi uliopo wa Chadema πŸ’

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Kuna ombwe la uongozi wa juu kitaifa chadema. Ingekua sio sahihi kisiasa, kwa mtu kuamini eti maandamano hayo haramu yangefanyika chini ya yuongozi uliopo wa Chadema
Kwa hiyo uongozi wa CHADEMA ungekuwa bora, maandamano haramu yangefanyika, au sio?
 
Heading v/s content.

JamiiCheck
 
Ma keyboard warriors waandamane wapi hao, hayo yanajua tu kupiga kelele mitandaoni tu ila kuingia field maoga balaa
 
Watu walishajipanga kusubiri kibaka yeyote apite mstari tuione mikia yao!
 
Mimi raia mwema na mzalendo, nimewaomba police waniazime tu RUNGU, niisaidie police katika kuwakanda migongo yenu kwa marungu, pale mtakapoandamana.πŸ˜‚πŸ˜‚
Sema kuwa wewe ni shetani aliyefuzu unayefurahia kumwaga damu za watu. Raia wema wote watafanya chochote, yakiwemo maandamano, kutetea uhai wa Watanzania.

Waandamanaji na Mungu.

Ninyi watekaji na wauaji na shetani wenu.
 
Naona umekuja kupima kama yapo au hayapo.
 
Wezi mnaishi kwa hofu Sana.
alieogopa ni nani sasa, chairman Mbowe alie itisha maandamano haramu na yeye mwenyewe kuyasitisha au uongozi mzima wa Chadema?πŸ’

ndio maana nasema chadema kuna ombwe la uongozi gentleman πŸ’
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…