SI KWELI Freeman Mbowe asitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike Septemba 23

SI KWELI Freeman Mbowe asitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike Septemba 23

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Mbowe maandamano.png

Nimeona video ikizunguka kwenye mitandao ya Kijamii ikonesha kuwa jioni ya leo, mwenyekiti wa CHADEMA amesitisha maandamano yaliyokuwa yafanyike Septemba 23

Tunachokijua
Freeman Mbowe ni ni mwanasiasa maarufu nchini Tanzania. Yeye ni kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ambacho ni chama kikuu cha upinzani nchini.

Baada ya taarifa ya kifo cha aliyekuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya CHADEMA Taifa na Msaidizi wa Katibu Mkuu Ally Mohamed Kibao kilichotokea Septemba 8, 2024, chama cha CHADEMA kiliweka azma ya kufanya maandamano Septemba 23, 2024 kupinga utekaji na mauaji yanayoendelea nchini (Soma Hapa). Baada ya azma hiyo tukio siku ya September 13, 2024 Jeshi la Polisi lilifanya Mkutano na Waandishi wa Habari kukikataza chama hicho kufanya maandamano hayo (Soma hapa).

Kama alivyodokeza mdau mleta mada hii leo kupitia mtandao wa X (Twitter) katika akaunti hii na hii kumechapishwa taarifa iliyoambatana na video ikimuoonesha Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe akitangaza uamuzi wa chama hicho kusitisha mpango wa Maandamano ili kutoa nafasi ya Viongozi wa dini kutafuta suluhu. Katika video hiyo yenye sekunde 33 Freeman Mbowe anaonekana akisema:

Tunaomba na kuwatangazia Viongozi wa ngazi zote za CHADEMA pamoja na Wanachama, Wabunge wakiwemo, Madiwani, Wafuasi na Mashabiki wetu Watanzania wote popote pale walipo, kwamba tunaahirisha mikutano na maandamano ya amani yaliyopanga kufanyika nchi nzima ili kutoa nafasi kwa viongozi wetu wa kiroho kutafuta suluhu ya jambo hili kwa kukutana na rais na serikali yake
Upi ukweli wa Video hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao wa JamiiCheck kupitia mtandao wa YouTube kwa kutumia maneno CHADEMA yasitisha Maandamano tumepata majibu kuwa video hii si ya mwaka huu wala haihusiani na mpango wa Maandamano ya CHADEMA ya mwaka huu. Video hii ilichapishwa kwenye mtandao huo mara ya kwanza Agosti 31, mwaka 2016 (tazama hapa na hapa) huku ikieleza uamuzi wa CHADEMA kusitisha kwa mwezi mmoja maandamano ya UKUTA waliyoyapanga kuyafanya Septemba 1, 2016.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ametangaza kuahirisha maandamano yaliyopangwa kuanza tarehe 23/9/2024 mbele ya waandishi wa habari katika mkutano wa TDC ili kupisha mazungumzo yatakayofanyika baina ya viongozi wa dini na Rais Samia.
Yaleyale ya UKUTA, waliahirisha ili viongozi wa Dini wakaongee na Magu.
Hao viongozi w dini na wenyewe ni sehemu ya makundi ya kijamii wana ya kwao. Hawapaswi kuangaliwa au kuchukuliwa kama mediators kati ya makundi mengine na serikali.
 
Nasema kila siku kizazi cha kuhitaji mabadiliko bado sanaaa lazima kizazi chetu cha Uwoga na Unafiki kitoweke Duniani kabisa.
Sahihi kabisa, yaani waliona 10yrs+ wote wafe leo hii, hawa walio chini wakikua huenda kukawa na jambo la kueleweka. Nchi hii shida sana.
 
kuna wakati unaweza kuwasikiliza hawa wanachadema unabaki kujiuliza hivi hawa watu chupa zina pooza au ni kitu gani
njaaa zinawauma we fikiria miaka yote walikuwa na ofisi kwenye nyumba ya mtu na hawaogopi juzi wameingia mikocheni makazi mapya naona wamekumbuka uswahilini kwao
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ametangaza kuahirisha maandamano yaliyopangwa kuanza tarehe 23/9/2024 mbele ya waandishi wa habari katika mkutano wa TDC ili kupisha mazungumzo yatakayofanyika baina ya viongozi wa dini na Rais Samia.
Jambo jema.
 
Sahihi kabisa, yaani waliona 10yrs+ wote wafe leo hii, hawa walio chini wakikua huenda kukawa na jambo la kueleweka. Nchi hii shida sana.
Ukweli ni kwamba hata kama Mbowe na wafuasi wang’e andamana bado kusingetokea mabadiliko yoyote.
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ametangaza kuahirisha maandamano yaliyopangwa kuanza tarehe 23/9/2024 mbele ya waandishi wa habari katika mkutano wa TDC ili kupisha mazungumzo yatakayofanyika baina ya viongozi wa dini na Rais Samia.
Hapo dj anaposhindwa kucheza na bit anatukata mood
 
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe ametangaza kuahirisha maandamano yaliyopangwa kuanza tarehe 23/9/2024 mbele ya waandishi wa habari katika mkutano wa TDC ili kupisha mazungumzo yatakayofanyika baina ya viongozi wa dini na Rais Samia.
Nilipomsoma Mnyika asubuhi alivyobadili chorus kutoka maandamano kuwa uchaguzi, nikajuwa kwisha kazi yao hao.

Ni vema wameelewa kuwa moto wake si mchezo.

Vyovyote vile, hao watazamwe kwa ukaribu mno. Boniface kayatapika yote huko alipo.
 
Pumbaf
 
Akili zako ww bibi unazijuwa mwenyewe.
Mental retardation
 
Hapo ujue imeingia Bil 5 akaambiwa tulia mwenyekiti

ipo siku wengi wataelewa hili

Hakuna Upinzani halisi Tanzania

Upinzani aliondoka nao Mch. Christopher Mtikila

Bilioni Tano ulilipa wewe?. Huyo Mtikila alipokuwepo mlisema hivi hivi.
 
Nampongeza sana Mr. Chairman Mbowe.

Anavyozidi kuzeeka naona busara nayo inaongezeka.

Safi sana.
 
Back
Top Bottom