Well said mheshimiwa Chairman, lakini naomba unithibitishie kweli Chadema ni chama cha wananchi, nashtuka kusikia hii
statement, manake kama kweli Chadema ni chama chetu sote kwanini wakati mnafanya maamuzi yenu ya kimafia
hamkutaka hata japo kutujuza. Mkaamua kuua UKAWA halisi ambayo ilikuwa na maono na malengo halisi ya kuliokoa taifa
hili.
Mr. Chairman kwanini hiki chama mmewapa watu wengine ambao hata misingi na malengo ya chama hawayajui.
Mr. Chairman kwa jinsi nijuavyo Chadema kilikuwa mtari wa mbele kupinga ufisadi na kulikuwa na makamanda wakina Dr.
Slaa, ZZK, John Mnyika na wengine, lakini kwa nini sasa hivi hatusikii hata japo mkigusia tu ufisadi? na hata kuukemea.
Kwa jinsi mambo yanavyokwenda sasa ni wazi kabisa Chadema kimekuwa ni chama cha watu wachache, waliopumbaza
watanzania wengi kwa kauli mbiu ya mabadiliko. Watanzania wengi hasa vijana wanaonekana wazi kabisa kushindwa
kujitambua na kufuata tu makundi bila hata ya kupambanua mambo. Ni wazi ualisia wa Chadema umezidi kupotea.
#BRINGBACKOURCHADEMA