Udhaifu mkubwa mnakimbia kujibu issues badala yake mnajikita kwenye mambo binafsi, siasa hizi mnazidi kuonesha kwamba ubinafsi ndio umewajaa badala ya maslahi ya taifa. Kila mwanasiasa anataka kuonekana bora , badala ya kujikita kujenga nchi yetu.
chadema ishapoteza muelekeo ata ufisadi amuwez kuuzungumzia
Ukawa ni gari iliyo speed na haina kuchimba dawa, ukibanwa na haja ruka kutokea dirishani kama mzee slaa
Padri aliyeshindwa utumishi
Nilipita juzi maeneo ya Kariakoo nikaona wamachinga wamejaa jazba kama sio munkari au mhemko. Walikuwa wanasema, "Ukiweka gogo ligombee kwa tiketi ya UKAWA ligombee na mgombea wa CCM, sisi tualichagua gogo! Sisi kwa sasa ni Lowasa tu, hatuoni wala hatusikii lingine!" Nikaona kweli watu wamefika mbali.
Katika hali ya kuchoshwa na ubinafsi siasa za kibabe na kifalme ndani ya CCM.
Na maisha mabovu kwa nchi yetu ndani ya miaka 54 ya uhuru.
Leo hii hata Mbowe na Mbatia wakiondoka UkKAWA kwa njia yeyote ile.Iwe kama Slaa au Lipumba walivyoondoka,mimi nitaendelea kumwamini Lowassa mpaka mwisho wa shughuli na kura yangu nitampigia.
Kwa msisitizo hata wamnunue Lissu na Mnyika na ikatokea Sumaye akafanya kama Said Nkumba kura yangu kwa Babu Duni na Lowassa ipo pale pale.
Na huo ndio msimamo wangu, naombeni na wana mabadiliko wote tusimamie hilo kwa dhati kabisa.
Tusiyumbishwe MUSA atatuvusha.