Freeman Mbowe: CHADEMA kufanya Mikutano Nchi nzima kuanzia Mwezi wa nne. Bado tunahitaji kujua waliomuua Aquilina

Freeman Mbowe: CHADEMA kufanya Mikutano Nchi nzima kuanzia Mwezi wa nne. Bado tunahitaji kujua waliomuua Aquilina

Tatizo lenu wasomi ndani ya kikundi chenu mmewaweka pembeni mkatanguliza mihemuko mihemuko. Hotuba ya Mh. Mbowe haikuandaliwa kabisa na wala hakuhusisha wabobezi ili aongee nini zaidi ya hisia zake ndiyo maana kaishia kuropoka ropoka
hotuba ya mwenyekiti wenu huwa inaandaliwa na nani? mbona huwa anajiongelea tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wangalau sasa Mbowe anazungumza lugha inayoeleweka japo imechelewa. Better late than never. Hapo tutapata tume huru ya uchaguzi na katiba mpya. Ile lugha ya kutaka maridhiano ilikuwa ni lugha ya kimama na kweli ilinikwaza sana.
Tume huru haipigi kura, njooni tushindane kwa hoja.
 
kapiga para kabadilika...apa nawaza tu, ivi viongozi wote bila kujali chama wangenyoa para na midevuuu nani angekuwa na mvuto?
 
-"Subira yetu, uvumilivu wetu na upole wetu umedharauliwa vya kutosha. Kama watatumia polisi na magereza kutufunga wote, watufunge. Tuko tayari kwa lolote. Kama wanafikiri mabomu, risasi na jela ni suluhu, basi wakatumie," Mbowe, Mwenyekiti Chadema.
 
Kwanini April wakati anajua kuna tahadhari ya corona? Au ni techique ya kuifanya serikali ikiri kuwa corona ipo tz?
 
Hawa watu wangeachiwa tu wafanye mambo yao kwa uhuru mbona CCM imefanya mengi yameonekana. Kwahili la kuwaingilia hawa naona tu nikujiaribia sifa yao kwa wananchi.
Huwezi kuwaachia wapotoshaji, bana mbavu mpaka mwisho wahuni kabisa. Tz inahitaji sera mbadala za maendeleo na si kuhamasisha uvunjifu wa amani
 
-"Subira yetu, uvumilivu wetu na upole wetu umedharauliwa vya kutosha. Kama watatumia polisi na magereza kutufunga wote, watufunge. Tuko tayari kwa lolote. Kama wanafikiri mabomu, risasi na jela ni suluhu, basi wakatumie," Mbowe, Mwenyekiti Chadema.


Hayaa ndo maneno niliyokuwa nayasubiri kutoka kwa Mbowe muda mrefu.
 
"Subira yetu, uvumilivu wetu na upole wetu umedharauliwa vya kutosha. Kama watatumia polisi na magereza kutufunga wote, watufunge. Tuko tayari kwa lolote. Kama wanafikiri mabomu, risasi na jela ni suluhu, basi wakatumie," Mbowe, Mwenyekiti Chadema. MwanaHALISI Digital on Twitter
Mbowe ni bonge la muhuni, si unajua alishawahi kutoga masikio??? Wafuasi wake wana upungufu wa akili
 
Unajua bwana wakati mwingine mtu unashindwa kuelewa haya mambo yanafanyika kwa kusudi gani. Kwamba, ni chuki tu au ni nini hasa....??

Mathalani, kama katika tukio hili ni kweli Halima Mdee, Jeska Kishoa na Esta Bulaya na wengine walikuwa ni wavamizi wa gereza. Ni sawa kabisa....

Kisha ikapulizwa filimbi ya hatari ikiwa ni ishara kuwataarifu askari magereza wengine wote kuwa "gereza limevamiwa" ili wakabiliane na wavamizi. Ni sawa kabisa....

Haya, wakaja na kukusanyika palipo na uvamizi na wavamizi. Hawa wavamizi cha ajabu hawakukimbia. Wakiwa barabarani ndani ya magari yao halafu tena kumbe ni wanawake wakiwa hawana silaha yoyote hata kisu tu. Ni sawa kabisa.....

Labda sasa Gereza la Segerea wajibu maswali haya ili pengine ambao hatujaelewa tuweze kuamini wasemaje wa serikali na magereza;

1. Ikawaje tena wakaanza kuwashambulia hao wanawake kwa bunduki, mateke na mangumi huku wakiwa tayari wako mikononi mwao?

2. Hizo zinazosemwa kuwa ni sheria, zinaelekeza nini kifanyike? Je, ni mtuhumiwa kupigwa hata pengine kuuwawa hata kama yuko tayari mikononi mwa polisi?

3. Kwanini kama kweli walikuwa wamekiuka taratibu na sheria fulani fulani za magereza, ikawaje baada ya "kina mama hawa wavamizi" kuwa mikononi mwao wasingewatia ndani ya gereza moja kwa moja kwa usalama wao kisha utaratibu wa kuwachukulia hatua za sheria ukafanyika?

4. Au mnataka kutueleza kuwa sheria hizo za "Gari kugonga Gari moshi" la Magereza zinataka yeyote azivunjaye apokee kipigo cha lazima na cha haja na kisha atupwe kusikojulikana??

Mimi naweza kukubaliana na Freeman Mbowe kuwa hii "State organized crime" kuwalenga baadhi ya wanasiasa wa vyama mbadala wanaomkosoa na kumsumbua Rais Magufuli.....
 
Back
Top Bottom