Pre GE2025 Freeman Mbowe: CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea. Anayetaka kugombea tukutane kwenye sanduku la kura

Pre GE2025 Freeman Mbowe: CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea. Anayetaka kugombea tukutane kwenye sanduku la kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Bezecky

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2024
Posts
494
Reaction score
897
Wakati wowote kuanzia sasa Mhe Freeman Mbowe kutoa tamko rasmi la ama atagombea Uenyekiti wa CHADEMA ngazi ya Taifa ama laa.

Mtakumbuka Mhe Freeman Mbowe ameitumikia nafasi hii kwa zaidi ya miongo miwili sawa na miaka 21 mfululizo.

Endapo atatangaza kugombea tena atakuwa ni mgombea wa nne nyuma ya Tundu Lissu na Odero Odero,

Je, kama Taifa tunatarajia nini kutoka Upinzani kuelekea 2025?

Usiondoke hapa Jf kwa habari zaidi

=======================================

Siku ya leo Disemba 21, 2024 Freeman Mbowe ametangaza rasmi kugombea kwa mara nyingine nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA Taifa.

Mbowe amsema kuwa kutokana na Uchaguzi mkuu ambao unakuja si vyema kubadilisha "makamanda" na kwamba bado yupo sana kuongoza chama hicho na mara baada ya mkutano anaenda kuchaukua fomu kwenye makao makuu ya chama hicho, Mikocheni.

"Kwa kuzingatia yote haya na mengine mengi ambayo sitaki kuwachosha. Nilisema mara nyingi kuwa nilitamani kuondoka lakini siwezi kuondoka katikati ya minyukano iliyopo. Kwa hiyo CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea"





View: https://www.youtube.com/live/8WGa7Xv3hKo?si=JjooipgRmN035_2F
 
Wakati wowote kuanzia Sasa Freeman Mbowe kutoa tamko rasmi la ama anagombea ama laa.

Usiondoka hapa Jf kwa habari zaidi,






View: https://www.youtube.com/live/8WGa7Xv3hKo?si=JjooipgRmN035_2F

Lazima agombee tena
Leo ndio tutajua Mbowe ni mpinzani wa kweli au mamluki,

CHADEMA lazima ipasuke lazima,
Ukilijua lengo hasa la kuanzisha kwa vyama vya Upinzani hapa Tz mwaka 1992, utakuwa unajua wazi kabisa kwamba Mbowe hawezi kuacha kugombea Uenyekiti huko Chadema.
Viongozi wengi wa vyama vya upinzani ni Mapandikizi ya Tiss, ukianzia:- Augustine Lyatonga Mrema, Cheyo, Lipumba, Mabere Marando, na hata huyo FAM
 
Freeman Mbowe ataheshimika sana kama ataweka tamaa nyuma na kuachia kiti kwa heshima. Otherwise, Chama kitakosa legitimacy na moral authority ya kuwasema vibaya CCM

Siku zote tunapaswa kuyaishi tunaoyaongea na kuwahubiria wengine wafanye. Vipindi vinne vya uongozi totalling 20 good years inatosha kabisa na hizi kelele nyingine ni kelele za wenye njaa wanaofaidika na mfumo uliopo
 
Back
Top Bottom