Pre GE2025 Freeman Mbowe: CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea. Anayetaka kugombea tukutane kwenye sanduku la kura

Pre GE2025 Freeman Mbowe: CHADEMA nipo, nitakuwepo na nitagombea. Anayetaka kugombea tukutane kwenye sanduku la kura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
We tulia
Yani leo unawatuhumu wajumbe wanapewa rushwa na Abdul, kesho wajumbe haohao uwaombe kukupigia kura? Mwambieni Lisu cha kwa ajifunze kutokuwa mropokaji, na kuna vitu vya kweli pia hutakiwi kuongea public, hii ni kanuni ya maisha inamuhusu binadamu yeyote.

Ccm Lisu wanamchukulia kama chizi tu na hawapo tayari kufanyakazi na chizi, kamanadhani ccm haihusiki na uchaguzi wa Chadema mnajidanganya wenyewe, huyo Mbowe utakuta hata usalama wa Taifa ndio wameindorse agombee, wengi hamjui hii nchi inaendeshwaje.
Rushwa lazima kupigwa vita kwa gharama yoyote , anaeona lissu kukemea rushwa adharani ndani ya chama amefanya makosa ,atakua mpumbavu kiwango cha rami, chadema lazima kiwe kisafi ili kiwe na uwezo wa kuikemea ccm .

Wajumbe kwa sasa Tuleteeni lissu
 
Hii si ndio Golden chance ya kumuondowa Mbowe kupitia danduku la kura? Au mimi ndio sielewi?
Kama Mbowe yuko powerful hivi maana yake huyo ndio mtu sahihi, wakutane kwenye box namba zitaongea, hiyo ndio Demokrasia sasa, ccm mwenyekiti inatoka fomu moja tu na mapovu hayawatoki, sasa Chadema mmepewa fursa mumchaguwe mnayetaka mnaweweseka, binafsi siwaelewi.
Wote wagombee, uchaguzi ufanyike kwa uwazi na whoever wins washindwa wakubali matokea. It's all about democracy.
Machawa wa pande zote waache kulialia.
 
We tulia
Rushwa lazima kupigwa vita kwa gharama yoyote , anaeona lissu kukemea rushwa adharani ndani ya chama amefanya makosa ,atakua mpumbavu kiwango cha rami, chadema lazima kiwe kisafi ili kiwe na uwezo wa kuikemea ccm .

Wajumbe kwa sasa Tuleteeni lissu
Tofautisha Mropokaji na mkemeaji, Nyerere alikemea rushwa hadharani, hakuwa mropokaji.
 
Wewe ni muongo sana sijawahi kuona, Lisu hakuwa na Chama, harakati zake alianzia Nccr Mageuzi anapanda majukwaani kumbe hata kadi hana ndio akastuka akachukuwa kadi ya Nccr Mageuzi.

Lisu amejiunga na Chadema kuongeza nguvu miaka 10 na kitu tu iliyopita.

Siku nyingine usirudie kudanganya watu hadharani kwa ushabiki na chuki zako kwa Mbowe, au uliliwa na mwenyekiti hukupewa viti maalum?
Wakati Chacha Wangwe anataka kugombea uenyekiti.Lissu hakuwa Chadema? ILIKUWA MWAKA 2008.Ninakumbuka Lissu alimlalamikia sana Chacha Wangwe hadi kusema kamsaidia case nyingi mno.I wish niupate ule uzi niuperuzi.Lissu alikuwa upande wa Mbowe .
 
Mkuu amini nakwambia utashangaa, tunataka sasa sisi wanachama ambao hatupigi kura tuone na tujiridhishe kama patafanyika upumbavu kama huo na sisi tuna akili tutaamua cha kufanya, tusihukum kwanza ngoja tuvuke mto ,tunataka mshindi halali ,

Wajumbe pesa mkipewa tafuna ila tuleteeni hitaji letu kwa sasa
Umesahau alivyosema Lissu kuwa kwenye chaguzi za Chadema kuna pesa nyingi ambayo haifahamiki inatoka wapi.....wajumbe wa kamati Kuu kwa Hali ya uchumi ilivyo mtaani hao watanunuliwa wote na Abdul!
 
Njoo ccm sasa

Mimi sinaga chama labda kwa badae maana naona miyeyusho tu.
Si Simba si yanga.
Mimi naamini katika kimsingi ya haki, kweli, uadilifu, uwajibikaji, utu, usawa, competencies, uhuru wa fikra na mawazo katika kuchangia mada za maendeleo, challenges ( kukosoana kwa nią ya kujenga) na yenye kufanana na hayo .
Mtu mwenye kuwa na kuyafanya hayo sijali atakuwa wa chama gani nitamkubali tu sababu Katiba inaruhusu vyama vingi .
 
Mimi sinaga chama labda kwa badae maana naona miyeyusho tu.
Si Simba si yanga.
Mimi naamini katika kimsingi ya haki, kweli, uadilifu, uwajibikaji, competencies, uhuru wa fikra na mawazo katika kuchangia mada za maendeleo, challenges ( kukosoana kwa nią ya kujenga) na yenye kufanana na hayo .
Mtu mwenye kuwa na kuyafanya hayo sijali atakuwa wa chama gani nitamkubali tu sababu Katiba inaruhusu vyama vingi .
Yaani mtu anagombea kwa kura, nyie mnachanganyikiwa

Mnatakaje sasa ndugu wanachama😀
 
Back
Top Bottom